Mtu Poa 2013
Senior Member
- Mar 26, 2013
- 105
- 65
Hii picha si ya shamba lako, mbona huko chini kuna maneno ya kiarabu?mtu poa 2013, mtoa mada, smart 2013, consolata2000, 3500 nadhani ni mtoa mada na ID zake tofauti
Hapana dada, hiyo nadhani ni kamera yenyewe maana imenunuliwa kutka doha. Mimi sio bwana biashara 2000
Hii picha si ya shamba lako, mbona huko chini kuna maneno ya kiarabu?mtu poa 2013, mtoa mada, smart 2013, consolata2000, 3500 nadhani ni mtoa mada na ID zake tofauti
Hii picha si ya shamba lako, mbona huko chini kuna maneno ya kiarabu?mtu poa 2013, mtoa mada, smart 2013, consolata2000, 3500 nadhani ni mtoa mada na ID zake tofauti
Hata lotti masai, mwana ally, ladyfurahia, thegreat genius, mimi.mimi, husninyo, dolevaby, africando na yeyote yule katika hii thread ni biashara2000! This guy has a lot of time in his hands.
Mi nadhani cha muhimu hapa ni kuendeleza kile ambacho baadhi ya members waliochangia katika thread hii walioamua kujiunga pamoja na ku share uzoefu wao na kuamua kukutana na kuanzisha mashirikiano, watu wa dar na arusha nadhani. Hii ndio inayotakiwa ifanyike. Watu wameamua kuondokana na umaskini. Kila mtu amechoka kuishi maisha ya kutokujua kesho atapata wapi chakula, mavazi na nyumba. Conspiracy theories kama unazipenda kuna section ya intelligence ningeomba uwe una spend muda wako huko. Humu watu waachwe wajifunze na kuanzisha miradi yao ya kujiingizia kipato.
Kuhusu ku share uzoefu, biashara2000 naona ana hamasisha watu kushirikiana na kushare information. Katika vitu ambavyo unachanganya ili kuongeza ubora wa mkaa wakati wa kuutengeneza kama ambavyo biashara2000 anavyoshauri, juzi nilimpigia simu akasema pia unaweza changanya kiasi kidogo cha sodium nitrate au chemicals nyingine ambazo yeye aliniambia kuwa weekend iliyoisha alikuwa anafanyia majaribio. Nimeona ni share info hii kwa kuwa leo ndio nimechanganya chemical hii na baada ya mkaa kukauka ntaangalia kama kuna tofauti.
Wangu bado sijauchanganya na kitu chochote kipya naona uko vizuri tu. Ila kwa kuwa haiumizi kujaribu vitu vipya, ntajaribu ujanja huo mpya. Hiyo chemical inasaidia nini hasa?
ni kweli kabisa hata mm na myamba mbepo juzi tulikua tunajadiiana kuhusu hizo chemicals cz tulipitia writtings mbalimbali tukakuta hivo vitu na wataalam wanasema kuna ya.kuongeza uwezo wa mkaa kuwaka kwa ukali,nyingne mkaa kuwaka muda mrefu hadi white chalk unatumija na wanasema una positive impact.
mm leo nitest sample yangu nyingne ambayo ni sample ya tatu baada ya ushauru wa bw 2000 na wadau wengne mtu poa na wengne na naona kuna dalili za kuwepo positive impact ksho kuanzia asubuhi ntautumia niendelee kuucheki
Yani mimi nishautengeneza na kuupikia several times..sijaweza bado kuwapa watu wengine wautest lakini uko poa.sana tatizo.kidogo ni kuwa majivu ni mengi na ukisha waka hautakiwi uguse guse jiko maana unavunjika. Vizuri uuongezee hapohapo. Nilimpigia Biashara2000 akanambia nikipata mashine kubwa kidogo nibadili ratio.. Sasa hivi niko na 5 kwa 10..NAJUA NTAFIKA TUU
Yani mimi nishautengeneza na kuupikia several times..sijaweza bado kuwapa watu wengine wautest lakini uko poa.sana tatizo.kidogo ni kuwa majivu ni mengi na ukisha waka hautakiwi uguse guse jiko maana unavunjika. Vizuri uuongezee hapohapo. Nilimpigia Biashara2000 akanambia nikipata mashine kubwa kidogo nibadili ratio.. Sasa hivi niko na 5 kwa 10..NAJUA NTAFIKA TUU
Halafu kama mkaa wako unapikia vizuri tu usisubiri kitu. We anza kuuza ilimradi tu uwauzie watu kwa bei nzuri wakati huo ukiendelea kushughulikia tatizo la majivu liishe. Hakuna kitu perfect duniani, hiyo isiwe sababu ya wewe kukufanya usubiri kupata maendeleo
Kuna kipindi nilikuwa Nairobi katika shughuli zangu za kutafuta maisha nikakuta katika maduka mengi wanauza huu mkaa wa kisasa ukiwa umepakiwa kisasa kabisa jambo ambalo lilinihamasisha sana. Nikaona hata mimi naweza fanya hivyo ingawa kwa sasa bado sijaanza kupaki kitaalamu. Ila nimeona ni idea nzuri kwa sisi watz nasi kuamua kufanya vitu kisasa zaidi kama wakenya. Kuna kampuni moja ya keny ainaitwa chardust Ltd ndo hao wanaotengeneza mkaa na kuupaki katika pakti ndogo ndogo za kilo 4 na kuuza kwa sh 200 ya kenya ambayo ni kama sh 3500 ya bongo. Cheki picha ya mkaa huo hapo
View attachment 183910
Hii ni changamoto ambayo inabidi tuweke mawazo yetu huko ili nasi tufanye mambo ya kisasa. Ila nimeona kampuni moja ya tz nao wameanza kupaki namna hii wanauuza mkaa wao pale shoprite mlimani city. Wamejitahidi. Na nikachunguza packaging yao nikagundua kuwa wanatumia mifuko flani hivi ya kaki inauzwa kwenye ma supermarket kwa ajili ya kubebea vitu na kuweka mkaa huko na kuweka nembo. Wanawekea nembo zao pale manzese darajani kuna jamaa wanachapisha nembo kwa bei nzuri. Nimeamua ku share info hii kama mchango wangu ktk jamii ya JF
aisee nahisi cjui ndo nature ya huu mkaa ukishawaka hautakiwikuguswa unamomonyoka..ila nadhani matumizi ya maji yapo tu kwenye hatua ya kupika uji mimi sieki maji baada ya hiyo hatua ya kupika uji lain stil ina hiyo tatzo la kummomomyoka ikiguswq wakati limeshika moto.ila maji nayotumia kwenye lupioa uji niya chumvi,ila pia bado naendeleq kufanya testing kwq mkono.pia wazo la kuuza mkaa ukiwa bado una kasoro na mm naona itakua c wazo zuri..unaua soko kwqn uliemuuzia kuja kumcomvice kua saivi ni mzuri itakua shughuli pevuchangamoto kama hilo nilikuwa nalo ila nilitatua kwa kuacha kabisa kuweka maji katika hatua za utengenezaji wa mkaa kwa maelezo ya biashara2000. Alisema maji yanaua nguvu ya mkaa na kuufanya uwe na majivu mengi. Usiweke maji kabisa katika mkaa wako
sawq mkuu ntatest then ntakupa feedbak badaeIjaribu hiyo kesho kama bado utakuwa unakutatiza nipigie tuendelee kushauriana na kurekebisha mambo mpaka utokee vizuri maana watu wengine wametoa vizuri tu
Mkuu tusonge mbele daima. Alhamisi ilopita mkuu Lotti Mmasai likuja kunitembelea. Tumepanga pia kutembelea na wadau engine ili kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika kuboresha izalishaji. Mimi kwa sasa nimetengeneza oven kubwa ya kukaushia mkaa maana hali ya hewa siku hizi si rafiki saana. Karibu Dar nasi pia tutakuja Moro mkuu. Ujapo ni pm kwanza nasi tutaku pm kabla ya kuja huko