Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Tuliambiwa kuwa Bunge litapovunjwa au kukaribia kuvunjwa,Wabunge wa upinzani, hasa wa CHADEMA, wangehama kwa wingi mithili ya maji ya mafuriko kwenda CCM na kwamba CHADEMA ndio ingekufa rasimi.
Swali: Mafuriko hayo yako wapi?
Je, wale Wabunge Bunge wa viti maalumu waliohama hivi karibuni, ndio hao ambao tuliambiwa wangesababisha mafuriko?
Na je, kaburi la CHADEMA liko wapi?
Watu wanaoendelea kuhamia CHADEMA kutoka vyama vingine kama kina Felix Mkosamali, wanatoa ujumbe gani kwa wanaodai CHADEMA inakufa?
Kwa sasa, tusubiri hatima ya kitisho kingine kutoka kwa watu walewale kuwa CHADEMA itaambulia wabunge wachache sana safari hii au isipate mbunge hata mmoja.
Jambo lingine, subirini kuona hamasa ya wananchi kwenye mikutano ya kampeni ya wapinzani huku nyie mkitegemea wasanii wa muziki wawasaidie kujaza mikutanon yenu.
Ukweli usiosemwa au kutojulikana kwa wengi:kuna mtu alifikiri mpaka tunaingia kwenye kampeni,upinzani utakuwa umeshasambaratika kabisa na kwamba asingepata tabu au ushindani wowote katika harakati zake za kurudi ofisini kwa awamu ya pili jambo ambalo mpaka sasa limefeli hivyo ajiandae kupambana kwani hakuna ushindi wa mezani hata akitangazwa mshindi.
Mungu si Magu!