Mafinga: Wazazi wasiopeleka chakula shuleni kukamatwa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wazazi ambao hawapeleki chakula Cha mchana katika shule za msingi kuchukuliwa hatua kwa mjibu wa Sheria na kushitakiwa kwa kutowajibika vema kwa Watoto wao.

Hayo yamejiri katika kikao cha dharula cha Wataalamu wa lishe wa mitaa sita ya kata ya Boma katika Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Julist Kisoma Diwani wa kata ya Boma ,amewataka Wataalamu wa lishe kushirikiana na kamati za shule kusimamia ulaji wa chakula na kufanya uchunguzi iwapo Wanafunzi wote wanakula chakula shuleni.

Bw. Salum Atlas Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji Mafinga, alisema kila shule inayo kamati ya chakula inayosimamia ulaji wa chakula hivyo ni suala la kushirikiana na Watendaji kuhakikisha kuwa wanaokiuka maagizo ya Serikali wanachukuliwa hatua.

Upande wake Bi. Anna Masoud Afisa mtendaji wa kata ya Boma, alisema azimio liliwekwa kuwa shule zinapofungua Wazazi wawe wamepeleka chakula na kama kuna watoto hawali shuleni sensa ifanyike na hatua
zichukuliwe kwa Wazazi.

Aidha Bi. Farida Saibati Kipangula Mwenyekiti wa Mtaa wa Malingumu,aliomba Uchunguzi ufanyike kwani Wanafunzi chakula wanachopewa hakilingani na fedha wanazotoa Wazazi .

Hata hivyo Bw. Isaack Ezekia Kilawa Mwenyekiti wa mtaa wa Ivambinungu na Bi.Josephine Kazikuboma Afisa mtendaji wa mtaa wa Mji Mwema waliomba muongozo wa kuwashughulikia Wazazi wajeuri na Wakolofi wasiopeleka chakula shuleni.
1741328931743.png
 
Wazazi ambao hawapeleki chakula Cha mchana katika shule za msingi kuchukuliwa hatua kwa mjibu wa Sheria na kushitakiwa kwa kutowajibika vema kwa Watoto wao.

Hayo yamejiri katika kikao cha dharula cha Wataalamu wa lishe wa mitaa sita ya kata ya Boma katika Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Julist Kisoma Diwani wa kata ya Boma ,amewataka Wataalamu wa lishe kushirikiana na kamati za shule kusimamia ulaji wa chakula na kufanya uchunguzi iwapo Wanafunzi wote wanakula chakula

shuleni.

Bw. Salum Atlas Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji Mafinga, alisema kila shule inayo kamati ya chakula inayosimamia ulaji wa chakula hivyo ni suala la kushirikiana na Watendaji kuhakikisha kuwa wanaokiuka maagizo ya Serikali wanachukuliwa hatua.

Upande wake Bi. Anna Masoud Afisa mtendaji wa kata ya Boma, alisema azimio liliwekwa kuwa shule zinapofungua Wazazi wawe wamepeleka chakula na kama kuna watoto hawali shuleni sensa ifanyike na hatua
zichukuliwe kwa Wazazi.

Aidha Bi. Farida Saibati Kipangula Mwenyekiti wa Mtaa wa Malingumu,aliomba Uchunguzi ufanyike kwani Wanafunzi chakula wanachopewa hakilingani na fedha wanazotoa Wazazi .

Hata hivyo Bw. Isaack Ezekia Kilawa Mwenyekiti wa mtaa wa Ivambinungu na Bi.Josephine Kazikuboma Afisa mtendaji wa mtaa wa Mji Mwema waliomba muongozo wa kuwashughulikia Wazazi wajeuri na Wakolofi wasiopeleka chakula shuleni.
View attachment 3262211
 
Attachments

  • 20250112_093956.jpg
    20250112_093956.jpg
    20.9 KB · Views: 1
  • Screenshot_20250213_083034_Instagram.jpg
    Screenshot_20250213_083034_Instagram.jpg
    446.2 KB · Views: 1
  • IMG-20250305-WA0007.jpg
    IMG-20250305-WA0007.jpg
    137.3 KB · Views: 1
  • IMG-20250303-WA0014.jpg
    IMG-20250303-WA0014.jpg
    38.4 KB · Views: 1
  • IMG-20250227-WA0032.jpg
    IMG-20250227-WA0032.jpg
    236.1 KB · Views: 1
  • IMG-20250225-WA0011.jpg
    IMG-20250225-WA0011.jpg
    49 KB · Views: 1
Sijaelewa kwani hao watoto wanaenda shuleni kusoma au kula?
 
Back
Top Bottom