PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Mafundi garage wa kitanzania wana mchango mkubwa sana katika kuyatia ubovu magari ya watu. Mafundi hawa ni wazuri sana kwenye kujipigia promo na kuwaharibia waliofanya uwekezaji mkubwa.
Utakuta fundi anawachambua yale magereji makubwa yakiwemo ya wachina na wakorea kwamba wale hamna kitu kabisa, hawatengenezi bali hununua na kufunga vifaa vipya.
Au wakati mwingine wanakuonyeshea jamaa anayepita kwenye hizo garage akiyza wiper, utasikia umemuona yule jamaa amepita na begi la waipa? Basi huyo ndiyo wachina wote hapa mjini wanamtegemea kusuka engine za magari yao.
Ukijichanganya ukawapa kazi hawa mafundi, basi tarajia gari kuua kifaa kingine, au vifaa kunyofolewa, gari kuanza kubadili milio n.k
Ukitaka kupaka rangi wataponda kwa nguvu zote watu wenye vifaa vya kisasa na kuanza kusifiana wao huku mitaani, paka rangi kwao sasa, miezi minne mingi gari imeshafubaa inaanza kukudai upya.
Wengine kwenda kutengeneza gari kwao inabidi uwe na fundi mwungine utakayekua una muuliza kama asemacho fundi huyu ni kweli na mara nyingi huishia kusagiana kunguni. Ukilaza gari ndiyo uhesabu umeisha. Kupaka rangi tu unalazimika kusubiria gari ikauke, ukiwaachia tu wanapita na masega.
Wito wangu kwa mafundi wa kibongo ni kwamba. Acheni gubu kwa wenzenu waliowekeza. Na nyie ikibidi unganeni muanze kufanya mambo ya kueleweka.
Mna mislead sana watu na kuwatia hasara. Mtu mpaka anahisi kuwa na gari isiyo na shida haiwezekani. Maana ukitengeneza kwao na gari ika misbehave wanakwambia gari yoyote ukitaka kujua kama ni nzima ni lazima iwe hivyo
Mpaka watu wanaogopa kununua gari isiyo na shida, wanahisi labda hiyo ndiyo feki.
Ifike mahali jifunzeni kuboresha mazingira ya kazi zenu. Pia muache udokozi wa vifaa kwenye magari ya watu.