Mafundi makochi Mungu anawaona!

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Unakuta kochi limemaliziwa vizuri linang'aa na kitambaa safi cha nguo, turubahi, au ngozi. Utadhani limetengenezewa Ulaya! Utapigwa hela ndefu seti 1.5million mpaka 5m. Sasa lipeleke nyumbani watoto waanze michezo yao! Utasikia mara ndani mbao zinaanza kukatika mara ukikaa unadumbukia kwenye uwazi/ shimo ndani ya miezi sita magodoro kama chapati na kuacha ngozi tipwatipwa kama ngozi ya mzee!

Niliwahi kununua makochi ya mnada pale British council Mitaa ya Posta huu mwaka wa 7 bado safi kama mapya nikiyasafisha na kuyapiga dawa fulani hivi ya kusafishia siti za gari.

Kwanini mafundi wa kiswahili mnashindwa kuwa wabunifu na kujiharibia soko? Nenda stoo za watengeneza makochi utakuta kochi kama lisiponunuliwa litaharibikia nyanga nyanga hapo hapo showroom bila hata kutumika kwa kuoza au kuliwa na mchwa kutokana na mambao chakavu wanayotumia.

Mafundi makochi badilikeni!! Mnashindwaje hata kuchukua/ kununua kochi moja la mtansha/mzungu mkadesa kalitengenezaje? Nenda hata pale 'Danube' Mlimani City chunguza yalivyotengenezwa na nyie tengenezeni hivyohivyo! Vinginevyo njaa zitawauma na kuwafichua hadi uvunguni.
 
Tatizo ni kwamba nyinyi hamfiki bei , una pesa ya tecno ila unataka kitu chenye ubora wa Iphone, haipo hiyo mkuu

Ninasema hivyo kwasabu nina ofisi ya furniture , chini ya mil 2.. Huwez pata sofa ya uhakika wa kudumu walau miaka 5 na kuendelea mwenye mil 1 atapata bidhaa ya mil 1.. Mwenye mil 3 atapata bidhaa ya mil 3, iko hvyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hili Sio kweli kabisa, mafundi wengi walaghai, wanajua kupiga Kiswahili tantatarila.

Wameniingiza mkenge majuzi tu bado nina hasira, wanaamini wateja tunaishia kwenye display tu... hata mteja akitoa pesa uitakayo bado utafinyanga malapulapu tu kwa ndani kisha kuremba finishing.
 
5m hapana aisee sofa ninunua mwisho 1m tuuu
Sofa (imported from Turkey/USA/UK) mbona zinaenda hadi 15mil? Ziko safi quality 100% zimetengenezwa kwa manyoya ya kondoo na spring na chuma kisichopata kutu na kunakishiwa na layer isiyokwaruzika!

Jaribu kutembea! Ukikalia kweli unasikia umeketi na utasikia mwili mwepesi kochi limechukua uzito wa mwili wako na kuubalance! Ama kweli ndo maana matajiri ufikiri hawatakufa kwa raha za mali na vitu!

Muraaaa! Tafuta hela!
 
Sio fundi, sio mmiliki wa ofisi ya furniture wala hujawahi kua mfanya biashara wa furniture , ila unambishia alieko ndani ya industry ...

Sofa imara ukitaka fungua mfuko , ila bei za kuunga unga hizo sijui mil , lazima tu yakukute ... Kitambaa chanye afadhali ni elfu 12 mita moja , vitambaa vya maana ni 25/30 elfu sasa imagine sofa ya watu saba hamna hamna ile mita 30... Spring pair mona ni elfu 20, pair saba n bei gani ??.. Hujanunua godoro , ukitaka dodoma za maana , za inch mbili tu sehemu ya kuegemea , ambazo sio chini ya 7 pia , moja inakwenda kwa elfu 28... Bado siti, bado frame , bado fiber n.k

Hapo bado pesa ya ufundi, bado faida ..

Alafu mtu anaona 1.5mil kama pesa kuubwa... Hao danube wanakuuzia sofa mil 5... Kuna mil 3 imekatika kwenye kutengeneza ... Makodi kodi na faida ndio yanafikisha huko kwenye mil 5

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu unataka hiyo hiyo hapa nyumban kwa mil 1.5 kweli ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…