Mafunzo kwa Askari wa Kike Afrika yafunguliwa Jijini Abuja, Nigeria

Mafunzo kwa Askari wa Kike Afrika yafunguliwa Jijini Abuja, Nigeria

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mafunzo kwa Askari wa kike ukanda wa Afrika IAWP yamefunguliwa leo Julai 02 katika kituo cha Rasilimali ya Polisi Abuja Nchini Nigeria ambapo mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo askari wa kike ukanda wa Afrika na wasimamizi wa sheria.

Akiongea leo Jijini Abuja Nchini Nigeria katika ufunguzi wa mafunzo hayo rais wa shirikisho la askari wakike Duniani Dkt. Leah Shibambo’s ameshukuru shirikisho la wakuu wa Polisi kwa namna ambavyo wakuwa na agenda za kuongeza nafasi za wanawake katika ajira na mgawanyo wa majukumu.
WhatsApp Image 2024-07-02 at 21.13.24_e6372ebe.jpg

WhatsApp Image 2024-07-02 at 21.13.25_fe263795.jpg

WhatsApp Image 2024-07-02 at 21.13.30_38121fe6.jpg

Ameongeza kuwa kitendo cha wakuu hao wa Polisi kuwa na agenda za kuwaweza na kujengea uwezo wanawake imeongeza kujiamini kwa kundi hilo katika utekelezaji wa majukumu yao huku ikileta matokeo Chanya katika kutoa huduma bora katika jamii.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Nigeria IGP Phd Kayode Egbetokun amesema kuwajengea uwezo askari wakike umewasaidia na kufanya askari hao kujituma katika kazi na kujiamini kitendo kilicholeta matokeo Chanya katika jamii huku akibaisha kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati sahihi ambapo dunia imejikita katika usawa wa kijinsia.

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi kutoka Nchini Tanzania Dkt SACP Debora Magiligimba ambaye ni mjumbe kutoka Tanzania anayeongoza Kanda ya ishiriki na moja ya nchi za SADC amebainsha kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuongeza ufanisi katika kazi zao za kila siku.

Mrakibu wa Idara ya Uhamiaji kutoka Nchini Ghana SI Doris Hajiman amebainisha kuwa maandalizi ya mafunzo hayo ni mazuri huku akiwapongeza waandaji wa mafunzo hayo ambao Nchi ya Nigeria.
WhatsApp Image 2024-07-02 at 21.13.26_c1dd0543.jpg

WhatsApp Image 2024-07-02 at 14.26.36_f97c9ceb.jpg

WhatsApp Image 2024-07-02 at 14.26.39_dd376e73.jpg
 
Back
Top Bottom