Mafuriko Dar es Salaam: liko wapi ziwa Mwananyamala, Ziwa Tandale na ziwa Magomeni?

Wakati tunajadili mafuriko, pia tujipe tafakari ya Dar es salaam ilivyopaswa kuwa na sisi tumeenda kinyume na hali ya mazingira kwa kiasi gani.

Ninaamini mito inayotoka maeneo mbalimbali ukanda wa pwani inaamini bado haya maeneo ya maziwa yapo, hivyo mito hiyo inaleta maji ziwani.

Tunashangaa mafuriko, kumbe hayo maeneo ni sehemu Mungu aliitenga kwa ajili ya maji.

Hakuna namna ya kuiponya Dsm dhidi ya mafuriko. Sinza, Tandale, Mwananyamala ni eneo oevu (ihefu ya jiji)

Wilaya pekee isiyo na mafuriko ni Kigamboni.
View attachment 2878546
Nasikia hii ni ramani ya mwaka 1957 😃😃 sasa wachaa waendelee kuogelea.
 
Kuna jamaa nikimtembeleaga pande hizo
Tukiwa tunatoka nje kutembea tembea najishangaa mbona kila muda mimi ni kuruka ruka tu na kupiga misamba 😄
😂😂😂😂😂 kwamba ardhi yao hainyonyi maji? Au ni mama ntilie wanachangia kuyamwaga mwaga?

Kuna Tabata shule, niliendaga mara1, napo sikuuelewa ule mtaa kabisa.
 
Mafuriko ya Jangwani yamesababishwa na washenzi waliojenga mahekalu pale mikokoni, karibu na daraja la slender
 
😂😂😂😂😂 kwamba ardhi yao hainyonyi maji? Au ni mama ntilie wanachangia kuyamwaga mwaga?

Kuna Tabata shule, niliendaga mara1, napo sikuuelewa ule mtaa kabisa.
Ni mwendo wa kuruka ruka tuu au kuzunguka maduara ya maji 😄
 
Wakati nikakua tukiishi mikocheni tangu 1979 , maeneo ya msasani , mbezi beach , mikocheni kulikuwa na mikondo ya bahari , bahari ikijaa inamwaga maji Kwenye mikondo maisha yanaendelea .
Kulikuwa na uwiano mzuri kati ya nguvu za asili na maisha ya kila siku .
Na maji yakitoka huko bara yanaelekea Kwenye Hiyo mikondo Mpaka baharini .
kulikuwa na maeneo ya kuvuna chumvi Kama pale bahari beach na ndege wa yanga yange ilikuwa sehemu Yao ya malisho na kupumzikia kabla ya kuanza safari ndefu ..
Kuanzia Miaka ya 1995 na kuendelea watu wakaanza kujenga kuvuruga ili asili yake .
Asili huwa haisahau ilipotoka , Leo ndiyo imekumbuka kwa kurudi kwa Kishindo.
 
Wakati tunajadili mafuriko, pia tujipe tafakari ya Dar es salaam ilivyopaswa kuwa na sisi tumeenda kinyume na hali ya mazingira kwa kiasi gani.

Ninaamini mito inayotoka maeneo mbalimbali ukanda wa pwani inaamini bado haya maeneo ya maziwa yapo, hivyo mito hiyo inaleta maji ziwani.

Tunashangaa mafuriko, kumbe hayo maeneo ni sehemu Mungu aliitenga kwa ajili ya maji.

Hakuna namna ya kuiponya Dsm dhidi ya mafuriko. Sinza, Tandale, Mwananyamala ni eneo oevu (ihefu ya jiji)

Wilaya pekee isiyo na mafuriko ni Kigamboni.
View attachment 2878546
Nadhani Ziwa magomeni limebaki tope zito tu
 
Kuna jamaa nikimtembeleaga pande hizo
Tukiwa tunatoka nje kutembea tembea najishangaa mbona kila muda mimi ni kuruka ruka tu na kupiga misamba 😄
Nakumbuka zamani miaka ya 92-94 pale mikocheni A kuanzia shoppers Hadi chama kulikuwa na mashamba ya mpunga na matete..
Eneo lote la msasani uwanja wa magunia ni bonde la mpunga zamani
 
Duh!
Kuna historia ya kuwa maeneo mengi dar yalikuwa maziwa, mabonde, mito, delta,mikondo ya bahari, mabonde ya mpunga, mabonde ya misitu ya mikoko, mabonde ya kuvuna chumvi, mabonde makubwa ya maji mpaka viboko wakubwa san walikuwa wanakaa maarufu kama Boko. Ndio maana Boko panaitwa Boko kwa kuwa kulikuwa na viboko wengi mno. Hiyo historia ipo toka enzi za Machifu, Masultani, Mjerumani, Muingereza, Baada ya uhuru, baada ya miaka ya 90 kuelekea 2000 ndio watu wakaanza kuelekea huko. Kwa hiyo inawezekana maji yanarudi kwenye njia zake za asili toka dunia kuumbwa.

Ndio maana kihistoria miaka ya 1885 na kuendelea,Mjerumani hakukaaga Dar wala kuweka makao yake Dar, bali aliweka makao makuu yake Bagamoyo mkoa wa Pwani na Tanga, kutokana na Dar kujaa maji mno Mara kwa Mara.

Kitaalam Dar ni mji wa "Seasonal Swamps"
 
]
Kuna jamaa nikimtembeleaga pande hizo
Tukiwa tunatoka nje kutembea tembea najishangaa mbona kila muda mimi ni kuruka ruka tu na kupiga misamba 😄
Hii mada leo Ina comedian wengi, anyway wabongo wanadai wakijenga njia ya maji, maji yanawakimbia, sasa maji ya Siku hizi viburi yanawakimbilia, ndio yanaitwa mafuriko
 
Wakati tunajadili mafuriko, pia tujipe tafakari ya Dar es salaam ilivyopaswa kuwa na sisi tumeenda kinyume na hali ya mazingira kwa kiasi gani.

Ninaamini mito inayotoka maeneo mbalimbali ukanda wa pwani inaamini bado haya maeneo ya maziwa yapo, hivyo mito hiyo inaleta maji ziwani.

Tunashangaa mafuriko, kumbe hayo maeneo ni sehemu Mungu aliitenga kwa ajili ya maji.

Hakuna namna ya kuiponya Dsm dhidi ya mafuriko. Sinza, Tandale, Mwananyamala ni eneo oevu (ihefu ya jiji)

Wilaya pekee isiyo na mafuriko ni Kigamboni.
View attachment 2878546
Nadhani hii ni Ramani ya Ujerumani.

Kitu ambacho hatuna Tanzania ni kupanga maisha yetu kwa miaka 50 ijayo.

Baada ya Dar es salaam kuwa mji mkubwa watu wakawa wanauziwa viwanja kila sehemu bila kujali Geographical survey matokeo yake watu wakajazana Maeneo yenye Swamps kama Magomeni, nina hukakika miaka ya 1600 haya maeneo yalikuwa ni seasonal swamps na hayajawahi kubadilika,

Tulivopata uhuru hatukuendeleza haya maeneo kwa ajili ya kuwa makazi, matokeo yake ni mafuriko kila sehemu, miji mingi ya Ulaya ilijengwa miaka kuanzia 1000 wakajenga kingo za mito na mito iko hadi leo weather inapungua au haipungui
 
Wakati nikakua tukiishi mikocheni tangu 1979 , maeneo ya msasani , mbezi beach , mikocheni kulikuwa na mikondo ya bahari , bahari ikijaa inamwaga maji Kwenye mikondo maisha yanaendelea .
Kulikuwa na uwiano mzuri kati ya nguvu za asili na maisha ya kila siku .
Na maji yakitoka huko bara yanaelekea Kwenye Hiyo mikondo Mpaka baharini .
kulikuwa na maeneo ya kuvuna chumvi Kama pale bahari beach na ndege wa yanga yange ilikuwa sehemu Yao ya malisho na kupumzikia kabla ya kuanza safari ndefu ..
Kuanzia Miaka ya 1995 na kuendelea watu wakaanza kujenga kuvuruga ili asili yake .
Asili huwa haisahau ilipotoka , Leo ndiyo imekumbuka kwa kurudi kwa Kishindo.
Usiwe na shaka, Nature itashinda kama hutaki kuishi nayo sawa, hii mikondo ya maji itakuja kurudi tu kawa hawatairudisha na kujenga mifereji mikubwa
 
Back
Top Bottom