Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,207
- 17,674
Leo tarehe 14/6/2024 treni ya umeme (SGR)imeanza rasmi safari zake za Dar - Moro ambapo abiria 600 wamesafirishwa ambao ni sawa na mabasi 10!, abiria hao wametumia masaa mawili tu kufika Morogoro hivyo kuokoa muda na foleni barabarani. Mwezi wa saba tarehe 25 treni hiyo itaanza rasmi kwenda Dodoma hivyo kuendelea kuokoa muda zaidi na kupunguza foleni njiani.
Ikumbukwe wakati Rais wa awamu ya 5, Hayati Magufuli akiweka jiwe la msingi kuanza ujenzi wa reli ya umeme na bwawa la mwl Nyerere alitukanwa na kukejeliwa na Tundu Lisu, John Heche, na Chadema kwa ujumla kwamba hiyo miradi itakuwa white elephant na haitafika popote zaidi ya kuharibu hela za wananchi tu. Tunashukuru moyo wa Magufuli aliokuwa nao wa kutokata tamaa na sasa watanzania tunaona faida yake baada ya miradi hiyo kukamilika.
Vipi kama Magufuli angesikiliza matusi ya Chadema na kuamua kuachana na hiyo miradi, Leo tungeona hizi faida za kuisha kwa mgao wa umeme na kupungua kwa foleni Nyerere road?