Mimi nakumbuka wakati nikihangaika katika kupata kipato cha kuniwezesha kujikimu kwa siku. Nilikuwa napata shida ya kupata hela ya kula, malazi yaani kodi na mavazi. Yaani ilikuwa shida sana. Hali ngumu kimaisha na kikipato. Nilikuwa naingia internet cafe kama njia ya kujaribu kuondoa mawazo. Bahati nzuri nilikutana na hii posti ambapo ilinihamasisha kuamua kuachana na shida na umaskini. Kwa kuwa jamaa alisema naweza kuanza hata nikiwa na mtaji wa sh 5,000, mimi nilianza na sh. 3200 nakumbuka kabisa. Nikaendelea hivyo hivyo hadi sasa ni miezi 4 sasa imeshapita tokea nianzishe biashara yangu. Ni ya wastani na inaniwezesha kujikimu kimaisha na siishi kwa hofu na kubangaiza tena kama zamani. Mi nakushukuru bw 2000.