Uchaguzi 2020 Mafanikio yaliyoletwa na Rais Magufuli yawaumiza kichwa wapinzani katika kampeni zao

Uchaguzi 2020 Mafanikio yaliyoletwa na Rais Magufuli yawaumiza kichwa wapinzani katika kampeni zao

Joined
Sep 8, 2020
Posts
67
Reaction score
133
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea na Kampeni katika mkoa wa Geita mabapo mbali na kuomba kura ameeleza mafanikio kadhaa yaliyopatikana katika mkoa huo huku akisisitiza katika kuleta maendeleo zaidi katika mkoa huo, haya ni baadhi ya aliyoyazungumza akiwa katika maeneo tofauti mkoani Geita leo Septemba 09, 2020

Katika sekta ya maji Serikali imetekeleza miradi mbalimbali ya maji na mji wa Geita umepangwa katika miradi mikubwa ya miji 28 itakayopatiwa maji ambapo mji wa Geita umetengewa shilingi bilioni 130.

Serikali imeongeza makusanyo ya Gawio kutoka Taasisi ambazo Serikali inazimiliki au ina hisa kutoka shilingi bilioni 161 mwaka 2014/2015 hadi shilingi tilioni 1.528 mwaka 2019/2020 kwa mwaka.

Serikali imefanikisha kupeleka umeme kwenye Vijiji 282 na kubakiza vijiji 116 tu. Kwa nchi nzima Serikali imepeleka umeme kwenye vijiji 9,570 na kubakiza takribani vijiji 2600. Kadhalika bei ya kuvuta umeme imeshuka hadi kufikia elfu 27 tu.

Katika Sekta ya Elimu Serikali imejenga madarasa 1,539 katika Mkoa wa Geita, Shule za Sekondari 27 na nyumba za walimu 162. Aidha imeleta takribani shilingi bilioni 35.3 ya elimu bila malipo.

Serikali imefanikiwa kuongeza makusanyo ya madini kutoka shilingi bililioni 160 hadi shilingi bilioni 528 mwaka 2019/2020. Kadhalika kuongeza makusanyo ya Halmashauri kutoka takribani shilingi bilioni 379 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 713.3 mwaka 2019/20.

Katika Sekta ya Madini, Serikali imeweza kudhibiti utoroshwaji wa Madini kwa kutunga Sheria ya kulinda rasilimali hiyo na kuanzisha Soko kubwa la Madini. Kabla ya hapo Madini mengi yalikuwa yakitoroshwa nje ya nchi, Serikali ilikuwa haipati chochote na wananchi hawakuweza kufaidika na chochote. Magufuli –Geita

Serikali imewawezesha wachimbaji wadogo wadogo kwa Kuwatengea maeneo, Kufuta au kupunguza viwango vya Kodi walizokuwa wakilipa, kuwapatia mafunzo na mitambo ya kuendesha shughuli zao za uchimbaji. Magufuli-Geita

Katika kipindi cha miaka mitano, Kumekuwa na ongezeko la mapato kwa wachimbaji wadogowadogo kutoka Mwaka 2016 ambapo waliuza dhahabu Kilo 337.482 yenye thamani ya shilingi bilioni 22.5 na kupelekea Serikali kupata Mrabaha wa shilingi bilioni 1.2 hadi kuuza dhahabu kilo 4,656.29 yenye thamani ya Bil 375.5 na kupelekea Serikali kupata Mrabaha wa shilingi bilioni 22.5 kwa mwaka 2019. Magufuli-Geita

Kumekuwa na ongezeko la mapato kwa Wachimbaji wakubwa. Mwaka 2016 waliuza dhahabu kilo 17,587.15 yenye thamani ya Dola za Marekani Mil 607.3 sawa na shilingi tilioni 1.4, Serikali ilipata Mrabaha wa thamani ya Dola za Kimarekani Mil 23.4 sawa na shilingi bilioni 53.81. Hadi mwezi Mei, Mwaka 2020 wameuza Kilo 21,652.77 zenye thamani ya Dola za Kimarekani Mil 949.8 sawa na shilingi tilioni 2.2 na kutoa Mrabaha wenye thamani ya Dola za Kimarekani mil 56.8 sawa na shilingi bilioni 130.64.

Katika kipindi kijacho Serikali imejipanga kutengeneza machinjio ya kisasa, kuendeleza na kujenga Maghala ya kuhifadhi Mazao na Vituo vya kuchakata. (Ilani ya Uchaguzi Uk 33-56).

[16:19, 09/09/2020] +255 762 525 411: Katika Sekta ya Miundombinu Kwa miaka mitano iliyopita Serikali imejenga barabara zenye viwango vya Lami Km 123.27 zenye thamani ya Shilingi Bil 212.67. Miaka Mitano ijayo Serikali imejipanga kujenga barabara za Lami nyingi zaidi ikiwemo kukamilisha barabara ya kutoka Geita- Bukori- Kahama. (Ilani ya Uchaguzi Uk 61-95). Magufuli-Mkoani Geita

[16:21, 09/09/2020] +255 762 525 411: Katika Sekta ya Afya Miaka Mitano iliyopita Serikali imeendeleza ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita. Aidha Serikali imejenga Hospitali nne za Wilaya. Magufuli-Mkoani Geita.
Ehdg76vXkAAJToJ.jpg
 
Kungekuwa na mafanikio yanayopendwa na wananchi tume na wakurugenzi wasingehangaika kutoa ushindi was mezani kwa ccm kamwe, wangewaachia wananchi waamue kupitia sanduku La kura.
 
Kichwa kinakuuma wewe kwani miaka mitano ya Jiwe watu wamekuwa mafukara haijawaji tokea.
mkuu usijekuta fukara uko peke yako, hizo kilo 4200kg za dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo unadhani hizo pesa ziko wapi? tatizo siku hizi yale mambo ya "unanijua mimi nani?" hayapo tena, watu wanatimba mikwanja kimyakimya.
 
Wataalam wa maendeleo ya watu na sio vitu,

Ndio maana wakaamua kubakia wapangaji tu mpaka leo.
 
mkuu usijekuta fukara uko peke yako, hizo kilo 4200kg za dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo unadhani hizo pesa ziko wapi? tatizo siku hizi yale mambo ya "unanijua mimi nani?" hayapo tena, watu wanatimba mikwanja kimyakimya.
Ni mjinga wa CCM tu ndiyo huamini takwimu fake na Jiwe.
 
Sami O,
Kichwa kinakuuma wewe kwani miaka mitano ya Jiwe watu wamekuwa mafukara haijawahi tokea.
Sema wewe ambae ulizoea kupata pesa bila kujishughulisha na ukiwa na matumizi makubwa,
Wanaofanya shughuli zao wanapata pesa sema ile ya matumizi ya hovyo ndio hakuna.
 
Nyonyoma kweli wewe ...umeenda huko Geita? Watu wanatumia maji ya lambo maji hayajulikani rangi!Hizo hossy zenyewe ziko mbali balaa....ukienda hata huduma za maana hakuna.. amewakuta na wenyewe wasukuma hawajijitambua thts y anabwbwaja tu km Linahara hivi.

Hizobkodi anazosema ametoa kwa wachimbaji wadogo ni zipi?akae walau siku moja mgodini aone watu wanavyolipishwa maushuru ya kisenge senge ..mxiew
 
Nyonyoma kweli wewe ...umeenda huko geita? Watu wanatumia maji ya lambo maji hayajulikani rangi!Hizo hossy zenyewe ziko mbali balaa....ukienda hata huduma za maana hakuna.. amewakuta na wenyewe wasukuma hawajijitambua thts y anabwbwaja tu km Linahara hivi...
Hizobkodi anazosema ametoa kwa wachimbaji wadogo ni zipi?akae walau siku moja mgodini aone watu wanavyolipishwa maushuru ya kisenge senge ..mxiew
mkuu hukumwona prof Mkumbo akichimba mtaro wa bomba mwenyewe? sasa ulitaka wasilipe kodi? nani alipe kodi?
 
Mwingine huyu! Mafanikio ya kuangusha uchumi, udhalimu, wizi na udikteta.
 
Ile sheria ya takwimu Ni kilio kwa jamii... Serikali unaweza kutoa takwimu za kubumba na hakuna atakaye pinga...
 
mkuu hukumwona prof Mkumbo akichimba mtaro wa bomba mwenyewe? sasa ulitaka wasilipe kodi? nani alipe kodi?

Uzi umesema ametoa Kodi nyingi kwa wachimbaji wadogo wadogo ndio nimeuliza kodi zipi hizo!? Kuna sehemu Kuna utitiri wa Kodi Kama migodini?

Kifupi hakuna lolote mbwembwe tu zaidi ya kuongeza masoko ya dhahabu
 
Uzi umesema ametoa Kodi nyingi kwa wachimbaji wadogo wadogo ndo nimeuliza kodi zipi hizo!? Kuna sehemu Kuna utitiri wa Kodi Kama migodini😏?
Kifupi hakuna lolote mbwembwe tu zaidi ya kuongeza masoko ya dhahabu
huo utitiri wa kodi hebu utaje, vinginevyo yatakuwa majungu, kama unasikiliza porojo za Lissu changanya na za kwako
 
Back
Top Bottom