Mafunzo ya kilimo cha kisasa cha greenhouse

Mafunzo ya kilimo cha kisasa cha greenhouse

Habari zenu.

Jamani kama kuna mkulima wa nyanya za green house au kuna anayejua mkulima wa nyanya izo naomba tuwasiliane kwa PM.
Nipo Dsm.

Asanteni
 
KWA NINI UWE MASKINI?

JE, UNGEPENDA KUVUNA NYANYA NYINGI KILA WIKI NA KUJIPATA KIPATO KIKUBWA KUPITIA KILIMO CHA GREEN HOUSE?

View attachment 165705


Team ya "AMKA NA BADILIKA" ya CONSNET GROUP ikishirikiana na wataalamu wa GREEN HOUSE katika maeneo ya joto AFFORDABLE GREENHOUSE kutoka Kenya wanapenda kukujulisha kuwa unaweza kujengewa GREEN HOUSE ya ukubwa wa Mita 8 kwa Mita 15 na kupanda mazao upendayo ya bustani kama Nyanya; Pilipili Hoho; Vitunguu; Bilinganya; Vitunguu; Matango nk ambayo yanaweza kukupatia zaidi ya tani zaidi ya 20 kwa Mwaka na kukuingizia kipato kikubwa.

Kujengewa GREEN HOUSE moja ya 8M X 15 M (Kutumia mirunda na mbao za dawa) ni TZS 5.0 Millions Tu na unajengewa katika kipindi cha wiki 2 pamoja na kupandiwa mazao. Pesa hiyo inahusisha mbegu za kisasa, mbolea, madawa, kupima udongo na maji maabara, tank la lita 1000, drip irrigation system, na mafunzo na kujengewa.

Kwa sasa zipo "KITS" za kutosha za Green House. Kama utapenda kujengewa Green House na bajeti iko tayari, tafadhali wasiliana nasi kupitia namba: +255 755 285 023.
Mkuu kama naitaji green house peke yake inakuaje
Mkuu, Hakuna Gh yenye udogo zaidi ya hiyo, au ukiweka ndogo ya hapo faida aitakuwa kubwa...
 
Kwanini wataalam wengi wa green house vipimo vyao vya eneo ni hivyo hivyo? 15x8?
 
Mkuu kabla ya ujenzi inafanyika soil analysis na water analysis kupitia maabara ili kujua virutubisho vilivyopo na kama kuna infection yoyote.

Unaweza kufanya Green House Kiluvya. karibu sana.
Je. Joto la dar es salaam alitoathiri mazao?
 
Greenhouse kwenye joto kama rufiji itakuwa poa?
 
Hii kilimo cha nyanya inalipa sana asikwambie mtu. Nilianza kulima mwaka Jana ingawa inahitaji mtaji lakini ni kilimo nzuri sana. Usianze kulima nyanya km huna elimu nayo itakuaibisha pia pale unapokurupukia kulima kwa vile umeona jirani yako analima.
 
Green hse ni wewe mwenyewe!! kama una mbolea ya samadi, maji na madawa ya kuulia wadudu why not make your own green hse?
 
Hivi na hili joto la pwani, inakuwa vp mle ndani!?? Au kunawekwa feni
 
Yaani nikishaona mtu katika biashara zetu za kawaida anaingiza mawazo ya kina Adam Smith, Mara sijui return of investment, accounting rate of return na mengine kama hayo, huyo hata umpe 1,000,000,000 afanye biashara kesho yake tu anafilisika. Na kawaida watu hao wengi unawakuta ana MBA au amesomea "masomo ya biashara", anadhani biashara ni vitabu, kibongobongo wanaotoboa katika biashara hata Adam Smith hamjui wala Hana mpango wa kumjua milele! Muuzlie S.H. Amon kama anamjua Adam Smith!
umeongea point mkuu
 
Wakuu nahitaji msaada wenu.

Nahitaji kulima nyanya katika banda kitalu, kampuni gani inayotengeneza mabanda yenye ubora, na wanaotoa ushauri jinsi ya kuhudumia hilo shamba?

Mwenye kujua anijuze tafadhali.
 
wakuu naitaji msaada wenu naitaji kulima nyanya katka banda kitalu kampuni gani inayotengeneza mabanda yenye ubora, na wanaotoa ushauri jinsi ya kuhudumia hilo shamba. mwenye kujua anijuze tafadhali
Fika wizara ya kilimo temeke watakupa ushauri mzuri sana
 
Back
Top Bottom