GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 4,291
- 5,786
Ni rahisi sana kunena na kutoa ahadi ambazo utekelezaji wake ni mgumu sana. Simkatishi tamaa lakini akumbuke kuwa AICC iliishafikia kilele cha mafanikio na jitihada zake zitafananishwa na mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya.
AICC tayari iko kweye ushindani na ndugu yake JNICC, lakini najaribu kuvuta taswira ya Dodoma ambayo ni makao makuu ya nchi kama itathubutu kuwepo bila ukumbi wa mikutano ya kimataifa. Hata kama Kizota itakuwa mkombozi kwa Dodoma, Swali linakuja kwa nchi jirani ya Rwanda ambayo ndio mshindani mkubwa wa AICC.
Mheshimiwa sana Mafuru amejipanga vipi kwanza kubadilisha au kuboresha mazingira ya kazi na miundombinu ya AICC kufikia kiwango cha kushindana na Kigali International Conversion Center? Vipi kuhusu nguvukazi watu, tuko vizuri kushindana na wakenya? waganda? wanyarwanda? warundi? .... Nadhani hata wakongo na wasudan wametutangulia sana kwenye nyanja za kimataifa. Kila la kheri Mheshimiwa sana Mafuru.