Another issue ambayo nilkuwa nafikiria sana!! Hivi ni Nyumba gani bongo zenye steel reignforced concrete? Halafu wajenzi wetu hujali tetemeko wakati wana-plan ujenzi? Ikitokea tetemeko kama hili, hivi Dar is-itakuwa flat! Acha vile vibanda vya mikoani?
Wajenzi mpo??
Dear I.O
Wajenzi tupo, tupo kabisa, kwa ajili ya taifa na wananchi
Sijajua wangapi wamechukulia hii thread kama 'jicho' la kuangalia kila kitu hapa nchini.
Ujenzi wa majengo(maghorofa) ya Tanzania, yako reinforced kwa kutumia steel.
Katika ujenzi inategemea hasa data za earthquake kwa miaka 50 au 100 iliyopita. Na hizi huwa zinatumika katika ujenzi, mathalani Dar es salaam record ya juu ya earthquake let say 3.0 magnitude. hivyo majengo mengi yanakuwa designed kwa hiyo record. Jengo la kawaida kabisa ambalo limekuwa reinforced na designer haku-consider earthquake linaweza kuhimili 2-2.5 Magnitude(inategemea na aina ya ujenzi)
Let say tunaamua leo kujenga majengo ya ghorofa yenye uwezo wa kuhimili 7.0 magnitude iliyotokea Haiti, tatizo lake ni gharama na owners wengi huwa hawataki kusikia hizo unforseen disaster zikitamkwa.
Tanzania yapo majengo imara sana siyo tu yanaweza kuhimili eathquake kubwa, bali hata terrorism attacks! ujenzi wa Tanzania unategema nani anajenga na ana ufahamu gani, siyo majengo yote yako hatarini!
Pili, hakuna Tanzania standard ya ujenzi wa majengo yake, we are using British(BS), Euro, USA n.k sana sana (TBS) wanajitahidi hapa na pale, japo kazi yao ni copy and paste ya BS).
Hatuna regulation ya majengo inayoendana na hali ya Tanzania, na iliyotayari kuhimili hizo disaster.
Wajenzi hawana tatizo( robot) tell them what to do, tena Tz civil engineers are doing very good job probably more than any other engineers. So ujenzi hauanzii kwa designer au contractor unaanzia kwa mmiliki na archtects wake, wao wanampa structural designer(yeye atawashauri kile anachoona kitafaa, msemaji wa mwisho ni archtects)
Due to global climate change ,these disasters for sure one day we may cry, research za wenzetu wanasema developing countries ndio tutaathirika sana. Ni jukumu la serikali kuweka requlations na kuzisimamia, na kuzi-update kila mara haya matatizo yanapotokea.swali ni kuwa wata update regulation zipi? wakati hazipo!!
Leo kwa mfano tunaweza kupitisha sheria kuwa lazima kila jengo liwe designed kwa ku-resist earthquake let say of 10.0 R , ujenzi wake ni gharama sana, sana, na wachache sana watakaoweza ku-afford, but at least yakitokea matatizo kama ya Haiti tunakuwa kwenye safe side.
Sasa hapa key players ni
serikali, mabenki yanayotoa loan, owners waelimishwe na ERB wasimamie hizo designs na ujenzi.
Leo kwa sababu tunaringa tuna matetemeko ya ardhi madogo, nyumba nyingi zimejengwa kwa standard za hali ya sasa. We need our standard, na kutokuwa na standard ni alama tosha kuwa serikali haitumii wataalamu wake.
we need smart leaders