Mafundi bomba (plumbers)

Mafundi bomba (plumbers)

Mzee wa kupambania

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2022
Posts
21,111
Reaction score
53,092
Naona mafundi bomba huku mtaani wengi bado wanapenda kujenga hizi chemba za kawaida (inspection chambers) katika mfumo wa maji taka wa nyumba (drainage system)

Kama upo kwenye ujenzi, utajenga au ulishajenga tuna kitu cha kujifunza katika mfumo huu wa maji taka nimeulewa sana

Kitaalamu mfumo huu unaitwa rodding eye drainage system. Faida yake;

(1) Mfumo huu unampa mwenye nyumba eneo kubwa la kufanya shughuli zake

(2) Hauingizi wala kufuga mende

(3) Unaongeza zaidi mvuto na mwonekano wa nyumba

(4) Unadumu kwa muda mrefu

(5) Haurudishi harufu

Screenshot_20221213-123127_Instagram.jpg


Screenshot_20221213-123149_Instagram.jpg





HAPA KABLA YA KUWEKA PAVING BLOCKS

Screenshot_20221213-080408_Instagram.jpg


BAADA YA KUWEKA PAVING BLOCKS 😍
Screenshot_20221213-080457_Instagram.jpg


👆Piga picha hapo ingekuwa zimewekwa chemba za kujengea zingekuwa ngapi na hako kanjia usingeweza kupita kwa uhuru au kupitisha vitu👇
Screenshot_20221213-080446_Instagram.jpg
 
Hii sojawah kuiskia, asante kwa madini
Poapoa mkuu

Hii iko poa sana nimeipenda, inapendezesha sana mazingira na mvuto wa nyumba tofauti na zile chemba za kujengea

Na unakuwa na nafasi ya kutumia vizuri uwanja wa nyumba yako
 
Vipi hiyo plastic ya chemba ikipigwa na jua muda mrefu haiwezi kupasuka.

Km wewe ni fundi weka namba. Au km una mjua mtaalamu wa hii kitu tupia mawasiliano yake
 
Vipi hiyo plastic ya chemba ikipigwa na jua muda mrefu haiwezi kupasuka.

Km wewe ni fundi weka namba. Au km una mjua mtaalamu wa hii kitu tupia mawasiliano yake
Mimi sio fundi ila fundi bomba alinielekeza kuhusu huo mfumo akanipeleka pale Nabaki Afrika tukanunua vifaa vyote.

Hiyo plastic ni ngumu sana hata gari ikanyage haivunjiki ilikanyaga fuso double ikiwa na mchanga mfuniko haukuvunjika
 
Back
Top Bottom