Mafuta na gesi ya Russia yaendelea kwenda kwa wingi India, China na nchi za EU. Hizo za ulaya wanayanunua kwa rubles

Mafuta na gesi ya Russia yaendelea kwenda kwa wingi India, China na nchi za EU. Hizo za ulaya wanayanunua kwa rubles

Wewe ndio ujibu unayejitia mjuzi kuwa kampuni za Urusi wamiliki warus tu isi unajifanya mjanja

Putin hana Jeuri kuwekea vikwazo nchi za Magharibi japo wamemuwekea vikwazo kibao kampuni zote kubwa za Urusi ziko soko la hisa Magharibi ndiko wanatoa mitaji yao

Wanampiga vitani na kwenye mitaji.mpuuzi mkubwa

Putin lofa tu yule na Urusi yake
unahemwa tu.amesema juz wao wapo tayar ku cooperate na any one sas ina faid gan kufuta had timu za mpira au za kwenye game au
 
Vita ni uchumi, vita ni pesa... bahati mbaya watu hawaangalii sana kwenye angle hii. Juzi waziri mkuu wa uingereza alikua Ukraine, pamoja na kutoa misaada pia walitoa mikopo mikubwa sana kwa Ukraine.

Vivyo hivyo USA na world bank wameikopesha pesa nyingi sana Ukraine, mara baada ya vita Ukraine itakua na madeni makubwa sana, pengine hayo madeni yatadumu miaka na miaka.

Rejea Marshall plan ya ku re boost uchumi wa ulaya toka marekani. Mpaka leo ulaya anadaia na USA... ndio maana anapelekeshwa kama mjinga.
Hii ni kweli kabisa, nilishangaa World Bank kutoa Mkopo kwa Ukraine ambayo IPO vitani.
 
January makamba bila hata ya aibu jana anadiriki kusimama na kukiri kuwa yeye na wizara yake nzima wamekosa "way forward" ya kufanya kuhusu swala la mafuta (hopeless kabisa), mpaka anafikia hatua ya kukaribisha watanzania wenye maoni/Ushauri nzuri wa nini cha kufanya ili kuweza kujitokeza kuishauri wizara yake.
Sasa ni wiki sita tangu vita ya Russia vs USA inayopiganiwa Ukraine ianze. Hakuna dalili ya vita hii kumalizika siku za karibuni. Na kuna uwezekano wa kugeuka kuwa vita ya kinuklia mbaya ambayo haijawahi kutokea hapa duniani.

Kabla ya vita hii, India ilikuwa inanunua asilimia 2 hadi 5% tu ya mahitaji yake ya mafuta haya kutoka Russia sawa na ambavyo USA ilivyokuwa inafanya. Asilimia kubwa iliyobaki walikuwa wanayanunua toka Saudi Arabia, Arab Emirates na Nigeria. Yale ya Iran yalipigwa ban tangia mwaka 2011 na jumuiya ya kimataifa inayoongozwa na USA.

Baada ya vita, kuanzia mwezi March mwaka huu mafuta yote ambayo India inanunua kutoka nje yanatoka Russia kwani bei yake ni zaidi ya nusu ya yale yanayotoka nchi zingine ambazo zimepandisha maradufu bei zake kwa kisingizio cha vita.

China ni wajanja zaidi. Wao wanachojali ni wapi watapata bei nafuu, hayo mengine ya kisiasa si ya muhimu hata kidogo.

Hivyo baada ya ban ya kimataifa kwa mafuta ya kutoka Iran tangia mwaka 2011 iliyopelekea mafuta ya Iran kuporomoka bei, waliendelea kuyanunua kimya kimya. China ndiyo mteja mkubwa wa mafuta ya Russia hata kabla ya vita hii. Mwaka 2021 China ilikuwa inanunua mapipa million 1.72 kwa siku. Baada ya vita mafuta yake yote inayanunua toka Russia, tena wazi wazi despite kubembelezwa na USA isifanye hivyo.

Pamoja na kelele za kisiasa zinazopigwa na nchi za Ulaya kupiga ban ununuzi wa gesi na mafuta ya Russia, ukweli ni kuwa nchi hizi zinaendelea kuyanunua kutoka Russia kwa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na kabla ya vita. Ukweli ni kuwa nchi hizi za ulaya haziwezi ku survive bila ya gesi na mafuta ya kutoka Russia. Zaidi ya asilimia 40% ya gesi inayotumika majumbani kwao na kwenye viwanda vyao inatoka Russia na hawana sehemu nyingine ya kuipata.

Nchi kama Ujerumani inategemea kwa asilimia 100% mahitaji yake ya gesi na mafuta toka Russia. Na kwa sababu ya kelele zao Russia imewalazimisha kununua gesi na mafuta hayo kwa pesa ya urusi inayoitwa rubles.

Hawana ujanja, wanayanunua kwa rubles kimya kimya. Bila gesi toka Russia wananchi wao watakufa nyakati za winter kwa kukosa household heating system majumbani kwao. Russia ikiamua kulifunga hilo bomba lake linalopeleka gesi na mafuta huko nchi za ulaya, viwanda vingi vya ulaya vitashindwa kufanya kazi na wananchi wao watakufa kwa baridi kwa household heating systems zao kuzimika.

Huo ndiyo ukweli. Ni jambo la muhimu na sisi tukafanya hivyo. Na tunaipongeza serikali yetu ku abstain kwenye kura huko UN security Council kama.ambavyo China na India walivyofanya kwa manufaa haya ya taifa letu.

Sasa kuna faida gani ya sisi ku abstain kwenye votes hizo? Wizara ya nishati haiwezi kukwepa kuwajibika na hali hii.

 
duh ila we jamaa mwongo!! ndo maana unashindwa hata kupangilia sentensi vizuri, maneno mengi hayasomeki vizuri kisa uongo, unakimbizana na keyboard ili uingie uzi mwingine ukaendelee kudanganya.... ila we jamaa muongo
Mkuu jamaa liongo sana. Linaleta story za vijiweni
 
Back
Top Bottom