Mafunzo ya EQUIP ni majanga kwa walimu vijijini

Mafunzo ya EQUIP ni majanga kwa walimu vijijini

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
234
Mradi huu ambao uko katika mikoa minane hapa nchini umeanza kwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa wadau anuwai kwa mikoa hiyo; lakini mradi huu unaonekana kama unafanya maigizo vile.

Mfano walimu wanaopata mafunzo vijijini wanalipwa Tsh 17,500/- kwa siku. Malipo hayo yanajumuisha Nauli, Chai, Chakula cha mchana na jioni na Malazi. Ni kwa vipi kiwango hicho kinaweza kukidhi mahitaji kwa mwalimu anayesafiri kwa zaidi ya km 10 kama si majanga kwa walimu,?

Endapo mfadhili wa EQUIP yuko serious na uboreshaji wa elimu kweli ajaribu kuliangalia hili kwa walimu wanaopewa mafunzo vijijini.! Inakatisha tamaa mwalimu kuanza kutumia gharama zake kwa shughuli ambayo hakuipangia bajeti.
 
Unaendeshwa na shirika gan? Na nani wafadhili wake ni watu gan?
Jamaa wanafuata guidelines ya serikali kwenye ulipaj wa perdiem.
 
Naomba nieleweshe maana ya EQUIP. Halafu mbona inaeleweka wazi kila mtumishi analipwa kutoka manispaa au halmashauri atokayo huwa wanaita perdm au night iweje hao walimu wakubali kulipwa tofauti na utaratibu unaeweka?
 
Nadhan hyo itakuwa ni half perdiem ya wilayani kwa rate ya hao waalimu. Unaweza kuta full perdiem yao ni 35000 kwa wilayani
 
Pinno huenda usemacho ndicho, but how comes, je walilubaliana? Walimu wanatumika vibaya Nchi hii bado uchaguzi mkuu 2015
 
Naomba nieleweshe maana ya EQUIP. Halafu mbona inaeleweka wazi kila mtumishi analipwa kutoka manispaa au halmashauri atokayo huwa wanaita perdm au night iweje hao walimu wakubali kulipwa tofauti na utaratibu unaeweka?

EQUIP = Education Quality Improvement Programme (in Tanzania) yaani Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu (Tanzania).
 
EQUIP = Education Quality Improvement Programme (in Tanzania) yaani Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu (Tanzania).

Quality improvement inaanzia wapi mpaka wapi??!!!
Weaknesses ni zipi kwa existing quality??!!
Hiyo improvement wameongeza na kwenye mtaala mama ili wanaotoka wawe na hiyo added quality??!!
 
Quality improvement inaanzia wapi mpaka wapi??!!!
Weaknesses ni zipi kwa existing quality??!!
Hiyo improvement wameongeza na kwenye mtaala mama ili wanaotoka wawe na hiyo added quality??!!

Weakness on existing quality ipo katika nyanja tofauti, unaweza kuona katika uwezeshaji katika learning and teaching materials hiyo moja la pili katika mtaala kwamba curriculum is not relevant to our environment, na lingine pia linaweza kuwa kutowajali wawezeshaji wa huo mtaala, naishia hapa kwa sasa kuwachia wengine nafasi ya kuchangia ahsante
 
It is more of policy and institutions than agents at implementation level then. . .. . . !!!
 
Mradi huu ambao uko katika mikoa minane hapa nchini umeanza kwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa wadau anuwai kwa mikoa hiyo; lakini mradi huu unaonekana kama unafanya maigizo vile. Mfano walimu wanaopata mafunzo vijijini wanalipwa Tsh 17,500/- kwa siku. Malipo hayo yanajumuisha Nauli, Chai, Chakula cha mchana na jioni na Malazi. Ni kwa vipi kiwango hicho kinaweza kukidhi mahitaji kwa mwalimu anayesafiri kwa zaidi ya km 10 kama si majanga kwa walimu,? Endapo mfadhili wa EQUIP yuko serious na uboreshaji wa elimu kweli ajaribu kuliangalia hili kwa walimu wanaopewa mafunzo vijijini.! Inakatisha tamaa mwalimu kuanza kutumia gharama zake kwa shughuli ambayo hakuipangia bajeti.

Huenda hicho kiwango cha EQUIP. Sidhani kama ni sahihi kuwalalamikia EQUIP. Kama kiwango hakitoshi, ninadhani Halmashauri ya Wilaya/Wizara husika ndio wa kuwaeleza ili wachangie. Ni ushauri tu!
 
Back
Top Bottom