Mzee wa Code
Member
- Sep 23, 2024
- 61
- 91
EWURA hii tabia ya wamiliki wa vituo vya mafuta kuuza nishati ya mafuta ya Petrol na Dizel kwenye madumu mtaikomesha lini huyu? Huyu kwenye picha ni mmoja kati ya Wananchi wanaonunua mafuta kwenye madumu katika Vituo vya Mafuta.
Watu kama hawa wanafanya manunuzi ya nishati hii katika Kituo cha Mafuta cha Puma hapa Dodoma Bahiroad, hatari zaidi amebeba mtoto mgongoni na mbaya zaidi amesafirisha mafuta haya kwa Pikipiki, na dereva Boda mwenyewe hajavaa kofia ngumu.
Jeshi la polisi kuna wakati linakuwa bize na dada poa na kuzuia maandamano lakini mambo kama haya awayaoni wala hawana muda wa kuzuia.
Safari hiyo ya huyu Dada hapo alielekea maeneo ya Iringa Road Maghorofani ambapo baadaye alifanya safari nyingine kwa kupakia madumu hayo kwenye gari la Abiria linalofanya safari za Iringa - Dodoma.
Akifika huko anakuwa anauza hayo mafuta kwa bei ya rejareja hasa kwa waendesha Bodaboda.
Natoa wito kwa EWURA, hivi mnasubiri siku watu waungue ndio mtoke ofisini kwa mtindo wa zimamoto kwa ajili ya kufanya ukaguzi?