Wakazi wa dar Wana roho ya chuma, Kuna njia nilikua napita kipindi nipo chuo, msimu wa mvua kuna wakazi wa nyumba flani muda wote utakuta wanachota maji na ndoo ndogo kuyatupia barabarani, kiufupi nyumba ilikua inaingiza maji si mchezo
Baada ya muda kuna dada nikazoeana nae alikua anakaa nyumba Hio, kumdadisi akaniambia wale wote ni wapangaji pale, nikawa nashangaa kwanini hamuhami kama Kila mwaka maji yanajaa na mnajua, akawa Hana jibu
Aisee mpaka naondoka huko niliacha wote bado wapo nyumba Hio, Kuna watu ni kama hao mafuriko wmezoea wanaishi nayo kibishi