Mafundi wengi ni wababaishaji nifanyeje?

Mafundi wengi ni wababaishaji nifanyeje?

The silenter

Member
Joined
May 19, 2018
Posts
18
Reaction score
10
Wakuu habari za majukumu ya kila siku. Nimepata shida sana napopeleka gari iwe ni service au Normal maintanance ya kubadili spea. Nashangaa nikienda garage badala ya gari kupona nakuta mafundi kwa uzembe wanazalisha tatizo jingine hapo hapo.

Na wengine wamejaliwa maneno sana yaaani utamuamini tu. Anakupa sababu kiabao kama vile anajua tatizo kumbe wapiiiiiiii.........!

Yaani sijui nifanyeje kupata permanent solution ya hii shida. Nipeni mawazo jamani......!
 
Mafundi pasua kichwa...wangu aliniambia break pads 85,000 (2pcs) nimeenda kariakoo....livingstone str...mwenyewe nimepata zilezile (genuine) kwa 15,000 (2pcs).
 
Dah...wajinga ndiyo waliwao..... Bei ya vipuri hutegemea na ubora.... Mfano mkanda wa kompresa Toyota Lc V8 ni laki na nusu....ila IPO ya buku8 utakayo tumia wiki mbili tu...badala ya miaka 2.....8000 x 56 = 448,000/- uchaguzi ni wako.....
 
Garage gani nzuri na ya ku aminika Arusha, hawa wa mtaani nimewachoka ,wamenitia hasara vya kutosha.
 
Dah...wajinga ndiyo waliwao..... Bei ya vipuri hutegemea na ubora.... Mfano mkanda wa kompresa Toyota Lc V8 ni laki na nusu....ila IPO ya buku8 utakayo tumia wiki mbili tu...badala ya miaka 2.....8000 x 56 = 448,000/- uchaguzi ni wako.....
Kumbe una akili mbali na rohombaya teh jokin..
Kimsingi bei za spea zinategemea ubora, sio kila genuine ni genuine.
Jambo lingine la msingi usipende kupeleka gari service kwa kigezo cha service charge ati fundi flani ni cheap bali zingatia uwezo wa fundi.
Peleka gari gereji yenye hadhi na ubora hata likitokea tatizo watawajibika na sio fundi wa mtaani
 
Wakuu habari za majukum ya kila siku. Nimepata shida sana napo peleka gari iwe ni service au Normal maintanance ya kubadili spea. Nashangaa nikienda garage badala ya gari kupona nakuta mafundi kwa uzembe wanazalisha tatizo jingine hapo hapo. Na wengine wamejaliwa maneno sana yaaani utamuamini tu. Anakupa sababu kiabao kama vile anajua tatizo kumbe wapiiiiiiii.........!
Yaani sijui nifanyeje kupata permanent solution ya hii shida. Nipen mawazo jamani......!
upo mkoa gani mimi ni technician kitengo cha umeme wa magari
 
Dah...wajinga ndiyo waliwao..... Bei ya vipuri hutegemea na ubora.... Mfano mkanda wa kompresa Toyota Lc V8 ni laki na nusu....ila IPO ya buku8 utakayo tumia wiki mbili tu...badala ya miaka 2.....8000 x 56 = 448,000/- uchaguzi ni wako.....
kuweka maji kwenye spea sio ishu. ishu ni kwamba unaenda tengeneza kumbe unazidi kununua ugonjwa mwingine mpya.....!
 
upo mkoa gani mimi ni technician kitengo cha umeme wa magari
Nipo Mbeya town hapa.......!
Yaani hivi navyoongea tayari fundi kasha ua booster ya kushoto ya taa za mbele. Kisa kawasha taa bila kuchomeka ile taa ya booster kwa hiyo imekula spark moja tu kwisha habar. Sasa nawaza tena booster mpya wakati ishu ilikuwa kubadili taa tu. Na booster used ya spacio new model sijui ni ngapi aisee
 
daaah pole sana ndugu jaribu kutafuta fundi mwenye uzoefu wa umeme wa magari atakusaidia mimi nipo MOROGORO
 
Hizi mnazoita garage kubwa ni jina tu. Spare parts wanaenda nunua madukani na kuongeza bei.
Ukipata fundi mzuri kanunue vifaa mwenyewe Toyota au Kisangani au MasterCard zote ziko msimbazi
 
Huenda unatengenezea pale december kwa vibaka
mkuu umegusa pabaya....hawa mafundi wa December si mafundi...miaka minne iliyopta walitaka waniunguzie gari...
ilikuwa hivi...
Nilinunua fog lamps nifunge kwenye kanissan note kangu...pale pale wakati wanafunga nikawa na mashaka eti fundi kawasha taa huku anamenya waya fyuzi ukakata...wakaunga fyuzi hiyo na waya kumbe ule waya ni mnene....siku chache baadaye pale walipounganisha zile fog lamp pakapiga shoti ile fyuzi waliyounga na waya mnene ikagoma kukata....kilichotikea niona moshi unapanda kwenye dash board..taa zote za gari zikagoma kuwaka...nikatoa betri nikamwita fundi waya wa kueleweka tukakuta bando la waya kama nyaya ishirini hivi urefu wa kama mita 1 zimeungua na kugandiana..basi tukasuka waya upya..
Kuanzia hapi gari langu haliguswi na kibaka anayejiita fundi..
Kuna fundi mwingine aliwahi kuninunulisha spea ya bei ghali kumbe spea hiyo ilikuwa haijaharibika..
Hawa mafundi wa kubahatisha we acha tu..Kwa sasa nina fundi wangu anaitwa Four Angle angalau huyu namuamini ila namsimamia na si kumwachia gari.
Bongo mafundi wa magari ya kisasa hakuna..kuna wagonga nyundo.
 
Pale Mwenge/itv mafundi wengi vibaka ukizubaa unabadilishiwa spea original wanakufungia feki. Kuna utapel wa ajabu
 
Back
Top Bottom