Mafisadi hawatashinda - the bright side.
Mwanakijiji, you could be right but only up to a point - ukweli ulio wazi ni kuwa tumewabana. Kama mfa maji, wanachofanya sasa hivi ni kutapatapa - hebu shuhudia mwenyewe vituko vyao kulingana na hizi habari chache kutoka sehemu mbali mbali.
Ukisikia mafisadi kuchanganyikiwa ndiko huku na kamwe hatutakiwi kulegeza kibano kwa namna yoyote ile - hivi vitendo vinazidi kuwaumbua kwa kuzidi kuanika maovu yao. Mafisadi lazima wawe na muundo unaowaunganisha ambao ama ni chama, kundi, mtandao, umoja au jumuiya - huko ndiko kimbilio na maficho yao, nje ya hapo hawawezi kufanikiwa. Wananchi kwa ujumla wao wanaanza kuwaona kwa sura zao halisi na si kama zamani walipoweza kujificha nyuma ya slogans za aina ya amani, utulivu na mshikamano.
Lazima sasa tuelekeze nguvu zetu katika kufyeka hiki kichaka.Kila siku tunasonga mbele na kila hatua ni pigo kwa mafisadi kwa kuwa pole pole tunawavua nguo. Mpaka sasa tumefanikiwa kuwatoa kwenye suti zao na hivi sasa wameanza kugombania kipande cha kanga waweze kujisetiri kwa hatari ya kubaki uchi. Taratibu kanga inaanza kuchanika na muda si mrefu, kwa aibu, kila moja wao ataanza kutimua mbio kivyake akitafuta pa kujificha - uzuri ni kuwa kichaka chenyewe tuko kazini tunakifyeka kama kazi.
Hapana Mwanakijiji, hakika tutashinda
Kimbilio la mafiasdi tusiliruhusu kuendelea kudumu