Mafunzo ya kilimo cha kisasa cha greenhouse

Mafunzo ya kilimo cha kisasa cha greenhouse

greenhouse mara nyingi wanapandaga mazao ya muda mfupi kama nynya hoho n lkely nakushauri mtafute biashara2000 humu atakuelekeza vizuri au soma post za humu na za kwene biashara utaona post zake na namba zake
 
greenhouse mara nyingi wanapandaga mazao ya muda mfupi kama nynya hoho n lkely nakushauri mtafute biashara2000 humu atakuelekeza vizuri au soma post za humu na za kwene biashara utaona post zake na namba zake
Asante Sana,nimeshamtafuta.
 
Panda nyanya, hoho,tango au biringanya ama ngogwe. Pia greenhouse inategemea sana na mazingira uliyopo kama ni sehemu ya joto ina standard zake ili kuruhusu air exchange na kama ni sehemu za baridi pia ina standard zake ili kukeep internal heat.
Greenhouse inayofaa kwa maeneo ya joto inatakiwa iwe na kimo/gutter height atleast 2.5-3M na Urefu wa kati kutoka chini 5M. Side walls inatakiwa iwe netted. Mfano wa greenhouse ya ukubwa 8×15M inaweza kukupa mavuno ya nyanya hadi tani 15 -20 kwa mwaka. Pilipili hoho nyekundu na njano grow better in ghouse than in open field
Niko Mwanza hali ya hewa naona ni yakawaida sio joto sana sio baridi,kuhusu ukubwa na vipimo vya hizi green house sijui kwa kweli labda niende na mtaalam anidadavulie zilivyo na size zake.
 
kama hujawai kuingia kwenye kilimo nipm namba yako tuchat whatsapp nikusaidie hatua kwa hatua otherwise wanaofunga grewnhouse wengi ni matapeli watakufungia below standard. au kama unaweza njoo wizara ya kilimo dsm
Nimewahi kulima ila open field,hizo green house zishafungwa , zilifungwa na kampuni kutoka Kenya 2 years ago ni za kutumia tu sio kuanza kufunga tena.
 
Bado najifunza Kilimo,ninazo green house kubwa 7 ambazo nimepewa niinvest baada ya kuonyesha interest kwenye Kilimo.Zote zina system ya drip irrigation, Maji ya kutosha na full equiped.Zipo Mwanza.

Je nilime nini, na Kama mwanafunzi na mgeni katika mambo ya kilimo hakitanigharimu Sana.Na nitapata soko kiurahisi,nataka nianze next month.

Ntashukuru kwa mawazo.
Upo Mwanza sehemu gani mkuu tuonane? Nmekuja kikazi kidogo huku
 
Nakushuri upande nyanya na hoho
Ungekuwa arusha moshi ningekutembelea
 
Dogo kama umepewa iyo kitu mm bnafs nakutaman vbaya.. huo ni bonge wa utajiri kjana panda mboga mboga ata nyanya za mavuno marefu utatajirika adi uzikatae nyanya..
 
greenhouse huwa zinakuwa na ukubwa flani? zenyewe zina ukubwa gani? (in metres).na ni za miti(milunda) au chuma?
greenhouse ,kutegemea na ukubwa wake zinaweza kukusogeza mbali sana kimaisha ukizingatia taratibu za kuzitumia, huo ni utajiri tayari.
 
Habari wana Jamvi.
Natumai mu wazima wa afya, lakini chukua dakika chache katika ule mda wako wa mapumziko iwe mchana kazini au jioni nyumbani upitie japo ni kwa kifupi Technology hii ya kilimo cha kisasa cha GreenHouse.

Najua wengi tunajua kilimo hichi ila tukumbushane tuongeze japo maarifa kidogo.
Green house au Banda kitalu ni Tech ambayo huipatia mimea mazingira mazuri ambayo yanasaidia mimea kuwa na mazao mengi kwa gharama ndogo baada ya kuifunga na kuyakinga yasidhurike na mvua kubwa,joto kali, wadudu na magonjwa.

Aina za Greenhouse.
1. Ufunikaji,
-greenhouse zinazotumia mifuko ya plastic 100% ila yana njia ndogo kwa juu inayoruhusu hewa kuingia na hii ni kwenye maeneo ya baridi na mazao yanahitaji joto
- Pia kuna yanayotumia Plastic 80% na plastic net 20% kwa maeneo ya joto.

2. Utengenezaji wa frame.
-Hapo wako wanaotumia miti
-Greenhouse za mabomba ya chuma
-Greenhouse za mabomba ya plastic

3. Matumizi.
-Greenhouse zinazoongeza joto
-Greenhouse zinazopunguza joto

4. Gharama za uwekezaji.
-Greenhouse za gharama kubwa->50mil
-Greenhouse za gharama za kati 20-50mil
-Greenhouse za gharama ndogo chini ya 20mil

5. Umbile/Shape.
-umbile la nusu duara.
-umbile la nusu duara na mstatili kwa chini.
-Pembe tatu
Na mengine mengi.

Labda tumalizie na faida kwa kifupi sana
1. Mavuno ni mara 10 zaidi
2. Uzalishaji ni kipindi chote cha mwaka
3. Uhakika wa mafuno
4. Dawa inafanya kazi kwa asilimia kubwa
5. Matumizi madogo ya maji hapa utatumia Drip Irrigation System.

Yako matumizi mengi pamoja na yale ya tissue culture na soilless culture.
 
"Soilless culture" unamaanisha "hydroponics"
 
Naona kama uwekezaji wake ni ghali lakini naona kwa hali ya sasa huwezi ukapata faida.
 
Umelima nini au bado ujapata ushauri ulime kitu gani??
 
Panda nyanya kaka au vitunguu, daah mm mkulima nipo moro naona unautajiri huo mkuu utumie vizuri
 
Back
Top Bottom