KERO Mafuta ya Petroli kuuzwa kwenye madumu kisha kusafirishwa katika magari ya Abiria sio salama, EWURA -Dodoma mpo?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Uchawi sio mpaka uwe na magunguli hata hili ni uchawi. Huwezi kuuona umuhimu wa wauza mafuta kwenye makopo kama unakaa mjini ambalo kila mita 500 Kuna kituo. Huku bush tunatembea km 40 mpaka 60 ndo unakuta kituo Cha mafuta na Hawa wauzaji wanafanya boda ziishi kwahiyo acha ukuda.
 
Haijalishi ulitaka kufikisha ujumbe gani lakini umekosea sana kuweka hiyo picha ya bidada na mwanae na namba za usajili za pikipiki bila kuzificha, unaona wao wamefanya makosa lakini wewe umefanya makosa zaidi
 
Mods njooni mfute uzi huku au kuondoa picha,tabia mbaya ya kuanika sura za watu,Hata kama dada anachofanya ni hatarishi kwake na kwa wengine(kama amebeba mafuta na sio maji maana wanasheria wa jeiefu wakija hapa wanakupopoa mawe 🤣🤣 )lakini Kama unamjali kweli usingeweka uso wake hata ungeficha na mtoto wake pia.
Moderator
 
Hili suala lina utata sana.
Wauza petrol kwa vichupa ni hatari Sana kwao na watu wanao wazunguka.
Lakini Kuna watumiaji mashine mbalimbali za diesel na petrol ambazo hawawezi kuzibeba kwenda kujazia mafuta petrol filling station.
Utafutwe utaratibu mzuri siyo kuzuia tu kununua kwenye madumu bila vifaa mbadala.
 
Mnasomaga kujibu na kupinga tu eti..... Si amekwambia hapo mpaka kituo Cha mafuta alichonunua!!??..... Na vituo vya mafuta vyote vina camera ...haya mpeleke wewe mahakamani.....
 
Kabla hujaanza kuprovoke mamlaka juu ya kumchukulia hatua mtu fulani basi ni vyema kwanza kujua the reason behind!
 
Huyo ana kituo Cha mafuta ni wezi sana.wanaogopa sababu wanajua wakiweka umo utaona hayajafika kwenye kipimo vzr.
 
Ni suala linalohitaji muda siyo kukurupuka tu.
 
Hayo mahojiano yapo wapi akikuambia kanunua mafuta kituo cha puma?picha akiwa puma filling station? tutaangalie wapi kwenye ayo madumu kujua kama yamebeba mafuta au maji? We unawachafua hao Puma, kingine hata kama nikweli ulitaka abebe jenereta aje nalo hapo kituo cha mafuta?
 

Huo mda na nguvu zako ungetumia kujua hicho kijiji na kuwasogezea kituo cha mafuta, ungekua mtu wa maana sana, ila sio hicho ulichofanya.
 
We ni fala, kama unalipwa mshahara wa bure hapo ulipo maana muda wa umbeya sijui unautoa wapi mtoto wa kiume.
 
Ukiona hivi ujue mtoa mada hamiliki hata bodaboda..😁😁

Maana ingekuwa anamiliki chombo chochote cha moto kinachotumia mafuta asingeweza kuandika alichoandika sababu angeweka akiba ya maneno kwamba ipo siku angepatwa na dharula ya hiyo nishati sehemu ambayo haina kituo cha mafuta karibu na angeagiza bodaboda akamletee hiyo nishati kwenye dumu kama hivyo kwenye picha ili maisha yaendelee.
 
Reactions: apk
Tafuteni jerry can
Ndiyo mtumie

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…