Mafuriko: Makanya, Same, Kilimanjaro

Mafuriko: Makanya, Same, Kilimanjaro

Hiyo hali imekuwa ni ya kujirudia rudia, sababu hilo eneo ni tambarare na mvua ya ukweli ikishapiga milimani kule...maji yote yanakuja tapikiwa huku bondeni ilipo barabara na reli...
 
Tuliambiwa mvua zitakuwa kubwa mikoa ya Morogoro , Pwani,Dar es Salaam, na Zanzibar. Morogoro ni Manyunyu...Kilimanjaro ambayo haimo kwenye orodha ni mafuriko!!
Unakaza ubongo, mafuriko inategemea na jiografia ya mahali husika wingi au uchache sio factor pekee
Makanya ni milima imezunguka hivyo maji yanatorokea katikati ambapo ndio barabarani
 
Unakaza ubongo, mafuriko inategemea na jiografia ya mahali husika wingi au uchache sio factor pekee
Makanya ni milima imezunguka hivyo maji yanatorokea katikati ambapo ndio barabarani
Kwa hiyo mkoa wa Kilimanjaro mvua ni ya manyunyu lakini milima ndiyo umegeuza manyunyu kuwa mafuriko.

Asante sana kwa ufafanuzi, tangu sasa nitalegeze ubongo.
 
Ajabu sana mwaka huu. Hayo maeneo ya Same na Makanya kuna ukame wa hali ya juu. Lakini pamoja na upungufu wa mvua katika maeneo mengi ya nchi yaliyokua yanapata mvua za kutosha eti leo hii Same na Makanya kumekua na mvua nyingi hadi zimeleta mafuriko
Maji ya mafuriko huwa yanatoka milimani huko, Chome, Tae, Vudee, Suji, Bwambo, Mamba na kwingine. Mvua ikipiga vizuri milimani, huko chini lazima kinuke.
 
Kwa hiyo mkoa wa Kilimanjaro mvua ni ya manyunyu lakini milima ndiyo umegeuza manyunyu kuwa mafuriko.

Asante sana kwa ufafanuzi, tangu sasa nitalegeze ubongo.


Makanya ipo Same Magharibi, Upande wa mashariki IPO Safu ya milima ya Upare. Makanya kutokana na IPO nyuma ya milima ya Upare haipokei Upepo wa bahari unaoruhusu Precipitation ku-take place Hali inayofanya eneo Hilo kuwa na mvua hafifu na kusababisha Hali ya unusu jangwa(Semi arid desert). Hivyo mvua nyingi hunyesha mashariki ya Same huko milimani na tambarare ya mashariki ya Same.

Mashariki ya Makanya ilipomilima ndio juu hivyo mvua zikinyesha huko maji yake huelekea Makanya mpaka Ruvu Ulipo MTO Ruvu.

Maeneo mengine yenye Hali ya Makanya ni Hedaru, Saweni, Nkwini, Kirinjiko, Same, n.k.

Hivyo Makanya mvua inaweza isinyeshe au isiwe kubwa lakini yakawepo mafuriko yanayotoka milimani huko, chome, Suji,mamba, n.k

Ni Kama upande wa nyuma wa mlima Kilimanjaro kule Kenya kuna Hali ya ujangwa kutokana na kuwa upepo wa bahari unavuma ukitokea Kusini mashariki huku Tanzania
 
Makanya, Same, Kilimanjaro, barabara haipitiki kwa sababu mvua imesababisha maji kupita juu ya daraja, na kusababisha msururu mrefu wa magari yanayotoka na kuingia Mkoa wa Kilimanjaro.

Mamlaka husika, hususani Mkoa wa Kilimanjaro, zichukue hatua za dharura kunusuru abiria na magari, na pia hatua za kudumu zichukuliwe, ikiwemo apanuzi wa daraja hapa Makanya.

Tumekwama hapa Makanya kuanzia saa tano usiku.

NB: Mamlaka husika Mkoa zikae standby, ikiwemo kuongoza magari, ili kuwepo na Usalama na kuepusha madhara.

Picha sijapiga ni usiku sana na mvua inanyesha bado.
Tumekupata Hassan Ngoma,,Mkuu wa Wilaya mchovu!!!
 
Back
Top Bottom