Mafundi makochi Mungu anawaona!

Mafundi makochi Mungu anawaona!

Sio fundi, sio mmiliki wa ofisi ya furniture wala hujawahi kua mfanya biashara wa furniture , ila unambishia alieko ndani ya industry ...

Sofa imara ukitaka fungua mfuko , ila bei za kuunga unga hizo sijui mil , lazima tu yakukute ... Kitambaa chanye afadhali ni elfu 12 mita moja , vitambaa vya maana ni 25/30 elfu sasa imagine sofa ya watu saba hamna hamna ile mita 30... Spring pair mona ni elfu 20, pair saba n bei gani ??.. Hujanunua godoro , ukitaka dodoma za maana , za inch mbili tu sehemu ya kuegemea , ambazo sio chini ya 7 pia , moja inakwenda kwa elfu 28... Bado siti, bado frame , bado fiber n.k

Hapo bado pesa ya ufundi, bado faida ..

Alafu mtu anaona 1.5mil kama pesa kuubwa... Hao danube wanakuuzia sofa mil 5... Kuna mil 3 imekatika kwenye kutengeneza ... Makodi kodi na faida ndio yanafikisha huko kwenye mil 5

Sent using Jamii Forums mobile app
Boss mimi ni fundi seremala. Najua unachokiongea wateja ndio shida wala sio mafundi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
But nmeona Quality centre wanasofa standard Bei 1.5 Hadi 2mil
 
Mimi niliisha apa kuwa sitanunua "tenga la nyanya" lililofunikwa vizuri na kitambaa na kuwa kochi. Nitaendelea kukalia mninga wangu na kubadilisha mito tu.
Unakuta kochi limemaliziwa vizuri linang'aa na kitambaa safi cha nguo, turubahi, au ngozi. Utadhani limetengenezewa Ulaya! Utapigwa hela ndefu seti 1.5million mpaka 5m. Sasa lipeleke nyumbani watoto waanze michezo yao! Utasikia mara ndani mbao zinaanza kukatika mara ukikaa unadumbukia kwenye uwazi/ shimo ndani ya miezi sita magodoro kama chapati na kuacha ngozi tipwatipwa kama ngozi ya mzee!

Niliwahi kununua makochi ya mnada pale British council Mitaa ya Posta huu mwaka wa 7 bado safi kama mapya nikiyasafisha na kuyapiga dawa fulani hivi ya kusafishia siti za gari.

Kwanini mafundi wa kiswahili mnashindwa kuwa wabunifu na kujiharibia soko? Nenda stoo za watengeneza makochi utakuta kochi kama lisiponunuliwa litaharibikia nyanga nyanga hapo hapo showroom bila hata kutumika kwa kuoza au kuliwa na mchwa kutokana na mambao chakavu wanayotumia.

Mafundi makochi badilikeni!! Mnashindwaje hata kuchukua/ kununua kochi moja la mtansha/mzungu mkadesa kalitengenezaje? Nenda hata pale 'Danube' Mlimani City chunguza yalivyotengenezwa na nyie tengenezeni hivyohivyo! Vinginevyo njaa zitawauma na kuwafichua hadi uvunguni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio wote. Me sofa zangu nafanya kubadilisha kitambaa tu na pale ninapotaka style mpya. Fundi wangu yupo tanga sabasaba pembeni ya tanga pazuri Ana center kubwa kiasi anaitwa Benjamin makoko. Huwa naingia gharama za usafiri za kuniletea popote nilipo maana huwa sikai Tanga.
 
Mkuu umeandika kwa spidi na hasira, tuambie taratibu...pointi zako za maana
Sio fundi, sio mmiliki wa ofisi ya furniture wala hujawahi kua mfanya biashara wa furniture , ila unambishia alieko ndani ya industry ...

Sofa imara ukitaka fungua mfuko , ila bei za kuunga unga hizo sijui mil , lazima tu yakukute ... Kitambaa chanye afadhali ni elfu 12 mita moja , vitambaa vya maana ni 25/30 elfu sasa imagine sofa ya watu saba hamna hamna ile mita 30... Spring pair mona ni elfu 20, pair saba n bei gani ??.. Hujanunua godoro , ukitaka dodoma za maana , za inch mbili tu sehemu ya kuegemea , ambazo sio chini ya 7 pia , moja inakwenda kwa elfu 28... Bado siti, bado frame , bado fiber n.k

Hapo bado pesa ya ufundi, bado faida ..

Alafu mtu anaona 1.5mil kama pesa kuubwa... Hao danube wanakuuzia sofa mil 5... Kuna mil 3 imekatika kwenye kutengeneza ... Makodi kodi na faida ndio yanafikisha huko kwenye mil 5

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana! Tengenezea nyumbani kuacha kulipa kodi ya pango tutakufuata! Kuna magodoro Dodoma hayasinyai! Sio mpaka manyoya ya kondoo! Hata kama utaniuzia 1.5mil angalau lidumu miaka kadhaa linisogeze
Yani ni limit ukuaj wa biashara yangu kwasababu ya mtu mmoja or wawil ?

Lakn kingine pia mkuu, usidhan labda kila mtu kajenga au kapanda nyumba za lak tano kwenda mbele kwamba utakua na eneo la kufanya kila kitu .. Tunatengeneza kila kitu sio sofa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sofa (imported from Turkey/USA/UK) mbona zinaenda hadi 15mil? Ziko safi quality 100% zimetengenezwa kwa manyoya ya kondoo na spring na chuma kisichopata kutu na kunakishiwa na layer isiyokwaruzika! Jaribu kutembea! Ukikalia kweli unasikia umeketi na utasikia mwili mwepesi kochi limechukua uzito wa mwili wako na kuubalance! Ama kweli ndo maana matajiri ufikiri hawatakufa kwa raha za mali na vitu!
Muraaaa! Tafuta hela!!!
Wewe ulianza story yako kwa ku refer mafundi wa hapa bongo, ndio maana wadau wakakushangaa kwa kutaja hiyo bei ya 5ml
 
Kuna dogo alikuwa anaoa!, washikaji tukajipanga tumtafutie zawadi ya kama M 2 hadi M3...washikaj wakatoa wazo wamtafutie makochi,kuna jamaa huwa anaagiza used kutoka UK,kabla ya kufanya maamuzi tukmwambia mwana,zawadi itakuwa makochi,hela itayobaki tutakukabidhi....jamaa akagoma,akadai tumkabidhi mpunga akachague mwenyewe....tukamkabidhi kama M 2.5....Baada ya kama mwezi tukaenda kumcheki duu makochi yashakuwa lonya na nyang'anyang'a...
 
Hayo ni yale ta mlopoo ya bei chee.

Sofa nzuri gharama.
 
Back
Top Bottom