pole sana Sipo, unaweza kuniambia walikuambia una aleji na kitu gani? nakuuliza hivi kwani mimi pia niliwahi kupatwa na tatizo kama lako kwa takribani miako mitano hivi.na sasa nipo fit kabisa sisumbuliwi tena na mafua ya mara kwa mara.Unaweza kunipa historia yako kwa kifupi labda mafua ya likuanza kipindi gani na kabla ya hapo ulikuwa unasumbuliwa na ugonjwa gani?na weza kukupa njia nilizotumia mimi
mafua yanatokana na sababu nyingi sana na ni vizuri kujaribu kupata ufumbuzi wa daktari kama yanakusumbua kwa mda mrefu.mimi mwenyewe niliugua sana na sasa nashukuru mungu nimepona.kuna dawa za haina nyingi kuanzia vidonge mpaka za kunyunyizia kwenye mto au za kuweka vitone puani moja kwa moja.kuna hio ya kuweka vitone puani daktari aliniandikia ndio imetatua matatizo yangu.ninge kushauri urudi tena kwa daktari ambae ni bora zaidi hili wafanye uchunguzi wa kina na ujaribu dawa zingine.
Jamani jana sijaweza kabisa kulala, mafua yaliyoandamana na chafya yalinisummbua sana please, tusaidiane dawa
pole sana mkuu sipo,
kweli ukizungumzia mafua,hiyo ni kero kubwa kwani hupunguza utulivu wa mtu kwa kiasi kikubwa.
kutokana na maelezo yako ni kweli kuwa kuna uwezekano mkubwa sana mafua yako yanasababishwa na allergy ya vitu fulani ambavyo mara nyingi unakutana navyo hasa inawezekana kuwa vumbi na baridi ama vinywaji vya baridi,si rahisi kuwa mafua yako yanasababishwa na infection kwani kwa kawaida mafua yanayotokana na infection huwa hayadumu kwa muda muda mrefu hata bila ya dawa yoyote huweza kuondoka yenyewe.je kwako huna pets au wanyama wengine unaofuga?kama una mbwa,paka,sungura epuka kuwasogelea karibu kwani manyoya yao yanasumbua kwa wenye allergy.jitahidi pia kuwa makini zaidi na vumbi la ndani,hii inaweza kutokana na carpets,magodoro au mito unayotumia ikawa na vumbi ambalo katika hali ya kawaida si rahisi kuliona.epuka vinywaji baridi na baridi yenyewe,kunywa maji kwa wingi ila yasiwe ya baridi ni vema zaidi kama yatakuwa vuguvugu.naamini tatizo lako halihitaji sana matibabu ya dawa kwani allergy ni ngumu sana kuitibu kwa kumeza dawa bali dawa ni kuepuka allergens.kama ukiweza kuepuka allergens unakuwa na uhakika wa kupona tatizo lako kwa karibu 100%.Zaidi ya hapo nakushauri uonane na daktari kwa uchunguzi zaidi na ushauri kulingana na mazingira uliyopo.kila la kheri mkuu.
Pole Mkuu Sipo
Mafua yanakera pia sana tena hizo chafya ndo usiseme. Mwenyewe naamka kila siku na mafua pia aleji na vitu kadhaa kama manukato makali,vumbi na spices za vyakula.
Nilikuwa natumia sana piriton, nimetumia celestamine,nimechemsha maji na kuweka nusu ndoo na kujifungia bafuni ili kupata mvuke kwa wingi vilevile nimelowesha kitambaa kwa maji ya moto na kuweka kwenye paji la uso mpaka puani..
Zote hizo hazijasaidia na mafua daily sikosi..Chafya ninafanya mpaka kichwa kiwe kinauma..Naishia kuwa na handkerchief kibao,yakianza nijifute tu ila sinywi dawa siku hizi kabisaa.
Hope Tutapata mwangaza kupitia wataalam hapa, pole sana Sipo!..
Kuna dada alisumbuliwa na mafua tulipokuwa kidato cha 5 mpaka cha 6. Na kabla ya hapo alisema kuwa alikuwa nayo. Alitumia dawa tofauti tofauti (sizikumbuki labda nimtafute), lakini Mafua yake yaliisha aliposhauriwa yafuatayo na Daktari mmoja.
Moja, kila akilala alalae na nguo, hasa inayofunika sehemu ya kifua. Hata kama kuna joto, manake aliambiwa asubuhi kunakuwa na baridi ambayo yeye atahisi ni ndogo na hata jifunika shuka, lakini inamuathiri (alikuwa anaishi Dar).
Pili, anywe maji vuguvugu, na aepukane na maji, juice (sharubati) ama vinywaji vyovyote baridi.
Tatu, asioge maji baridi hata kama kuna joto. Muda wowote akitaka kuoga aoge na maji moto (vuguvugu).
Nne, ajihadhari vitu vinavyotoa vumbi ama moshi (hii ilimsaidia shuleni hakupangwa kwa vitu hivyo).
Ninavyokumbuka kwa kuwa Daktari aliyomshauri hayo hakumpa dawa yoyote, yule dada alimdharau yule Daktari. Lakini aliamua kujaribu hayo aliyoambiwa. Baada ya siku chache mafua yakaanza kuondoka, na hadi nilipoonana naye baada ya kumaliza shule alikuwa hana tena hayo Mafua.
Nakushauri jaribu kufuata hayo mambo niliyoandika, na pia ufuate na waliokushauri wengine. Lakini muhimu ni kuwaona wataalamu wa afya. Lakini nahisi sijakumbuka yote ila kwa uchache nimekumbuka.
Mola akupe nafuu haraka na POLE.
pia nasikia kuwa vitunguu saumu vinasaidia sana. hebu jaribu kila wakati wa kulala usugue nyao zako vizuri na kisha upake urojo wa vitunguu saumu kwenye nyao zote, itaweza kusaidia kupunguza au kuondoa tatizo