Hivi Magufuli tu ndio alikuwa katili au yeye alikuwa hawezi kung'ata na kupuliza? maana nakumbuka alivyofanywa Dr. Ulimboka kwenye utawala wa Kikwete ila sioni watu wakimzungumzia Kikwete kama katili.
Ulimboka alitumika na watu wenye uroho wa madaraka.
Walikua wanamtumia kutengeneza taharuki(corruption) ili Rais aliekuwepo kipindi kile ambae ni jk aonekane ni dhaifu na nchi ionekane imemshinda.
Ukumbuke kulikua na taharuki kila sehemu.
Migomo ya madaktari ,mgao wa umeme,mandaamano ya wanachuo,wafanyakazi kudai nyongeza, migomo ya madereva wa mabasi nk.
Hii ni mbinu ya kimapinduzi ya dunia ya sasa, yanaitwa mapinduzi ya kisiasa.
Mtu mmoja mwenye uwezo wa ushawishi na fedha anafanya ili kumpindua mwenzie.
Mbinu hii ya kimapinduz inafanywa baada ya ile ya kijeshi kuonekana ina vikwazo vingi kutoka kwenye jumuia za kimataifa.
Hivyo kwa wakati ule tushuru kulikua na usalama imala kujua vijana wa aina ya urimboka wanavyo tumika na kwakua jk alikua hapend zambi na kula damu za vijana wa aina ile,aliishia kuteswa tu ili wataje anaowatumia akishataja anaachwa.
NAKUHAKIKISHIA MITIHANI ALIEKUMBANA NAE JK KWENYE UTAWARA WAKE KWA WAKATI ULE ANGEKUA MAGU WANGEPOTEA WENGI.
Visa vile ndio vilivyomuondoa mzee wa rich.
Na naamini magu alikua muoga sana kuhusu haya mambo na ndiomaana hakutaka kusikia mtu yeyeyote kumkosoa maana aliethubutu kumkosoa alikiona chamoto kama sio kupote kabisa.