Mafundi makochi Mungu anawaona!

Mafundi makochi Mungu anawaona!

Nnaona umeamua kujipigia promo
Sio wote. Me sofa zangu nafanya kubadilisha kitambaa tu na pale ninapotaka style mpya. Fundi wangu yupo tanga sabasaba pembeni ya tanga pazuri Ana center kubwa kiasi anaitwa Benjamin makoko. Huwa naingia gharama za usafiri za kuniletea popote nilipo maana huwa sikai Tanga.
 
Mtakufa kwa laana na njaa sasa maana mnazingua
Ndugu yangu Kama siku ikitokea ukamuona fundi amekufa njaa naomba unitafute kwa gharama yoyote.
Na hakuna laana yoyote juu ya ufundi ya moja kwa moja.
 
Wananunua magodoro yaliochakaa na kuyatumia
. Kuna anko wangu alinunua godoro likawa linanuka mkojo.
Unakuta kochi limemaliziwa vizuri linang'aa na kitambaa safi cha nguo, turubahi, au ngozi. Utadhani limetengenezewa Ulaya! Utapigwa hela ndefu seti 1.5million mpaka 5m. Sasa lipeleke nyumbani watoto waanze michezo yao! Utasikia mara ndani mbao zinaanza kukatika mara ukikaa unadumbukia kwenye uwazi/ shimo ndani ya miezi sita magodoro kama chapati na kuacha ngozi tipwatipwa kama ngozi ya mzee!

Niliwahi kununua makochi ya mnada pale British council Mitaa ya Posta huu mwaka wa 7 bado safi kama mapya nikiyasafisha na kuyapiga dawa fulani hivi ya kusafishia siti za gari.

Kwanini mafundi wa kiswahili mnashindwa kuwa wabunifu na kujiharibia soko? Nenda stoo za watengeneza makochi utakuta kochi kama lisiponunuliwa litaharibikia nyanga nyanga hapo hapo showroom bila hata kutumika kwa kuoza au kuliwa na mchwa kutokana na mambao chakavu wanayotumia.

Mafundi makochi badilikeni!! Mnashindwaje hata kuchukua/ kununua kochi moja la mtansha/mzungu mkadesa kalitengenezaje? Nenda hata pale 'Danube' Mlimani City chunguza yalivyotengenezwa na nyie tengenezeni hivyohivyo! Vinginevyo njaa zitawauma na kuwafichua hadi uvunguni.
 
Dunia kote utengenezaji wa masofa ni mmoja
Kikubwa kwenye sofa ni godoro ndani liwekwe
Imara na ngumu,fundi apige stepler sjui punch
Vizuri,kitamba kiwe imara na kizuri

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Unakuta kochi limemaliziwa vizuri linang'aa na kitambaa safi cha nguo, turubahi, au ngozi. Utadhani limetengenezewa Ulaya! Utapigwa hela ndefu seti 1.5million mpaka 5m. Sasa lipeleke nyumbani watoto waanze michezo yao! Utasikia mara ndani mbao zinaanza kukatika mara ukikaa unadumbukia kwenye uwazi/ shimo ndani ya miezi sita magodoro kama chapati na kuacha ngozi tipwatipwa kama ngozi ya mzee!

Niliwahi kununua makochi ya mnada pale British council Mitaa ya Posta huu mwaka wa 7 bado safi kama mapya nikiyasafisha na kuyapiga dawa fulani hivi ya kusafishia siti za gari.

Kwanini mafundi wa kiswahili mnashindwa kuwa wabunifu na kujiharibia soko? Nenda stoo za watengeneza makochi utakuta kochi kama lisiponunuliwa litaharibikia nyanga nyanga hapo hapo showroom bila hata kutumika kwa kuoza au kuliwa na mchwa kutokana na mambao chakavu wanayotumia.

Mafundi makochi badilikeni!! Mnashindwaje hata kuchukua/ kununua kochi moja la mtansha/mzungu mkadesa kalitengenezaje? Nenda hata pale 'Danube' Mlimani City chunguza yalivyotengenezwa na nyie tengenezeni hivyohivyo! Vinginevyo njaa zitawauma na kuwafichua hadi uvunguni.
Mafundi wetu sawa na Mainjinia wetu, uvhuzi duni saaaana
 
Sio fundi, sio mmiliki wa ofisi ya furniture wala hujawahi kua mfanya biashara wa furniture , ila unambishia alieko ndani ya industry ...

Sofa imara ukitaka fungua mfuko , ila bei za kuunga unga hizo sijui mil , lazima tu yakukute ... Kitambaa chanye afadhali ni elfu 12 mita moja , vitambaa vya maana ni 25/30 elfu sasa imagine sofa ya watu saba hamna hamna ile mita 30... Spring pair mona ni elfu 20, pair saba n bei gani ??.. Hujanunua godoro , ukitaka dodoma za maana , za inch mbili tu sehemu ya kuegemea , ambazo sio chini ya 7 pia , moja inakwenda kwa elfu 28... Bado siti, bado frame , bado fiber n.k

Hapo bado pesa ya ufundi, bado faida ..

Alafu mtu anaona 1.5mil kama pesa kuubwa... Hao danube wanakuuzia sofa mil 5... Kuna mil 3 imekatika kwenye kutengeneza ... Makodi kodi na faida ndio yanafikisha huko kwenye mil 5

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mngepewa hizo hela bado hamna ujuzi wa kutengeneza vitu quality. Mashinezemyeqe za kufanyia kazi hamna
 
Inawezekana! Tengenezea nyumbani kuacha kulipa kodi ya pango tutakufuata! Kuna magodoro Dodoma hayasinyai! Sio mpaka manyoya ya kondoo! Hata kama utaniuzia 1.5mil angalau lidumu miaka kadhaa linisogeze
Hawa jamaa huokoteza vijiti na misimari afu wanagonga, hata kilemba hawawezi
 
Tatizo ni kwamba nyinyi hamfiki bei , una pesa ya tecno ila unataka kitu chenye ubora wa Iphone..haipo hiyo mkuu

Ninasema hivyo kwasabu nina ofisi ya furniture , chini ya mil 2.. Huwez pata sofa ya uhakika wa kudumu walau miaka 5 na kuendelea ...mwenye mil 1 atapata bidhaa ya mil 1.. Mwenye mil 3 atapata bidhaa ya mil 3 ... Iko hvyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Aaa tajiri kama tajiri.
DanPol kama Danpol.
Die hard fan [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Iwe mvua iwe jua lazima wakuelewe.
 
Ukitaka sofa nzuri muite fundi akutengenee nyumbani kwako,material ya vifaa uvitakavyo unanunua mwenyewe
Ndo kitu nilichofanya hiki, na masofa bado mapya kabisa mwaka wa tano[emoji848]
 
Kuna sofa zilinunuliwa nje toka 2006 hadi leo zipo swafi kabisa, zingine 2010 had leo nikienda home bado zipo.

Zangu 2016 ila hazitamaniki, mara mbao zimekatika, mara zibonyee
 
Back
Top Bottom