Mafunzo ya jeshi

Mafunzo ya jeshi

Lastmost

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2022
Posts
802
Reaction score
919
Habari za muda wakuu.
Naomba kwa yeyote anayeweza saidia ktk hili asaidie.
Baada ya majina ya vijana watakaoenda jeshini kutoka,watu waliyapokea kwa namna tofauti.
Wapo waliofurahi,na wapo ambao waliapa kutokwenda.
Mimi kijana wangu ambaye yuko chuo Cha ualimu( special diploma) alifurahi Sana na kutamani kwenda.
Ila baada ya siku kadhaa leo wametaarifiwa kuwa hawatakwenda jeshini Ila wataendelea na masomo mwezi wa Saba.
Kijana anaingia mwaka wa tatu hapo mwezi wa Saba na ndio mwaka wake wa mwisho.
Jee Kuna uwezekano akishamaliza chuo kwenda jeshini km wenzake wa kidato Cha sita wanavyokwenda.?
Na jee Ni tatatibu zipi anatakuwa azifate ili mwakani akimaliza chuo aende jeshini?
 
Kwenda kama mujibu wa sheria asipoenda sasa hataweza tena,
mara nyingine ataenda kwa njia ya kujitolea sio tena mujibu.
 
Kwenda kama mujibu wa sheria asipoenda sasa hataweza tena,
mara nyingine ataenda kwa njia ya kujitolea sio tena mujibu.
Kwa hiyo Kuna kwenda kwa hiari siyo?
Utaratibu unakuwaje?
 
Kwa hiyo Kuna kwenda kwa hiari siyo?
Utaratibu unakuwaje?
Uwa wanatangaza nafasi za kujitolea JKT baadhi ya miaka, unapitia mchujo kuanzia wilayan,mkoani then unapangiwa kambi utakayoenda, sema kujitolea mara nyingi ni miaka miwili.
Ukiwa na mtu mzito wa kukupeleka autaangaika na michujo utaripoti kambini moja kwa moja.
Sema siku hizi kujitolea hakuna faida waweza poteza muda bure na usipate ajira yoyote nzuri.
Kama amechaguliwa na angeweza ni heri aende tu hii mujibu ya miezi mitatu.
 
Uwa wanatangaza nafasi za kujitolea jkt baadhi ya miaka, unapitia mchujo kuanzia wilayan,mkoani then unapangiwa kambi utakayoenda, sema kujitolea mara nyingi ni miaka miwili.
Ukiwa na mtu mzito wa kukupeleka autaangaika na michujo utaripoti kambini moja kwa moja.
Sema siku hizi kujitolea hakuna faida waweza poteza muda bure na usipate ajira yoyote nzuri.
Kama amechaguliwa na angeweza ni her aende tu hii mujib ya miez mitatu
Asante kwa ufafanuzi boss
 
Kijana asome, hilo ndilo la muhimu kwa sasa.

Nafasi za kujitolea zikitoka ataomba kupitia ofisi ya Mkuu wa wilaya huko ulipo.

Akikosa, mwakani majina ya Form Six yakitoka naye aende Makao Makuu ya JKT, Dodoma.

Wale wanavyopenda nguvu kazi, watamtupa kwenye kambi za kilimo. Akahenyeke huko.
 
Shukrani boss
 
Hivi ili mtu awe mwanajeshi anatakiwa kusomea fani gani?(Mimi sii mjuzi wa haya Mambo)
Vyuo viko wapi?
 
Back
Top Bottom