Jack HD
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 851
- 1,168
Habari wanajukwaa,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Nimekuwa mfugaji wa kuku wa nyama kwa miaka kadhaa na nimefikia wakati nimenotice soko la kuku kutokuwa zuri hususani kuelekea mwishoni mwa mwaka hasa mwezi november tofauti na kasumba tunayoijua ya mwishoni mwa mwaka kuna high demand ya kuku.
Kumekuwa na sababu mbalimbali kutoka kwa wafugaji ambazo zinaenea kwa kasi katika mwezi huu tu, ikiwamo serikali imeruhusu vifaranga kutoka nje kuingia nchini. Kuna vifaranga vya Zambia vinasemekana vimeingia na wanafungwa maeneo mbalimbali kwenye jiji la Dares Salaam. Pili, kuna taarifa ya Waziri ilitolewa kuhusu kuwashirikisha wenzetu kutoka Uholanzi juu ya kutatua Uhaba wa Kuku nchini, kibaya taarifa hii imefika kwa wakulima kuwa Uholanzi imeanza kusupply kuku waliochinjwa kuja Tanzania na kupelekea soko la Kuku Kushuka. Miezi iliyopita mpaka kufikia mwezi wa kumi ilishuhudiwa Kuku kuuzwa kati ya Tshs. 5300-5800 Kulingana na ubora wa kuku.
Leo hii soko la kuku huyo huyo limefikiwa wastani wa Tshs 4500 - 5000 na bado kuku hawauziki kwa kusemekana kuku wamekuwa wengi na ni wakubwa kuliko kipindi cha nyuma. Nini Tatizo? Nafahamu JF ni kijiji kilichokusanya watu wa kada na kutoka kwenye taaluma mbalimbali, hivyo jibu litapatikana.
Nawasilisha!!