Maridadi kabisa. And thats my point.
Tumekuwa taifa la walalamishi, ujanja ujanja, mkato mkato....wizi pety pety.....yaani hatujitambui..kuanzia kwa viongozi mpaka kwetu wananchi. Lakini kikubwa zaidi..ni kipi kifanyike kuaddress hili tatizo? Mi naamini lazima tuanze kwa kubadilika kifikra. Angalia hata humu JF..kuna watu wakisikia unacomment against their belief in CCM or Chadema or whetevver party..unaonekana msaliti..huna shukrani kwa serikali sikivu! Jana nilibahatika kuangalia bunge na michango ya wabunge! Specifically nilimwangalia msomi Omar Nundu (I didnt know the dude had been a minister)..Yaani I felt very sorry for myself and my country. Yaani jamaa anaongea pumba ni hakuna mfano! Yaani nilikubali ule msome kwamba..some people appear smart until you hear them speak.
I mean wengi wetu tumeshajikatia tamaa kabisa....Lakini is it true kwamba hatuwezi kubadilika? tujadili hili.
Tujue kabisa kwa kila maamuzi tuyafanyayo...lazima kuna consequences. The only way the poor can engage in deliberative dialogue in society such as ours..is to be responsble kwenye maamuzi muhimu kama ya kuchagua viongozi na kuwawajibisha. These viongozi are damn tired na wameshiba mpaka wamejisahau. Unajua wenzetu wanasema stupidity..is doing something over and over again..expecting different results. TuNAFANYA UJINGA ULE ULE tukitegemea mambo yatabadilika.
Naamini ni muhimu hata mitaala yetu ya kishule tuibadilishe kwa namna fulani kuendana na hali halisi. Imagine mtu ana div. four ndo anachaguliwa ualimu. Juzi jamaa ananiambia..bro..nimefeli form four hebu nifanyie mpango wa upolisi au Jeshi!!! Means hizo fani ni za failures! Mkuu kama tumefikia huko na bado hatulioni huoni hatari?
Ndo maana mkuu..leo ukiendesha gari zuri au ukajenga nyumba nzuri..watu wanajua umeiba.....maana hata viongozi wetu..wametuonyesha kwamba kufanikiwa lazima uibe kodi za raia. Sad indeed.
Lakini ideas kama hizi za akina Msimbe..can change one's life positively kabisa..sema wengi wetu tumekata tamaa na I really hope tutabadilika.
Masanja
Some thing is wrong.
Laiti kama tungekutana watu 28 wenye malengo yanayoshabihiana ya kukataa umasikini na kuamua mawazo ya kinyonge na uoga kwamba hatuwezi kisha tukasimama kwenye jambo moja ambalo tutaona linafaa na kisha tusiwe wachoyo...tuwe transparent kwa wenzetu wasioamini hadi waone! Nina hakika kila mmoja kwenye hao 28 angeweza kuinspire watu sita hadi nane kutoka kitongoji chake na katika hao nao wangehamasika na kuhamasisha watu wawili watatu kwenye mitaa yao na finaly kaya zote zingekuwa na mwamko wa aina moja, na tumaini jipya na moto ingekuwa...alaaah kumbe tunaweza!
Baada ya hilo tungeyatazama maisha katika angle tofauti,mind zetu zisingekuwa iddle tena kufikia kiwango cha kuanza kulaumu circumstances!
Jana nilisoma chapisho moja la kijana ninayeheshimu sana uwezo wake wa kuchanganua mambo na namna anavyowaza na kujenga hoja fikirishi Malisa Godlisten ...
Alitoa mfano wa namna wenzetu wanavyotumia advantage ya kutojitambua kwetu kwa kunufaika na ujinga wetu...alimzungumzia bwana mmoja aliyetoka kwao ughaibuni kwa mtaji mdogo wa Mil. Moja kuja kwetu kuwekeza kwenye biashara ya kununua ngegere kwa kiwango cha sh. 10,000 kwa kila ngedere of whom aliwapata ngedere 50 kwa kiwango cha sh. 500,000.
Baada ya kuadimika akaamua kupandisha dau hadi sh. 20 na kufanikiwa kupata wengine ishirini kwa jumla ya sh 400,000..na baada ya kuona scarcity imeongezeka akiwa amebakiwa na 100,000 akapandisha tena dau hadi sh. 50,000 kwa ngedere na kupata wawili tu....
Kwa kutambua kuwa ngedere wamemalizika kwenye kijiji alichowekeza akapandisha dau hadi laki tatu kwa ngedere mmoja, kwa tamaa ya fedha wanakijiji wakaamua kusaka ngedere kila kona na muda haukupita wakapata habari ya uwepo wa mzee mmoja kwenye kijiji cha jirani aliyekuwa anauza ngedere mmoja kwa bei ya sh. 200,000. Wakafanya kila waliloweza kwa kukopa na kupita hapa na pale wakawanunu ngedere wote of which walikuwa 72 kwa bei ya laki mbili mbili ili wakauze kwa bei ya laki tatu...
Fadhaa ikawapata baada ya kurudi kwao na kumkosa mnunuzi aliyewaahidi 300,000... Wakasubiri siku ya kwanza hawakumuona, siku ya pili, ya 3, mara wiki, mara mwezi, mara mwaka....
Behind the scene...
Wale ngedere waliokuwa kijiji cha pili ni wa yule mzungu. Alikua anawanunua kwa wale wanakiiji anakwenda kuwahifadhi kijiji cha jirani kw yule mzee.
Kichwani alijua kbs ipo siku ngedere wataisha na ataanza kuwauzia walewale wanakijiji bila wao kujua, tena atauza kwa bei kubwa.
Yeye alitumia milioni moja kununua ndedere 72.... sasa amekuja kuwauzia wanakijiji walewale kwa laki 2 kwa kila ngedere. Hivyo akapata jumla ya sh.milioni 14.4, Kisha akaondoka na hela zake, akawaachia wanakijiji ngedere wao plus madeni na umasikini wa kutupa...
Angalizo tunalopata hapa ni kwamba mitaji mikubwa tunayopaswa kuwa nayo ni akili zetu na si kiasi kikubwa cha fedha na kuwa makini na maamuzi tunayofanya leo ili yasitugharimu kesho....Kwa maana nyingine, ni kwamba umasikini na utajiri wetu uu proportional na uwezo wa akili zetu!
Wasalaaam!