Mafuta ya kupikia yaadimika mitaani

Mafuta ya kupikia yaadimika mitaani

Tanzania itakua ndio kimbilio la kila nchi yenye watu waliogoma kupungua uzito na unene

hivi unakuja Tanzania nchi hatuna mafuta tunakula michemsho tu dadadeki,unanenepaje

ndio mana siku hizi idadi ya watu wanene road imepungua,nikahisi labda mazoezi yamekubali

kumbe mama anapunguza watu mafuta mwilini,sio siri Tanzania patamu,mchina sasa hivi

anashusha makontena ya mafuta ya kupikia ndio mtajua hamjui Mpke wali na mafuta taa au mnunue mafuta yakupkia ya kichina...
 
Mafuta yapo tele ttzo Bei kila duka naona mafuta ila Bei ndio ishu mM ssh kashindwa hata kudhibiti mfumuko wa Bei yey anaweza nn jmn huyu bb wa Zanzibar Kaz kuchamba tu Ila Kaz hawezi na ujui ufatiliaji wa kuleta tija
 
Kuna watu wanamhujumu Mheshimiwa Rais na pengine yeye hajui hili. Kwa sasa huku mitaani mafuta ni adimu sana, na pale ambapo yanapatikana basi bei yake haishikiki. Dumu/Ndoo ya Lita 20 iliyokua ikiuzwa TZS 70,000/- mwezi wa sita mwaka jana leo inauzwa TZS 140,000/-

Aliekua Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alipata kusema kua sababu ya kupanda huku ni kuadimika Kwa vibarua huko Malaysia sababu ya COVID-19. Kigoma inaongoza Tanzania Kwa kuzalisha chikichi, je wameweza kuchukua mazao yote yanayozalishwa pale mpaka yakaisha imebidi waagize Malaysia sasa?

Kwanini wasi encourage na ku facilitate kilimo hiki Kwa hapa Tanzania mpaka tulazimike kuagiza nje? Singida wanalima sana Alizeti, na mikoa ya kusini wanalima sana Ufuta, je mazao haya yamechukuliwa yote na bado kukawa na upungufu wa mafuta?

Haya maeneo (Singida na Mikoa ya Kusini) bado kuna mapori mengi tu, kama wanazalisha malighafi za mafuta na bado hazitoshi kwanini Serikali isiwawezeshe basi kuongeza zaidi maeneo ya kulima kwenye hayo mapori yaliyobaki ili kuongeza zaidi malighafi hizi?

Sasa kuna Hussein Bashe kwenye hii Wizara, nilidhani ni mtu Smart lakin naona nae mfumo umemmeza, amesha adopt tabia za mfumo alioko. Juzi nimemsikia akiwa mkali kweli kweli juu ya kupanda Kwa mbolea kutoka 108,000/- Kwa gunia mpaka 140,000/-, lakini nimkumbushe tu hata hiyo 108,000/- bado tunapigwa, kwani hapo kabla ilikua haizidi 60,000/-

Mafuta Sasa hayako tena mitaani, wenye vigenge/duka wanasema Kwa yalivyopanda bei hata wakiyaleta hawajui watauzaje. Mafuta yanagusa kila mtu, isije ikawa ni bomu linategwa kwenye most consumable products ili likilipuka liguse sehemu kubwa ya watu. Zama hizi za "Kazi Iendelee" tunashuhudia mfumuko mkubwa wa Bei.
Tumia mafuta ya kitimoto utanishukuru
 
Nimepita pale kwa mangi majuzi kati namwambia Mangi nipe SUNDROP liter 1

ananiambia ni 10,000 ikabidi nishuke nimfate maana kuongea umekaa maskio hayaskii vyema

nikamfata tena mangi namwambia Mjomba sundrop sh ngapi,ananiambia Bwashee ni Buku Kumi tu

ikabidi tu nimuulize Mangi hivi hamna namna ya kupka ubwabwa bila kutumia Mafuta,akasema labda nioke

Hapa nipo Google naangalia namna ya kuoka Ubwabwa, ki ukweli anaenenepa Awamu hii ni Ana kiburi na kashindikana.
Pikia mafuta ya nazi.
 
Mafuta ni anasa,waongezee tu bei mpaka ifike laki tano ndoo la lita 10
Kwakweli usipo tia mafuta huwezi kufa,kuna vitu vya kuongelea ila sio mafuta, wazee wa zamani waliishi vipi?
Watu wa vijijini wanaishi vipi?

Mnawapa kichwa hawa jamaa ndio maana wanapandisha
Mkiona yanapanda suseni achen msinunue tuone kama watakuwa na jeuli,nasema tena mnawapa kichwa

Hivi unajua kama demu ukipenda kumsifia muda wote anakutunia,ndio kinachoendelea kwenye mafuta hebu suseni, karanga zipo, nazi zipo, nchi ina utajiri wa viungo bado mnalialia utafikiri mmenyimwa pumzi,kuweni serious basii,
Nani kakwambia vijijin hawatumii mafuta??.
Usije ukadhani siku hzi kuna vijiji kama vya zamani now days vijijin wanaishi maisha mazuri kuliko ata mjini utofauti ni maghorofa na Range Rovers za wahindi tu.
 
Kuna mnyama flani ana mafuta ya kutosha. Hamieni huku wenzenu muda mrefu tushahamia
 
Inabidi tujifunze kula michemsho sasa Hayo machemical yanayowekwa humo bora mchemsho au nazi tu,,,Sunflower oil mazuri kama ukitengeneza mwenyewe,Wanasema kila kitu ni kizuri kama ukiandaa mwenyewe!!!Organic Virgin Olive oil ndio mafuta mazuri sema hiyo bei yake sasa hahaha ila nayo sijui kama hayakosi chemical humo!
IMG_6102.jpg
 
Tunaingia kwenye Mfungo soon,
Huyu Mama naamini ni muumini mzuri tu wa dini yake, anaelewa umuhimu wa mfungo kwa kwa muumini, na umuhimu futari kwa aliefunga.

Chonde Chonde mama, fanya kitu angalau tufurahie mfungo. Hivi kweli kama tunafunga huku tunanung'unika bei za vyakula zimepanda itakua ni salama kweli kwa aliesababisha haya madhila?

Wewe kwa Nafasi yako kama Rais unaweza kuzuia hili, aliepita aliweza vipi wewe ushindwe? Jitahidi uzuie hili tatizo ili usionekane wewe ni either sehemu au chanzo cake.
 
Back
Top Bottom