Mkuu hii kitu me niliipata kwenye kidole cha kati mkono wa kulia. Hatari. Wengi wakasema nitumie dawa za kienyeji, nilitumia hadi mzigo ukaiva. Lakini nilikuwa napata maumivu muda wa kulala maana mapigo ya moyo unayasikia yanapigia kwenye kidole.
Kijijini walikuwa wanakamua daily but usiku ngoma inajaa tena. Kidole kikaanza kutoa harufu. Ikabidi niombe waniwahishe zahati, ilikuwa jmos, zahanati pamefungwa. Nikaenda home kwa mganga. Akanichoma sindano ya ganzi then akachana sehemu kubwa na wembe akatoa uchafu wote. Akanifunga na bandage then akaniandikia dawa za kuwa nameza. Akanishauri niwe naenda clinic kusafishwa kila baada ya siju moja.
Hiyo siku nakumbuka nililala fresh, kidole hakikuuma hata kidogo. Nikapata doctor mstaafu wa jeshi ana pharmacy yake sehem. Nikawa naenda clinic. Huyo doctor alikuwa kiazi kishenz, kila nikienda anatoa bandage anaweka dawa then anafunga nyingine.
Week mbili kidole hakina dalili ya kupona. Nikawashilikisha wazazi maana wakati wote nilikuwa na bro tunahangaika. Wazee walinimind but wakanipeleka kwa nurse flani mbobezi wa vidonda. Yule nurse aliponiona akaifumgua ile bandage, kidole kilikuwa kimeanza kuoza. Mamangu alitoa machozi, nurse akaitoa ngozi yote ya kidoleni maana ilikuwa siyo ngozi tena. Kidole kilikuwa kimeanza kutunga funza. Yule nurse alinihudumia vizuri sana. Alinisafisha kidonda akanipa vifaa na kunielekezakujihudumia mwenyewe. Balaa likaanza kidole kikawa kinajikunja hakitaki kunyooka. Nikaanza kuwa naenda nurse ananinyoosha maana maza anahuruma sana. Hadi nilipona kabisa
View attachment 1903980