TANGAZO: Tokea nilipoanzisha hii thread kuhusu jinsi ya kutengeneza mkaa na jinsi mimi ninavyoendesha biashara hii ya mkaa, watu wengi ambao hawako interested au ambao hawana mpango wa kuanzisha biashara ya mkaa ila ni wajasiriamali, wameniomba niwape uzoefu wangu katika kuanzisha na kukuza biashara yenye mafanikio. Na hii inatokana na ukweli kwamba ukiacha kuwa mimi natengeneza mkaa ila zidi hii ni biashara kama biashara nyingine inayoongozwa kwa mfumo wa kibiashara.
Kutokana na nchi hii na duniani kwa ujumla elimu ya biashara imekuwa ikitolewa kwa mfumo wa theory tu kwa maana kuwa elimu inatolewa na watu ambao sio wao wenyewe wafanyabiashara, imefanya watu wengi wanaomaliza vyuo waliosomea biashara au watu waliojifunza biashara kupitia mtandaoni, wanaingia mtaani kuendesha biashara na kukumbana na challenges zinazowafanya wafunge biashara na kugeukia kuajiriwa ili angalau wawe na uhakika wa kupata hela ya kula. Nadhani mnafahamiana na mifano hii huko mitaani.
Kwahiyo wajasiriamali wengi wameniomba niwape elimu kutokana na uzoefu wa ufanyaji biashara ambao nimeupata kwa kufanya biashara katika mazingira ya nchini kama vile jinsi nilivyohangaika kupata vibali mbalimbali vya biashara, jinsi nilivyopata mitaji, jinsi ya kuuza bidhaa katika soko gumu la bongo, jinsi ya ku deal na wafanyakazi, jinsi ya kufikia malengo yako, kuondoa uoga ulionao kwa njia rahisi bila kutumia njia zisizofanya kazi zinazoandikwa kila mahali kwenye internet, na kadhalika wa kadhalika.
Unapoamua kujifunza kupitia mtandao unakuwa unapotea kwa kuwa 1. anayekupa hiyo elimu ni mwandishi tu wa blog ambaye si mfanyabiashara, so ni theory tu, 2. unajifunza biashara katika mazingira ya ulaya na marekani ambapo mazingira yake ni tofauti na bongo. So naandaa kitabu hiki kwa ajili ya uzoefu wangu wa kufanya biashara hapa bongo na challenges zake na solution zake. Sisemi mimi ni bingwa wa biasha ila nachofanya ni kukueleza niliyojifunza kwa kufanya biashara ninayofanya.
Kitabu nimekuwa nikikiandaa tokea nilipoanza kupigiwa simu za maombi. Kitakuwa tayari kesho ijumaa tarehe 1 mwezi wa 2. Kinapatikana kwa sh. 10,000 tu na utajifunza mambo mengi sana yakiwemo hayo niliyoyasema hapo juu. Kwa sasa kitakuwa kinapatikana katika soft copy.
Asanteni sana.