Mafisadi wa Tanzania wazuiwa kuingia Marekani

Mafisadi wa Tanzania wazuiwa kuingia Marekani

wawataje majina basi tujue. kama kubwa la mafisadi Balali alikuwa na resident permit mpaka amezikwa huko hii kama sio danganya toto ?
 
kwani hivi ni vikwazo vya uchumi? wafungieni mpaka kikwete mwenyewe
 
Hawa Wamarekani hawana chochote, ni ma-opportunist tu na wanataka kumpa ujiko JK swahiba wao. Wangetuambia kuwa wanachumguz na watafunga akaunti zote za mafisisadi zilizomo kwenye Mabenki ya Kimarekani hapo ningesema kweli wanatupenda na wanamaanisha wanachosema.

Vinginevyo ni Wasanii tu, hawana kitu!
 
Wana majina hao????? waongo wakubwa kama wanayo watutajie basi kuwa fulani bin fulani ni fisadi tumemnyima visa wasitudanganye hawana lolote changa la macho tu

MAJINA MAJINA MAJINA TUNATAKA Mh. Balozi Green
 
Jamani hivi mmnasahau kuwa tumekwenda kwa ajiliya shopping!! MBONA MNAPENDA KUCHUNGUZA MAMBO YA WAKUBWA ADABU ZENU MMEZIWEKA WAPI, kwenu Baba akitokka mtoto anauliza kwanini BABA AMETOKA au baba ndiyo wakumuuliza MTOTO.


2010 ndio tutajua mbivu na mbichi... migomo iko mingi inakuja MUHIMBILI wamadanganya kwa laki moja ya ramadhani (IDD) na xmas.
WALIMU wamefoji majina
WAFANYAKAZI SERIKALINI tunachambua waliokufa ndipo tuwalipe
RELI ngoma mbichi haijakauka.

OMBI LANGU MOJA WANAJESHI NAO WAGOME TUONE JK NA MAFISADI WAKE WATAFANYAJE TENA WAUNGANE WOTE WAGOME SIKUMOJA
 
kama kweli mpango huu utafanyiwa kazi utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya wezi wa mafisadi.
lakini ni kweli marekani ipo tayari kuwakimbiza mafisadi na watoto wao ambao wanakuna fedha za masikini kwenye kila kona ya mareakani.

Tunawaona watoto wao wanavyokula fedha za walipa kodi kuanzia Houston Mpaka seatle, Dc mpaka Miami na sehemu mbali mbali za marekani.
haya kazi kwetu tuipeleke jamii forum homeland security na majina ya mafisadi na watoto wao. Wote warudi wakapambane na wananchi wenye hasira.
 
Wote warudi wakapambane na wananchi wenye hasira.

Kwa nini wasipambane na wewe kwani naona wewe pia inaonekana una hasira sana. Nakubaliana na wewe ikiwezekana warudishwe, lakini wewe uwatafute wote hawa "watoto wa vigogo" na kukabiliana nao sambamba kuanzia pale wanaposhuka kwenye pipa eapoti, au unasemaje?
 
Kwa nini wasipambane na wewe kwani naona wewe pia inaonekana una hasira sana. Nakubaliana na wewe ikiwezekana warudishwe, lakini wewe uwatafute wote hawa "watoto wa vigogo" na kukabiliana nao sambamba kuanzia pale wanaposhuka kwenye pipa eapoti, au unasemaje?

Why are you so NEGATIVE?
 
If anything, you may want to accuse me of being too real ...now what's up with that? You don't want to face plain reality Sir?

The reality is that you, him and me to do our bits. And that is what he said. That is the reality. What other reality are you talking about?
 
The reality is that you, him and me to do our bits. And that is what he said. That is the reality. What other reality are you talking about?

Exactly, its always easier said than done, and that's why I proposed that he/she lead the charge of purportedly "angry" hordes of Wananchi dying to get their hands on "mafisadi na watoto wao". Thats the kind of reality I'm referring to.
 
Exactly, its always easier said than done, and that's why I proposed that he/she lead the charge of purportedly "angry" hordes of Wananchi dying to get their hands on "mafisadi na watoto wao". Thats the kind of reality I'm referring to.

Anyway, let's do what we ought to or at least what we can, to effect justice and stop waiting for the lead.
 
Anyway, let's do what we ought to or at least what we can, to effect justice and stop waiting for the lead.


Talk is indeed very cheap, Sir, and it couldn't be much further from grand visions of a lynch mob of thousands of angry Wananchi waiting at the the airport for "mafisadi na watoto wao" to leave that plane so that they could rip off their limbs apart in a vicious fit of rage and kill them in an instant. Don't you think so?
 
Date::9/9/2008
Marekani yasubiri majina ya mafisadi toka serikali ya Tanzania
Na Kizitto Noya
Mwananchi

MAREKANI imesema inasubiri orodha ya mafisadi kutoka serikali ya Tanzania ili iwaingize kwenye orodha ya watu wanaotakiwa kuzuiwa kuingia ndani ya taifa hilo la Amerika Kaskazini.

Marekani, ambayo inasifika kama kinara wa demokrasia duniani na ambayo imekuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, juzi ilitangaza kuwa watu wote wanaojipatia fedha isivyo halali kwenye nchi zao, hawataruhusiwa kuingia nchini humo kwa shughuli za kibiashara, matembezi au kutafuna fedha hizo haramu.

Jana, msemaji wa ubalozi wa Marekani nchini, Jaffery Salaiz aliliambia gazeti hili kuwa kwa sasa nchi hiyo haina orodha ya mafisadi wa Tanzania na hivyo haiwezi kuwaingiza kwenye mpango huo mpya, lakini macho yake yanaelekezwa kwa watuhumiwa wa ufisadi wa EPA, Richmond na Rada.

Salaiz alisema hayo alipoulizwa na gazeti hili endapo Marekani imeshapata orodha ya mafisadi inaokusudia kuwazuia kuingia nchini humo kama sehemu ya utekelezaji wa tangazo namba PP7750 la Rais George W. Bush.

Alisema watuhumiwa wa ufisadi wa wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), utoaji wa zabuni kwa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond na ununuzi wa Rada wataingizwa katika orodha hiyo baada ya kuthibitika kuwa walishiriki katika vitendo vya ufisadi unaoathiri maslahi ya Marekani.

"Sasa hatuna orodha yao na hao wanaotuhumiwa kwa ufisadi wa EPA, Richmond na Rada wataingia kwenye orodha yetu baada ya mchakato unaoendelea sasa na kuthibitika kuwa walishiriki matendo ya ufisadi," alisema Salaiz.

Katika tangazo hilo la rais namba PP7750 Marekani pia imekusudia kuwafukuza maafisa wa serikali wanaotuhumiwa kwa ufisadi na ambao tayari wamewekeza nchini humo au kusafiri kwa ajili ya matumizi ya mali walizopata kinyume cha taratibu.

Marekani imekuwa ikionekana kama kiota cha mafisadi ambao hujichotea mamilioni ya fedha kwenye serikali za nchi changa na kutowekea kwenye taifa hilo kwa lengo la kuwekeza, kutembea au kuanza maisha mapya.

Balozi wa Marekani nchini, Mark Green alisema katika taarifa yake kuwa mafisadi wanaoomba na kupokea rushwa na hata wanaotumia madaraka yao vibaya, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao wanaofaidika na ufisadi huo, hawataruhusiwa kuingia Marekani.

Green alisema uamuzi huo ni tangazo jipya la rais na linawahusu maafisa wa umma na viongozi wa serikali wenye tabia ya kuomba na kupokea rushwa au kutumia madaraka yao vibaya kwa faida binafsi.

Kwa mujibu wa Balozi Green, marufuku hiyo ya kuingia Marekani pia inawahusu wachumba, watoto na wategemezi wa wafanyakazi wa sekta binafsi wenye tabia ya kuwahonga watendaji wa serikali na maafisa wa umma ili wafanye mambo kwa maslahi yao badala ya umma wanaoutumikia.

Alisema Marekani haitakubali kuwa kiota salama cha mafisadi na walarushwa na mpango huo mpya wa kuwazuia mafisadi kuingia nchini humo, umelenga kuieleza dunia kwamba Marekani iko makini katika suala hilo.

"Uwazi na vita dhidi ya ufisadi ni tunu za Marekani. Tunaendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania ili kung'oa mizizi ya ufisadi na kumpeleka mbele ya sheria mtu yoyote anayetuhumiwa na kubainika kushiriki matendo ya kifisadi," alisema Green katika taarifa yake.

Alisema mpango huo unawalenga watumishi walioshiriki ufisadi nchini mwao na kuathiri maslahi ya Marekani ambayo ni pamoja na shughuli za biashara za kimataifa na uchumi za nchi hiyo.

Green alitaja maslahi mengine ya Marekani yanayopaswa kulindwa kuwa ni malengo ya misaada yake kwa nchi husika, usalama wa nchi hiyo, ujenzi wa demokrasia na mambo yanayokiuka sheria mpya ya rushwa inayofanyika katika matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Mpango huo wa Marekani umeanza kuwa maarufu duniani baada ya kuanza kutekelezwa na karibu nchi zote zilizoendelea (G8) kama sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya nchi hizo yaliyofikiwa mwaka 2003.

Katika Mkutano huo wa Juni 2003, Rais George Bush wa Marekani na viongozi wengine wa nchi hizo walikubaliana kutoruhusu nchi zao kuwa kimbilio la Mafisadi kutoka nchi zinazoendelea.

Marekani na wenzake pia wamekubaliana kushirikiana na nchi zinazoendelea kuwatambua, kuwatafuta, kufuatilia mali za mafisadi na kuzikamata kisha kuzirudisha kwa wahusika na kuwafungulia mashtaka.

Hivi karibuni viongozi hao katika mkutano mwingine uliofanyika Hokkaido, walikubaliana kuendeleza ushirikiano huo unaoongozwa na Umoja wa Nchi za Amerika (OAS) na Jukwaa la Kiuchumi la Asia Pacific Cooperation (APEC)
 
Je, SIRI KALI itatayarisha list ya majina ya kweli ya mafisadi kama tunavyowajua Watanzania akina Fisadi Mkapa, Fisadi Lowassa, Fisadi Sumaye, Fisadi Rostam Azizi, Fisadi Chenge, Fisadi Karamagi, Fisadi Mramba, Fisadi Msabaha, Fisadi Hosea na mafisadi wengi kama wanavyojulikana na Watanzania? Au itatayarishwa list ya majina bandia na kukabidhiwa ubalozi wa Marekani?

Je, list ya majina ya mafisadi hao itawekwa hadharani ili na Watanzania pia tuione au itakuwa ni SIRI KALI? Au ombi hili la Balozi wa Marekani litadharauliwa kama lile la offer ya kumrudisha Ballali lilitolewa mwezi wa pili mwaka huu na JK hakusema lolote kuhusu offer iliyotolewa na Balozi wa US kumrudisha Ballali arudishwe Tanzania kwa msaada wa US ili ajibu tuhuma za ufisadi wa BoT dhidi yake. Tutege masikio.
 
Back
Top Bottom