Mafuriko ya kuku wa nyama Dar es salaam na bei kushuka nini chanzo?

Kwani jeshi haliwezi kuingilia kati likanunua kuku wetu wote ?
 
Badili mfumo hamia kwa kuku wa mayai ingawa ufugaji wake ni gharama kidogo au ufuge wa mayai ya kienyeji soko lake halishukagi kirahisi na ningumu kuwa imported kutoka popote
 
Nina kuku zangu saba za kienyeji home nasubiria bei ifike 100k[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Peleka uholanzi
 
Kuna jirani yetu alikua anafurahi kila anaposikia hakuna nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi, alikua anaongelea kooni kwa kisema "NAA BAADO" Kibri chote kimeisha na mstaarabu mno, mtaani anaitwa mpya.
kijumla hii hali Heshima inakuja.
 
Wanunuzi mifuko imetoboka,vyuma baba vyuma........
 
What I suggest serikali kuziba mipaka kuruhusu ndani tu mzunguko wa kuku hii itarejesha heshima ya soko kama nyuma
 
In short sio kuku tu. We fatilia hata mazao ya wakulima wa tz kma matikiti, maembe, machungwa, vitunguu. Hivi vyote vimeporomoka bei.


Sababu ni kuwa watu hawana pesa. Sasa mfanyakaz mwaka wa 3 hajaongezewa mshahara mnatgmea nn?
Na bei ya magari nayo imeshuka?
 
Ikumbukwe ni sisi wenyewe wananchi tulipiga sana kelele serikali ilipoamua kuwa strict na uingizaji holela wa vifaranga na kuku. Kelele zilipigwa sana.

Kwa hiyo kwa serikali kuregeza msimamo ili kuongeza uingizaji wa vifaranga na kuku, Mimi naona ni ku respond kwa matakwa ya wananchi.

Ushauri wangu, sababu tuna serikali iliyoonyesha nia ya dhati ya kuendeleza uzalishaji wa ndani, ni vema wafugaji wakawa na chama imara kitakachotoa ushauri muafaka kwa serikali hasa kuhusiana na kadhia tunayoijadili.
 
Chanjo ambayo haikuhifadhiwa vizuri ukawapa kuku wako na kisha wakafa wewe kama mfugaji unajuaje kua hii chanjo haikua na ubora? Na baada ya kuku kufa ulienda kwa daktari akafanya postmortem na kukupa matokeo kua wamekufa kwasababu ya chanjo haikua na ubora? Kuna magonjwa yakuzuiliwa na chanjo na mengine yanatibiwa na dawa hivyo hatakama umewapa kukuwako chanjo haimaanishi kua hawatakufa na ugonjwa mwingne (ambao hauna chanjo)!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…