Mafuriko Dar ushauri wa bure kwa vijana wanaotafuta maisha

Foffana

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2022
Posts
861
Reaction score
1,547
Habari za jioni wakuu straight to the point

Niwape ushauri vijana wenzangu ambao tumepanga huku mabondeni na ambao wanatarajia kupanga kuwa wasijaribu hiko kitu

Mafuriko yanarudisha sana nyuma hasa kwa vijana ambao tunahustle ili tuweze kutoboa

Leo asubuhi nilitoka kidogo ghetto kuna mishe nilikuwa naifuatilia sehemu mida ya saa 10 napigiwa simu kuwa maji yamejaa vibaya mtoni nikajitahidi kuwahi chap nikakuta ndo yanagonga mlangoni kufungua mlango sekunde kadhaa tu maji tayari magotini, nikafanikiwa kuliwahi godoro, nguo na vitu kadhaa ila feni,subwoofer,kifridge vyombo vidogo vidogo na kisofa vyote chali

Aisee vijana wenzangu hata kama kodi ni ndogo huku mabondeni na kulingana na kipato chetu inatulazimu kuishi huku.....tuikatae hii hali mafuriko yanarudisha sana nyuma

Wasalaaam
 
Daah hii mvua imekuja speed sana mzee , leo ndo sku ya kujua fundi wako wa mfumo wa maji taka ni mzuri au chenga , leo ndo sku ta kujua kiwanja ulichonunua ulinahatisha au umepigwa ....!! Mvua inamyeshaje non stop masaa sita bhana
 
Hayo maji ni ya mavi washafungulia mabomba yao. .
 
Aise pole
 
Wakazi wa dar Wana roho ya chuma, Kuna njia nilikua napita kipindi nipo chuo, msimu wa mvua kuna wakazi wa nyumba flani muda wote utakuta wanachota maji na ndoo ndogo kuyatupia barabarani, kiufupi nyumba ilikua inaingiza maji si mchezo

Baada ya muda kuna dada nikazoeana nae alikua anakaa nyumba Hio, kumdadisi akaniambia wale wote ni wapangaji pale, nikawa nashangaa kwanini hamuhami kama Kila mwaka maji yanajaa na mnajua, akawa Hana jibu

Aisee mpaka naondoka huko niliacha wote bado wapo nyumba Hio, Kuna watu ni kama hao mafuriko wmezoea wanaishi nayo kibishi
 
Ukihama wew kesho mwenzio anaingia.......kwaio hizi lawama za mafuriko ni continuosly
 
Kimbilia Goba mafuriko utaskia kama ya atokea nchi jirani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…