Mafisadi watashinda! - A somber look

 
analysis nzuri !

Hata hivyo sina uhakika ni ushindi/mafanikio gani ambao ulitegemea hivi karibuni. Nadhani ni mapema mno tena sana, na hawa watu ili kuangushwa haitotokea ndani ya usiku mmoja, lakini ninachoweza kusema kazi ya kuufumua huu mtandano wa wahalifu imeshaanza lakini itachukua muda kuufumua wote. Akina zitto na dr slaa naweza kusema wamefanya waliyosema na kipande kilichobaki sasa ni kwetu sote.

Iwapo tunaamini elimu ( yaani ni uraia ) nayo itasaidia kuamsha akili za watz basi tukazane kuhimizana juu ya hilo. Hivyo ningependa nitofautiane na wewe kwamba mafisadi wanashinda. Hapana hawashindi isipokuwa wanajiweka vizuri, na huko kujiweka vizuri kwao inabidi "ITEGEMEE" kwa maana ya kwamba "WASIGEUKANE" na hiyo mipango yao iwe imesukwa "kweli kweli". Hata hivyo ninaamini there still will be a way through kuwaondoa.

No matter how difficult it is, i still see a shiny Tanzania within the next few years ! Yes i do, sio kwamba nasema tu, bali nuru ishaanza kuonekana angalau kupitia kwa watu wachache wenye uwezo wa kuthubutu kama wa akina Dr. Slaa ! Tusiangalie ni kiasi gani ya watu, wafanyabiashara, wanasiasa au mapadri wapo katika huo mtandao, BALI tuangalie Dr. Slaa wangapi tunaweza kuwa nao ili kulikomboa taifa !! Ukisema uuangalie huo mtandao, utaumiza kichwa bure !
*NB - kuna mafisadi nao washaanza kupiga kelele ili waonekane nao wanapinga ufisadi, yaani mafisadi washaanza kuingiza watu wao katika kundi safi ili kulidhoofisha. Wengi wa hawa ni wabunge, haina haja ya kuwataja nadhani wanafahamika !

Hakuna ugumu wowote katika kuubomoa huu mtandao, isipokuwa itahitaji muda na subira itahijika! Mambo ya Inside Information mkuu !

Kazi na Dawa wazee!
 
Last edited:

Hii imetulia mzee, tatizo lipo hapo vita dhidi ya ufisadi imegeuka kuwa chaka la watu kuwamaliza wenzao ( risasi kidole ) Mtu akitaka kugombea mahala utaambiwa kutumwa na kambi ya fulani ( mafisadi ) kummaliza fulani kwa sababu eti yeye anapinga mafisadi!
 
Kama mafisadi watashinda, kwa nini bado uko hapa? Ukistaajabu haya ya wapiganaji vita dhidi ya ufisadi....
 

Mara zote mwisho wa vita huwa ni mwanzo wa vita nyingine. Jambo kubwa ni kuendeleza mapambano(alluta continua).
Hata hizi dalili za uhuru wa kuzungumza haya yote ni dalili za ushindi katika mapambano kumbukeni hatukuwa na hii hali tuliyo nayo sasa.(joy comes in morning)tuko gizani/usiku lakini asubuhi inakuja.
Tusikate tamaa ninaimani hili vuguvugu hatimaye litazaa matunda iko siku.
 
Mafisadi hawatashinda - the bright side.

Mwanakijiji, you could be right but only up to a point - ukweli ulio wazi ni kuwa tumewabana. Kama mfa maji, wanachofanya sasa hivi ni kutapatapa - hebu shuhudia mwenyewe vituko vyao kulingana na hizi habari chache kutoka sehemu mbali mbali.


Ukisikia mafisadi kuchanganyikiwa ndiko huku na kamwe hatutakiwi kulegeza kibano kwa namna yoyote ile - hivi vitendo vinazidi kuwaumbua kwa kuzidi kuanika maovu yao. Mafisadi lazima wawe na muundo unaowaunganisha ambao ama ni chama, kundi, mtandao, umoja au jumuiya - huko ndiko kimbilio na maficho yao, nje ya hapo hawawezi kufanikiwa. Wananchi kwa ujumla wao wanaanza kuwaona kwa sura zao halisi na si kama zamani walipoweza kujificha nyuma ya slogans za aina ya amani, utulivu na mshikamano.

Lazima sasa tuelekeze nguvu zetu katika kufyeka hiki kichaka.Kila siku tunasonga mbele na kila hatua ni pigo kwa mafisadi kwa kuwa pole pole tunawavua nguo. Mpaka sasa tumefanikiwa kuwatoa kwenye suti zao na hivi sasa wameanza kugombania kipande cha kanga waweze kujisetiri kwa hatari ya kubaki uchi. Taratibu kanga inaanza kuchanika na muda si mrefu, kwa aibu, kila moja wao ataanza kutimua mbio kivyake akitafuta pa kujificha - uzuri ni kuwa kichaka chenyewe tuko kazini tunakifyeka kama kazi.
Hapana Mwanakijiji, hakika tutashinda​
Kimbilio la mafiasdi tusiliruhusu kuendelea kudumu
 

I like this one! tutashindaje though wakati the odds are stacked against us.. nyie subirini ya kesho na keshokutwa...
 

Hypothetically thinking. if JK does not return to power, in whatever means, will the situation be any better?
 
Mkuu FMES na Mzee Mwanakijiji,

Alichokisema Mwanakijiji.....niliki-highlight karibu miaka miwili iliyopita. Napenda kusisitiza tena ni vema kujua unapigana na nani na unapigania nini (we must reach a point inabidi tu-itemise hivi vitu)........hapo kati kati tumekuwa na maendeleo mazuri kiasi......ila kwa sasa tumeanza kujichanganya tena sisi wenyewe kwa wenyewe.......kwa sababu za UBINAFSI, UNDUGU, UDINI, URAFIKI nk.....bila ya kuweka haya mambo pembeni trust me HAKUNA KUMKOMA NYANI GILADI.............

kuna kitu kinaitwa "BLACK CRAB SYNDROME" ndiyo inayotusulubu sasa hivi hapa JF na hata kwenye System i.e. Serikalini.

THE ONLY DAWA,
FIGHT FROM BOTH ANGLES i.e FROM INSIDE and FROM OUTSIDE.......somewhere we will have to put a STOP.(step by step)........and that will be the begining of a FUNDAMENTAL CHANGE WE CAN BUILD UPON
 
hii vita ni ngumu sana, lakini tutashinda tena kwa kishindo. Kazi kubwa ni kila mmoja kuchagua upande halafu kuanza kuelimisha wananchi ni nini madhara ya wizi wa fedha za kodi. Na ningeshauri kutoa elimu sana kwa watoto wa primary na secondary, kuonisha maisha na viwango vya elimu wanazopata kuwa vinasababishwa na vitendo vya ufisadi. Kuendelea kuweka wazi familia zilizofaidika na vitendo vya kifisadi na kuonyesha wazi tunawachukia kwa matendo yao, kutoa hawa watu kwenye kumbukumbu ya nembo ya utumishi wa umma na kuwaweka kama watu na familia hatari kwa ustawi wa jamii.

Ni lazima kuweka kumbukumbu na za matukio ya aibu yaliyofanywa na mafisadi kwa majina yao.
Vita hii sio rahisi ni ngumu ushindi sio mrahisi. Mafisadi watashindwa ila kabla ya ushindi kutachimbika.
Kuelimisha watanzania kuwa hatuna amani na neno hili amani ni silaha ya mafisadi. hakuna amani kwani wananchi wengi wanakufa kwa wizi na utendaji wa mafisadi.

Na tukumbuke kuwa Fisadi namba moja ni raisi wa nchi kwani ndiye analea mafisadi. Fisadi namba mbili ni bunge la taznania kwani linashangilia mafisadi. Fisadi namba tatu ni mahaka kwani haitoa hukumu zinazofaa kwenye kesi za kifisadi.

Raisi anamamlaka makubwa sana anaweza kupunguza au kumaliza mafisadi kama yeye sio mmoja wao. anawateua majaji, usalama wa taifa, mkuu wa polisi, mkuu wa majeshi.
Ukiangali kwa undani teuzi hizi ndizo zilizofanya ufisadi , wafanyabiashara walibeba tu mikoba ya ufisadi sasa watu wa kwanza kuwasulubisha lazima wawe wao, tukianzia na mkuu wa kaya.

Nitapigana na ufisadi kwa nguvu zangu zote na sasa naanzia na JK.
 
siwezi kuwasaliti watz kwa kujiunga nao...tutapigana mpaka tunaenda kaburini.mzee mwanakijiji aluta......cont
 
Asante MMK kwa analysis yako.
Lakini nadhani hakuna sababu ya kufa moyo, mafisadi wamejijenga kwa muda mrefu na wana mizizi mirefu sasa, ambayo unapoingoa pia inabidi ingooke na mimiea mingeine mizuri. Lakini tukubaliane kuwa japo mafanikio katika kupigana na ufisadi hayajaonekana lakini angalao sasa wanafahamu kuwa vita ipo dhidi yao, na hii ni hatua nzuri.

Watoto wa MBWA WAMEFUNGUKA (PASUKA) MACHO, sasa hawawezi tena kuendelea kulala!
 
siwezi kuwasaliti watz kwa kujiunga nao...tutapigana mpaka tunaenda kaburini.mzee mwanakijiji aluta......cont

- Angalia usije ukasalitiwa na hao hao WaTZ kwa vitenge na fulana,kangha kabla ya pilau! We haya tu!

Respect.

FMES!
 
In his book, man’s search for meaning, Viktor E. Frankly said, I quote
"Don't aim at success - the more you aim at it and make it a target, the more you are going to miss it. For success, like happiness, cannot be pursued; it must ensue, and it only does so as the unintended side-effect of one's personal dedication to a cause greater than oneself or
as the by-product of one's surrender to a person other than oneself. Happiness must happen, and the same holds for success: you have to let it happen by not
caring about it. I want you to listen to what your conscience commands you to do and go on to carry it out to the best of your knowledge. Then you will live
to see that in the long run - in the long run, I say! -success will follow you precisely because you had forgotten to think of it."
MMKJ, huyu shetani atashindwa ila ni vita ambayo siyo ya siku moja au wiki kadhaa kama tunavyofikiri.
Tukumbuke uhuru ulichukua muda mrefu kuudai na kuupata toka kwa wakoloni. Ingekuwaje wazee wale wangekata tamaa? Tunajua vuguvugu la kuudai lilianzaje? Naamini wema utaushinda uovu. Ni kweli kabisa umafia upo Tanzania na kwa bahati mbaya unawanufaisha baadhi ya watu wanaoufanya wakidhani wanalisaidia Taifa. Kuna siku ipo yaja tutaona mabadiliko ya kweli tusikatee tamaa
 
hata wakinisaliti nitapigana kivyangu mkuu mpaka kijulikane
 
Ukiwa vitani hutakiwi kukata tamaa, kujua mbinu za adui yako ni success factor ya ushindi wako so Mwankijiji kama ushajua mbinu za hawa fisadi basi tujipange kutegua mitego yao nakuwashambulia zaidi.
 
It can be done! Play your part. Haya maneno ya miaka 48 iliyopita have more meaning today than at any other time.
 
Hypothetically thinking. if JK does not return to power, in whatever means, will the situation be any better?

It might push the leaders to be more aware of the people they lead. CCM never lost an election & no sitting president has ever lost a second term, if JK looses then that will be a big message sent by the people telling the leader that non of them are immune. Nadhani tatizo kubwa ni kwamba kuna baadhi ya viongozi wana jiona nothing can ever be done to them. If we do something to them then it will make them check their egos & inflated heads.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…