Mafundi wa ujenzi wa nyumba njooni mnipe mawazo na mimi niwape kazi

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari,

Kama nina nyumba ya kawaida tu siyo ghorofa na sitaki kuibomoa ila mahali hapo hapo nataka juu ya nyumba hii nijenge nyumba nyingine ambayo haitategemezwa na nyumba hii ya zamani kiasi hata hii ya chini ikichakaa sana na kubomoka ile ya juu itasimama bado.

Watalaamu wa ujenzi nijuzeni uwezekano huu. Nasubiri.
 
1098049_185352481641304_759462040_n.jpg
 
Ni ngumu hiyo mkuu, kuwezekana ni ngumu sana.
Hapo kwa lugha rahisi tunaweza kusema ni kama umevaa shati fulani unalipenda sana, sasa unataka uvae shati lingine tofauti kwa juu yake na bado unataka hilo shati la ndani liendelee kuonekana.
Ngumu kidogo hiyo "shee wangu"
 
Hivi haiwezekani kuweka nguzo ndefu nne imara halafu juu anafunika kwa zege Au ni lazima pawepo na nguzo katikati
 
Thanks lakini najua inawezekans labds shida ni ufundi. Shukrani sana angalau kwa kuelewa maelezo yangu.
 
Habari,

Kama nina nyumba ya kawaida tu siyo ghorofa na sitaki kuibomoa ila mahali hapo hapo nataka juu ya nyumba hii nijenge nyumba nyingine ambayo haitategemezwa na nyumba hii ya zamani kiasi hata hii ya chini ikichakaa sana na kubomoka ile ya juu itasimama bado.

Watalaamu wa ujenzi nijuzeni uwezekano huu. Nasubiri.
Mkuu hilo swali siyo la mafundi bali ni la structure engineer.
Inawezekana ila baadhi ya kuta za zamani itabidi zife ili ku accommodate nguzo/columns na ngazi.
Ni gharama kubwa sana utakayo ingia kwa kutekeleza wazo lako kwani hiyo nyumba ya chini haitakuwa na huusuani na nyumba ya juu hivyo kupelekea hiyo design mpya iwe na span kubwa ya ku-transfer load na kupelekea iwe sawa na design ya 5 floors kwa just a single floor
 
Mkuu haiwezekani kuweka supporting polls za kutosha na kuweka platform inayoweza kusimamisha nyumba?
Hela yake utaiweza mkuu?
Maana kitu unachotaka wewe ni kama milioni 500 unaizika kwa ajili ya kuweka mazingira ya kupata sehemu ya kuweka nyumba juu, hapo bado hujajenga nyumba yenyewe.
Kwahiyo ni kiitu ambacho inakuwa ni upotezaji wa pesa.
 
Mkuu hilo swali siyo la mafundi bali ni la structure engineer.
Inawezekana ila baadhi ya kuta za zamani itabidi zife ili ku accommodate nguzo/columns na ngazi.
Ni gharama kubwa sana utakayo ingia kwa kutekeleza wazo lako kwani hiyo nyumba ya chini haitakuwa na huusuani na nyumba ya juu hivyo kupelekea hiyo design mpya iwe na span kubwa ya ku-transfer load na kupelekea iwe sawa na design ya 5 floors kwa just a single floor
Wazo lake litawezekana akiwa na zaidi ya mil 500.
 
Habari,

Kama nina nyumba ya kawaida tu siyo ghorofa na sitaki kuibomoa ila mahali hapo hapo nataka juu ya nyumba hii nijenge nyumba nyingine ambayo haitategemezwa na nyumba hii ya zamani kiasi hata hii ya chini ikichakaa sana na kubomoka ile ya juu itasimama bado.

Watalaamu wa ujenzi nijuzeni uwezekano huu. Nasubiri.
Haiwezekani, ingekuwa ni Load-Bearing Building ingewezekana lakini kwa hapo haiwezekani. Load Bearing ni kama yale majengo yanayojengwa mjini (ghorofa ambazo kuta zake hazibebi mzigo bali zinakaa tu kama kizuizi, mzigo wa jengo unabebwa na slab kwenda kwenye beam, beam kwenda kwenye column, column kwenda kwenye base na base kwenda kwenye udongo). Kama inawezekana vunja uanze upya kujenga msingi imara wenye nguzo
 
Hivi haiwezekani kuweka nguzo ndefu nne imara halafu juu anafunika kwa zege Au ni lazima pawepo na nguzo katikati
Nguzo imara lakini zitakaa mbalimbali sana, hivyo zitahitaji utegemezi katikati.

Idea ya jamaa inawezekana ila tu baadhi ya sehemu sa nyumba ya chini itabidi abomoe kuweka nguzo ambazo msingi wake unajichimbia zaidi kuliko msingi wa nyumba ya kawaida
 
Inawezekana kabisa kufanya au kutengeneza unachotaka, hata hiyo nyumba yako waweza toa paa na ukaweza ka gorofa hapo juu.

Ingia YouTube andika tinny houses utapata design nyingi, au tafuta hii channel YouTube " living big in a tinny house "

Utanishukuru
 
Back
Top Bottom