Mafundisho makuu ya Yesu aliyofundisha ni yapi ?

Mafundisho makuu aliyofundisha Yesu mwenyewe mfano wa mafundisho ya akina Budha au Confucius ambayo ni ya kipekee (unique) yeye akiwa kama muasisi wake ni yapi ?
Unaamini Yesu ni mwana wa Mungi?
 
Hata hivyo mafundisho ya Yesu ambayo huweza kuchukuliwa kama yakipekee

1. Wapendeni Adui zenu na waombeeni wanaowaudhi.

2. Mtu akitaka kuwa wa kwanza, atakuwa wa mwisho wa wote, na mtumishi wa wote.— Marko 9:35.
 
Mafundisho ya upendo yalifundishwa na Confucius miaka 500 kabla yake
Don't miss the point, Confucius alifundisha upendo wa kijamii unaoenda kwa ngazi yaani uipende familia yako kwanza, kisha marafiki, na mwisho jamii. Ni upendo wa kiwango cha ubinadamu wa kawaida.

Yesu alileta radical concept ya upendo wa kiungu, alisema wapendeni maadui zenu. Confucius mwenyewe kwenye Analects alipoulizwa kuhusu kulipa ubaya kwa wema, alisema lipa ubaya kwa haki/hukumu na wema ulipwe kwa wema. Yesu akapindua meza hapo kwa kusema lipa ubaya kwa wema wa hali ya juu. Hapa ndipo penye utofauti mkubwa.
 
Acha ngonjera
 
"Vya kaisari mpe kaisari na vya Mungu mpe Mungu". Msemo kuntu Sana huu.
 
Hiyo haikuwa chanamoto yangu sana.Isipokuwa,iweje mtu mwenye akili timamu aende kanisani halafu hana imani na wala si mfuasi wa muanzisha kanisa?Utata.

😆😀😂

Mimi naenda nikiwa na mambo mengine mkuu

Kuna jumuiya. Kuna biashara. Na wengi wanaoenda kwaajili ya imani kama unavyosema wewe.

Kwani wachungaji na baadhi ya manabii huenda kanisani kusali au kwa imani ya Yesu au wanaenda kwa sababu ile ni kazi au biashara kama zilivyobiashara zingine?
 
Hiyo haikuwa chanamoto yangu sana.Isipokuwa,iweje mtu mwenye akili timamu aende kanisani halafu hana imani na wala si mfuasi wa muanzisha kanisa?Utata.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa raia wengi wanaoitwa Wakristo nchi za Ulaya hasa Scandaniva, wengi wamebaki kwenda kanisani kama sehemu ya kujumuika tu kijamii katika matukio muhimu mfano ndoa na mazishi.
 
Hayo mafundisho yake ya uamsho wa kiroho wa ndani ni yapi ?
Uamsho wa kiroho wa ndani katika mafundisho ya Yesu ni mabadiliko ya kina ya mtazamo, nia, na tabia ya moyo wa mtu ambapo mtu anazaliwa upya kiroho, badala ya kutegemea tu taratibu za nje za dini au sheria.

Yesu alifafanua hili vizuri alipozungumza na Nikodemo akasema mtu lazima "azaliwe mara ya pili" (kuzaliwa kwa maji na kwa Roho) ili kuona ufalme wa Mungu (Yohana 3:3-5).

Wakati mafundisho mengi ya kimaadili yanalenga kurekebisha matendo ya nje ya binadamu ili jamii iwe na amani, Yesu alisisitiza kuwa jamii haiwezi kuwa njema mpaka kwanza moyo wa mtu binafsi utakapopata uzima mpya kutoka kwa Mungu — hilo ndilo linafanya uamsho huu kuwa wa ndani na wa kipekee
 
Kuna watu walikuwa wanafundisha kupenda/kuwajali maadui kabla Yesu hajaja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…