Don't miss the point, Confucius alifundisha upendo wa kijamii unaoenda kwa ngazi yaani uipende familia yako kwanza, kisha marafiki, na mwisho jamii. Ni upendo wa kiwango cha ubinadamu wa kawaida.
Yesu alileta radical concept ya upendo wa kiungu, alisema wapendeni maadui zenu. Confucius mwenyewe kwenye Analects alipoulizwa kuhusu kulipa ubaya kwa wema, alisema lipa ubaya kwa haki/hukumu na wema ulipwe kwa wema. Yesu akapindua meza hapo kwa kusema lipa ubaya kwa wema wa hali ya juu. Hapa ndipo penye utofauti mkubwa.