Mafuta ya kupikia yaadimika mitaani

Mafuta ya kupikia yaadimika mitaani

Hatuna watunga sera wazuri;
Kwa ukubwa wa ardhi ya Tanzania; serikali inashindwa kutengeneza mazingira bora kwa wakuli wa mazao muhimu kama alizeti na chikichi kwa ajili ya uzalishani wa mafuta ya kula?
Wizara imejaa maandiko na mipango lakini hakuna utekelezaji. Kila siku ni maneno ya ''tutafanya'' na wala husikii waziri wa kilimo akisema ''tumefanya''
Tunaishi tu bila mipango endelevu.

Lakini wanasiasa hawaishi kusema kuwa tunajitosheleza.

Tumekabidhi hatma ya taifa kwa watu wasio na mipango ila wana maneno mengi mazuri.

KIla kinachotokea duniani kinaongeza ugumu wa maisha kwa mtanzania.

Uliyosema ni ya kweli, serikali kuzindua mipango ya kwenye makaratasi isiyo wezeshi kwa ilo tunajitahidi. Ikija utekelezaji utasikia hovyo hovyo hakuna cha maana.
 
Wanamuhujumu ?

Duh watu tunapenda kupewa credit lakini hatutaki kuchukua lawama..., kama ni mtu wa kuhujumiwa basi huenda sio tactician na hio kazi haimfai..., inabidi aweke watu wa kutokumuhujumu....

Na haya mambo ya kupenda Soko Huria tu pale bei zinaposhuka haifai..., inabidi tukifurahia wakati bei ya kutupa hence shida kwa wauzaji, basi tukaze buti pale zinapopanda hence shida kwa sisi watumiaji (Ila all in all Tatizo la Tozo na Makodi mara nyingine ndio linapelekea bei kutokushuka sana)

Kama wakulima tu wanakosa mbolea kwa bei rafiki utasema kweli tuna nia kama nchi ya kumsaidia a common mwananchi ? (Obviously hata kama bila Ukraine wala Corona hapo lazima kutakuwa na knock on effect kwenye mambo mengi), After all tunalaumu Corona.., huenda bila hilo janga hizi nyimbo za madarasa tungekuwa hatuziimbi
 
Tatizo pia serikali yetu si wezeshi linapokuja swala la kuplan kwa ajili ya muda mrefu utasikia sera sera za miaka 20 lakini hakuna cha maana.

Tuweze niche ndogo za kilimo tuwatoe wanaolima hekari chache kua wakulima wa hekari nyingi.
Si mpango wa wanasiasa huo! Huu ushenzi unaoendelea una baraka za watawala na ndio maana huwezi ona ukiisha. Ukiwa mzalendo wanakuua kwa sababu uzalendo hauendani na ufisadi.

Kinacholiponza hili taifa hakuna vipaumbele wala visionary leaders ila kuna politicians kwenye strategic positions.

Kuna billions of money za kukodisha mfumo wa kuendeshea shirika ila hakuna hela kwa ajili ya ku support kilimo kwenye taifa. Kuna billions za kusaport vitu visivyo na tija ila hakuna hela ya kufanya mambo muhimu.

Kuanzisha estate za kilimo ambazo watu watazalisha malighafi kwa ajili ya ku process mafuta na kutumia ndani ya nchi pia ku export hazimalizi hata trillion 1 ila tunaweza kuimaliza hio hela kufanyia mikutano kulipana posho na anasa za ajabu ajabu.
 
Si mpango wa wanasiasa huo! Huu ushenzi unaoendelea una baraka za watawala na ndio maana huwezi ona ukiisha. Ukiwa mzalendo wanakuua kwa sababu uzalendo hauendani na ufisadi.

Kinacholiponza hili taifa hakuna vipaumbele wala visionary leaders ila kuna politicians kwenye strategic positions.

Kuna billions of money za kukodisha mfumo wa kuendeshea shirika ila hakuna hela kwa ajili ya ku support kilimo kwenye taifa. Kuna billions za kusaport vitu visivyo na tija ila hakuna hela ya kufanya mambo muhimu.

Kuanzisha estate za kilimo ambazo watu watazalisha malighafi kwa ajili ya ku process mafuta na kutumia ndani ya nchi pia ku export hazimalizi hata trillion 1 ila tunaweza kuimaliza hio hela kufanyia mikutano kulipana posho na anasa za ajabu ajabu.

Uliyosema yana kweli ndugu yangu
 
Tatizo pia serikali yetu si wezeshi linapokuja swala la kuplan kwa ajili ya muda mrefu utasikia sera sera za miaka 20 lakini hakuna cha maana.

Tuweze niche ndogo za kilimo tuwatoe wanaolima hekari chache kua wakulima wa hekari nyingi.

Hata hao wanaolima hekari chache kuna saa wanakosa masoko ya uhakika hizo hekari nyingi wakishalima ndio watazipeleka wapi ?

Yaani tunataka mkulima awe Mtaalamu Kilimo, Mtaalamu wa Masoko , Financial Guru na vilevile speculator wa nini kitapanda bei saa ngapi ? (utagundua huyo sio mkulima per se bali ni an entrepreneur ambao majority hawawezi wakawa hivyo); Kwahio Wizara za Kilimo / Biashara n.k. ziwasaidie kwanza hawa waliopo kupata masoko ya uhakika
 
Si mnamshabikia Putin?

Tanzania inazalisha 45%ya mahitaji yake ya mafuta ya kula na huagiza 55% toka Malaysia, India na Uturuki.

Duniani mzalishaji mkubwa wa mafuta ni Ukraine, sasa baada ya uvamizi wa Urusi, Ukraine amestop uzalisha na Rassia anaemfuatia amewekewa vikwazo hivyo mafuta ya Uturuki saivi yanaenda ulaya na ya Malaysia yanaenda Japan na Korea ili kuziba pengo la mafuta ya Urusi na Ukraine ambapo hayapo sokoni. Na Korea na Japan wananunua Bei nzuri kuliko sisi

Mungu ajalie mvua Ifike mwezi wa 4 nivune alizeti yangu ni jenge.
Kila kitu mnasema Ukraine na Russia inazalisha mbna waongo sana nyie
 
kinachofanyika hapo ni ulanguzi hiyo vita ya Ukraine ni sababu ya kuhalalisha.
Hii ni fursa kuna kundi lilikuwa linaisubiria kwa hamu. Awamu hii ukijua mahali pa kusimama utabeba hela kwenye sandarusi
 
Mafuta ni anasa,waongezee tu bei mpaka ifike laki tano ndoo la lita 10
Kwakweli usipo tia mafuta huwezi kufa,kuna vitu vya kuongelea ila sio mafuta, wazee wa zamani waliishi vipi?
Watu wa vijijini wanaishi vipi?

Mnawapa kichwa hawa jamaa ndio maana wanapandisha
Mkiona yanapanda suseni achen msinunue tuone kama watakuwa na jeuli,nasema tena mnawapa kichwa

Hivi unajua kama demu ukipenda kumsifia muda wote anakutunia,ndio kinachoendelea kwenye mafuta hebu suseni, karanga zipo, nazi zipo, nchi ina utajiri wa viungo bado mnalialia utafikiri mmenyimwa pumzi,kuweni serious basii,
 
Kuna watu wanamhujumu Mheshimiwa Rais na pengine yeye hajui hili. Kwa sasa huku mitaani mafuta ni adimu sana, na pale ambapo yanapatikana basi bei yake haishikiki. Dumu/Ndoo ya Lita 20 iliyokua ikiuzwa TZS 70,000/- mwezi wa sita mwaka jana leo inauzwa TZS 140,000/-

Aliekua Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alipata kusema kua sababu ya kupanda huku ni kuadimika Kwa vibarua huko Malaysia sababu ya COVID-19. Kigoma inaongoza Tanzania Kwa kuzalisha chikichi, je wameweza kuchukua mazao yote yanayozalishwa pale mpaka yakaisha imebidi waagize Malaysia sasa?

Kwanini wasi encourage na ku facilitate kilimo hiki Kwa hapa Tanzania mpaka tulazimike kuagiza nje? Singida wanalima sana Alizeti, na mikoa ya kusini wanalima sana Ufuta, je mazao haya yamechukuliwa yote na bado kukawa na upungufu wa mafuta?

Haya maeneo (Singida na Mikoa ya Kusini) bado kuna mapori mengi tu, kama wanazalisha malighafi za mafuta na bado hazitoshi kwanini Serikali isiwawezeshe basi kuongeza zaidi maeneo ya kulima kwenye hayo mapori yaliyobaki ili kuongeza zaidi malighafi hizi?

Sasa kuna Hussein Bashe kwenye hii Wizara, nilidhani ni mtu Smart lakin naona nae mfumo umemmeza, amesha adopt tabia za mfumo alioko. Juzi nimemsikia akiwa mkali kweli kweli juu ya kupanda Kwa mbolea kutoka 108,000/- Kwa gunia mpaka 140,000/-, lakini nimkumbushe tu hata hiyo 108,000/- bado tunapigwa, kwani hapo kabla ilikua haizidi 60,000/-

Mafuta Sasa hayako tena mitaani, wenye vigenge/duka wanasema Kwa yalivyopanda bei hata wakiyaleta hawajui watauzaje. Mafuta yanagusa kila mtu, isije ikawa ni bomu linategwa kwenye most consumable products ili likilipuka liguse sehemu kubwa ya watu. Zama hizi za "Kazi Iendelee" tunashuhudia mfumuko mkubwa wa Bei.
Mafuta sehemu nyingi tuu sio tz tu. Nilikuwa nafikiri sababu ni vita ya Ukraine
 
Mafuta sehemu nyingi tuu sio tz tu. Nilikuwa nafikiri sababu ni vita ya Ukraine
Hawa Wa Ukraine na Urusi mnawasingizia, wameanza kuchapana February tu hapa, mafuta yamepanda toka mwaka jana. Mmeapata Sababu Kwa kila kitu sasa, pengine hata Nyanya zikiadimika tutaambiwa ni vita y Urusi vs Ukraine.

Shida tunaishi ili tupitishe siku muda wetu uishe waje wengine. Sio tunaishi ili tufurahie Maisha. Mipango kazi ya kwenye makaratasi ni mingi sana lakini utekelezaji hakuna. Watu wanalipwa mishahara minono tu na marupurupu ya kutosha Sababu ya mipango hewa.

Hawa hawawezi kuona tabu ya mfumuko wa bei ulioko sababu ya vipato vyao, au pengine wao ni sehemu ya Sababu za huo mfumuko (Rushwa).

Kwa mapori yaliyoko hapa Tanzania haikufaa leo tupate tabu ya mafuta kisa tu vibarua hakuna Malaysia, au Urusi anamchampa M Ukraine. Ingekua hatukuwahi kulima Ufuta, Chikichi au Alizeti hapo sawa, lakini vipo hivi hapa kwetu.

Tumezoea siasa Kila mahali,
 
Kamati iingie 'field' kwa wazalishaji, waje na 'facts' za sababu zinazosababuisha mafuta kupanda bei, na nini kifanyike ili yaweze kushuka.
 
Tuanze kula chuku chuku mkuu Ni nzuri kwa afya
 
Ni uzembe wetu hatuoni fursa ardhi tele tupu tumeshindwa panda mafuta ya kula hadi tuna import
 
Back
Top Bottom