Foffana
JF-Expert Member
- Oct 29, 2022
- 861
- 1,547
Habari za jioni wakuu straight to the point
Niwape ushauri vijana wenzangu ambao tumepanga huku mabondeni na ambao wanatarajia kupanga kuwa wasijaribu hiko kitu
Mafuriko yanarudisha sana nyuma hasa kwa vijana ambao tunahustle ili tuweze kutoboa
Leo asubuhi nilitoka kidogo ghetto kuna mishe nilikuwa naifuatilia sehemu mida ya saa 10 napigiwa simu kuwa maji yamejaa vibaya mtoni nikajitahidi kuwahi chap nikakuta ndo yanagonga mlangoni kufungua mlango sekunde kadhaa tu maji tayari magotini, nikafanikiwa kuliwahi godoro, nguo na vitu kadhaa ila feni,subwoofer,kifridge vyombo vidogo vidogo na kisofa vyote chali
Aisee vijana wenzangu hata kama kodi ni ndogo huku mabondeni na kulingana na kipato chetu inatulazimu kuishi huku.....tuikatae hii hali mafuriko yanarudisha sana nyuma
Wasalaaam