Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Kuna watu wanamhujumu Mheshimiwa Rais na pengine yeye hajui hili. Kwa sasa huku mitaani mafuta ni adimu sana, na pale ambapo yanapatikana basi bei yake haishikiki. Dumu/Ndoo ya Lita 20 iliyokua ikiuzwa TZS 70,000/- mwezi wa sita mwaka jana leo inauzwa TZS 140,000/-
Aliekua Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alipata kusema kua sababu ya kupanda huku ni kuadimika Kwa vibarua huko Malaysia sababu ya COVID-19. Kigoma inaongoza Tanzania Kwa kuzalisha chikichi, je wameweza kuchukua mazao yote yanayozalishwa pale mpaka yakaisha imebidi waagize Malaysia sasa?
Kwanini wasi encourage na ku facilitate kilimo hiki Kwa hapa Tanzania mpaka tulazimike kuagiza nje? Singida wanalima sana Alizeti, na mikoa ya kusini wanalima sana Ufuta, je mazao haya yamechukuliwa yote na bado kukawa na upungufu wa mafuta?
Haya maeneo (Singida na Mikoa ya Kusini) bado kuna mapori mengi tu, kama wanazalisha malighafi za mafuta na bado hazitoshi kwanini Serikali isiwawezeshe basi kuongeza zaidi maeneo ya kulima kwenye hayo mapori yaliyobaki ili kuongeza zaidi malighafi hizi?
Sasa kuna Hussein Bashe kwenye hii Wizara, nilidhani ni mtu Smart lakin naona nae mfumo umemmeza, amesha adopt tabia za mfumo alioko. Juzi nimemsikia akiwa mkali kweli kweli juu ya kupanda Kwa mbolea kutoka 108,000/- Kwa gunia mpaka 140,000/-, lakini nimkumbushe tu hata hiyo 108,000/- bado tunapigwa, kwani hapo kabla ilikua haizidi 60,000/-
Mafuta Sasa hayako tena mitaani, wenye vigenge/duka wanasema Kwa yalivyopanda bei hata wakiyaleta hawajui watauzaje. Mafuta yanagusa kila mtu, isije ikawa ni bomu linategwa kwenye most consumable products ili likilipuka liguse sehemu kubwa ya watu. Zama hizi za "Kazi Iendelee" tunashuhudia mfumuko mkubwa wa Bei.