Mafuta ya kupikia yaadimika mitaani

Mafuta ya kupikia yaadimika mitaani

Kuna watu wanamhujumu Mheshimiwa Rais na pengine yeye hajui hili. Kwa sasa huku mitaani mafuta ni adimu sana, na pale ambapo yanapatikana basi bei yake haishikiki. Dumu/Ndoo ya Lita 20 iliyokua ikiuzwa TZS 70,000/- mwezi wa sita mwaka jana leo inauzwa TZS 140,000/-

Aliekua Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alipata kusema kua sababu ya kupanda huku ni kuadimika Kwa vibarua huko Malaysia sababu ya COVID-19. Kigoma inaongoza Tanzania Kwa kuzalisha chikichi, je wameweza kuchukua mazao yote yanayozalishwa pale mpaka yakaisha imebidi waagize Malaysia sasa?

Kwanini wasi encourage na ku facilitate kilimo hiki Kwa hapa Tanzania mpaka tulazimike kuagiza nje? Singida wanalima sana Alizeti, na mikoa ya kusini wanalima sana Ufuta, je mazao haya yamechukuliwa yote na bado kukawa na upungufu wa mafuta?

Haya maeneo (Singida na Mikoa ya Kusini) bado kuna mapori mengi tu, kama wanazalisha malighafi za mafuta na bado hazitoshi kwanini Serikali isiwawezeshe basi kuongeza zaidi maeneo ya kulima kwenye hayo mapori yaliyobaki ili kuongeza zaidi malighafi hizi?

Sasa kuna Hussein Bashe kwenye hii Wizara, nilidhani ni mtu Smart lakin naona nae mfumo umemmeza, amesha adopt tabia za mfumo alioko. Juzi nimemsikia akiwa mkali kweli kweli juu ya kupanda Kwa mbolea kutoka 108,000/- Kwa gunia mpaka 140,000/-, lakini nimkumbushe tu hata hiyo 108,000/- bado tunapigwa, kwani hapo kabla ilikua haizidi 60,000/-

Mafuta Sasa hayako tena mitaani, wenye vigenge/duka wanasema Kwa yalivyopanda bei hata wakiyaleta hawajui watauzaje. Mafuta yanagusa kila mtu, isije ikawa ni bomu linategwa kwenye most consumable products ili likilipuka liguse sehemu kubwa ya watu. Zama hizi za "Kazi Iendelee" tunashuhudia mfumuko mkubwa wa Bei.
Nchi hii kila siku ni mipango tu, utadhania uhuru tumekabidhiwa jana!!hakuna kiongozi mwenye nia ya dhati ya kukuza kilimo nchi hii, huko kwenye mafuta ya kula ndiko achana napo kabisa, wastani kwa Tz kwa mwaka mahitaji ni tani 600, 000, lakini uwezo wa ndani ni tani laki 2 tu, hilo gape la tani laki 4, lazima liagizwe toka nje!!leo watakwambia kuna kilimo kikubwa cha michikichi kinaendelea huko kigoma!!subilia uone baada ya miaka 10 mbele, kama hutasikia story hizi hizi tu!!!Na aliyetibua soko la mafuta ya kula nchini ni jiwe, na sera zake mbovu, za kuongeza kodi kwa mafuta ya kula ambayo hayajasafishwa, na waingizaji kushindwa kabisa kuyaingiza!!ndipo chanzo cha tatizo kilianzia.
 
Punguzeni kulaumu kla kitu yan Wabongo tumekua waty wa lawama kla sku tufanyeni kaz tuache Siasa
Mafuta lawama
Umeme kodi lawama
Polisi lawama
Simu kulipa miamala lawama
Ttzo letu wabongo tunapenda starehe uwezo wetu mdg tujipangeni upya maisha yamebadilika
Tujifunzeni kuishi kulingana na vipato vyetu rasivyo tutakua watu wa lawama kla sku
 
Punguzeni kulaumu kla kitu yan Wabongo tumekua waty wa lawama kla sku tufanyeni kaz tuache Siasa
Mafuta lawama
Umeme kodi lawama
Polisi lawama
Simu kulipa miamala lawama
Ttzo letu wabongo tunapenda starehe uwezo wetu mdg tujipangeni upya maisha yamebadilika
Tujifunzeni kuishi kulingana na vipato vyetu rasivyo tutakua watu wa lawama kla sku
Tatizo hiyo mifano uliyotoa hapo pesa zote zinaishia kwa wajanja wachache tu halafu tukae kimya ingekuwa zinaenda serikalini moja kwa moja hapo sawa
 
Punguzeni kulaumu kla kitu yan Wabongo tumekua waty wa lawama kla sku tufanyeni kaz tuache Siasa
Mafuta lawama
Umeme kodi lawama
Polisi lawama
Simu kulipa miamala lawama
Ttzo letu wabongo tunapenda starehe uwezo wetu mdg tujipangeni upya maisha yamebadilika
Tujifunzeni kuishi kulingana na vipato vyetu rasivyo tutakua watu wa lawama kla sku
Wakati unasema wapunguze lawama ungeanza ku analyse watu wenye nyadhifa za kufanya monitoring & control wamefanya nini hadi sasa!
 
Hayo ndio mavuno ya viongozi wasio maono. Endeleeni kufungua nchi.
 
Watanzania mnaishia kulalamika
Kama bei ya Mafuta kupikia imepanda
Na yalianza kupanda muda
Sahv mnalalama tu bila ku take action,
Pikeni kuleni chukuchuku tu
Wenyewe watayashusha bei
Acheni utumwa na addiction mliyokuwa nazo

Ova
 
MaCCM yakielezea kuwa kuna matatizo ndiyo maana mafuta hayapatikani mtaani😁😁😁
 
Hata hao wanaolima hekari chache kuna saa wanakosa masoko ya uhakika hizo hekari nyingi wakishalima ndio watazipeleka wapi ?

Yaani tunataka mkulima awe Mtaalamu Kilimo, Mtaalamu wa Masoko , Financial Guru na vilevile speculator wa nini kitapanda bei saa ngapi ? (utagundua huyo sio mkulima per se bali ni an entrepreneur ambao majority hawawezi wakawa hivyo); Kwahio Wizara za Kilimo / Biashara n.k. ziwasaidie kwanza hawa waliopo kupata masoko ya uhakika
Masoko yapo kibao, na watu wanaweza kulima sana tu. kilichopo ni serikali kuwakataza kuuza nje ili bei iwe chini nchini. Matokeo yake wakulima wakubwa hawalimi na nchi inashindwa kujitosheleza. Sera kama hizo nchi nyingi waliziacha sababu zinaleta tu njaa, lakini hawa tunaita viongozi hawana kitu kwa kichwa.
 
Tukubali kuwa sisi ni nchi ya wapumbavu. Ukubwa wa nchi yetu ni mara tatu ya Malaysia. Lakini tunategemea mafuta ya kula toka Malaysia. Tz hii alizeti inaweza kulimwa kila kona. Kama inasitawi nchi kame kama Singida basi inaweza stawi popote. Msiba wa kujitakia huu.
 
Back
Top Bottom