Mafuta ya Safi na Korie yanatokana na Alizeti gani inayoganda?

Safi na korie sio alizeti
Ni mawese toka Thailand
Wanaleta toka nje wanakuja kusafisha wanapack
Soma hata package zao hazijaandikwa alizeti
Sawa kabisa na yameandikwa kabisa kuwa ni mawese. Na yale ya alizeti inaitwa korie sundrop( sunflower )
 
Hivi ile michikichi ya JPM na Majaliwa wakati wanaingia madarakani iliishia wapi? Nakumbuka walisema mbegu za muda mfupi. Sasa mpaka leo hawajaanza kuvuna na kuzalisha mafuta?
 
Habari za mda huu!

Naenda kwenye mada fupi tu. Nimetaja mafuta hayo sababu common sana kwa wengi wetu. Ila kuna mafuta mengi yapo mtaani ambayo yanaganda.

Na uhakika wa haya mafuta kuwa yanaganda kwa asilimia 100. Na mafuta haya utengenezwa na alizeti kwa mujibu wa watengenezaji, ila ukweli hamna mafuta ya alizeti yanayoganda. Pia mafuta mengi ya mimea huwa hayagandi.

Mafuta yanayoganda ni ya wanyama ambayo ni hatari sana kwa mlaji. Sasa nauliza hata kama ni wanyama wanapata wapi kiasi kingi hivi? Au ni ya nyangumi? Haya nimawazo yangu ila natamani sana kujua haya mafuta yanatokana na nini?
Korie ni mawese., period
 
nilinunua hayo mafuta wanadai n alizeti ahsee nimekaa nayo kama mwez ivi nakuta kweny kidum yameganda yote kama baraf vile
Nikaon nigawe tu Maan duh hata kuyamimina kutok kweny dumu n kazi yan mpka uyaanike ahse!
Kwa hiyo ukawagawia wengine ili wafe au sio, kwa nini hukuya-dispose tu??
 
Sawa kabisa na yameandikwa kabisa kuwa ni mawese. Na yale ya alizeti inaitwa korie sundrop( sunflower )
Ni hivi kiwanda cha kuzalisha korie kinaitwa murzah nadhani
Kinazalisha pia mafuta ya alizeti yanaitwa sundrop
So kuna mafuta ya kawaida yanaitwa korie pia ya alizeti yanaitwa sundrop
Yanatoka kampuni moja
 
Habari za mda huu!

Naenda kwenye mada fupi tu. Nimetaja mafuta hayo sababu common sana kwa wengi wetu. Ila kuna mafuta mengi yapo mtaani ambayo yanaganda.

Na uhakika wa haya mafuta kuwa yanaganda kwa asilimia 100. Na mafuta haya hutengenezwa na alizeti kwa mujibu wa watengenezaji, ila ukweli hamna mafuta ya alizeti yanayoganda. Pia mafuta mengi ya mimea huwa hayagandi.

Mafuta yanayoganda ni ya wanyama ambayo ni hatari sana kwa mlaji. Sasa nauliza hata kama ni wanyama wanapata wapi kiasi kingi hivi? Au ni ya nyangumi? Haya nimawazo yangu ila natamani sana kujua haya mafuta yanatokana na nini?
Kwahiyo palm ni alizeti!
 
Kwa hiyo ukawagawia wengine ili wafe au sio, kwa nini hukuya-dispose tu??
Kwanza si mara ya kwanza kuona haya mafuta yaliyoganda kwa watu wengin ila Kwang ndio ilikuw mara ya kwanza kukutana nayo mimi kama mm so sikujua athari zake na pia sikuyapenda tok yaanze kukanda.
So kipind nipo kweny process za Kuya dispose wadau wang wengin wakayaomba kwamb wao huwa wanatumia ko nisiya tupe. ningefanyej sasa,??
 
Mafuta ya alizeti huganda au kuwa na mnato mzito kutokana na sababu kadhaa.
Joto la chini – Mafuta ya alizeti yana kiwango fulani cha mafuta yaliyojaa (saturated fats), ambayo yanaweza kuganda au kuwa mazito yanapowekwa kwenye halijoto ya chini, hasa chini ya 10°C.

Kutokuwa na usafishaji wa viwandani – Mafuta yasiyosafishwa vizuri au yaliyoandaliwa kwa njia ya asili (cold-pressed) huwa na sehemu nyingi za asili ambazo zinaweza kuganda haraka ikilinganishwa na mafuta yaliyosafishwa viwandani.

Mchanganyiko wa mafuta – Ikiwa mafuta ya alizeti yamechanganywa na mafuta mengine yenye kiwango kikubwa cha mafuta yaliyojaa (kama vile mafuta ya mawese), yanaweza kuganda kwa urahisi.

Uhifadhi usiofaa – Mafuta yanapohifadhiwa kwenye mazingira yenye unyevunyevu au kwenye vyombo visivyofaa, yanaweza kubadilika muundo na kuonekana kama yameganda.
 
Habari za mda huu!

Naenda kwenye mada fupi tu. Nimetaja mafuta hayo sababu common sana kwa wengi wetu. Ila kuna mafuta mengi yapo mtaani ambayo yanaganda.

Na uhakika wa haya mafuta kuwa yanaganda kwa asilimia 100. Na mafuta haya hutengenezwa na alizeti kwa mujibu wa watengenezaji, ila ukweli hamna mafuta ya alizeti yanayoganda. Pia mafuta mengi ya mimea huwa hayagandi.

Mafuta yanayoganda ni ya wanyama ambayo ni hatari sana kwa mlaji. Sasa nauliza hata kama ni wanyama wanapata wapi kiasi kingi hivi? Au ni ya nyangumi? Haya nimawazo yangu ila natamani sana kujua haya mafuta yanatokana na nini?
mafuta ya kondoo wa mturuki
 
Serikali ifanye mchakato wa kuzalisha mafuta hapa hapa nchini haya mambo ya kuagiza mafuta ya kupikia wakati tuna alizeti na mawese ya kutosha ni miyeyusho matokeo yake binti mdogo anaonekana kama mshangazi.
Serikali gani? Serikali hii chovu isiyoweza hata kuendesha bandari ndiyo itaweza kulima? Wananchi nao ni wavivu wamebaki kukata viuno tu.
 
Iko hv , mafuta yote tunayotumia hap nchini na dunia kwa ujumla kwa kupikia ukitoa mafuta ya alizeti ,yote yanatokana na mawese (palm fruit).
Japo kuwa Kuna canola oil, soybean oil n.k haya hayatumiki Africa Sana .
Sasa hayo mafuta ya korie yanaganda kwa sababu ifutayo.
1. Cloud point (cp).
Is the temperature at which a liquid begin to form cloudy or wax crystals.
Ni jotoridi ambayo kiminika huanza kuganda.
Mafuta ya mawese ambayo hayachakatwa Wala kusafishwa(CPO), huwa yanapitishwa kweny mashine ambapo huchanganywa na kemikali tofaut tofaut(swez kuztaja zote maelezo yatakuwa marefu) ili kupata mafuta yaliyo Safi (Refined (RBD)palm oil), hvyo Basi katika mashine huwa yana-sort-iwa Ima yawe cp6 au cp10 au cp8, hii Ni kumaanisha yaanze kuganda au kutengeneza cloud katika temperature ipi? Ima 8celcius au 6celcius au 10celcius.
Hvyo kuganda inategemea umehfadh wap na mafuta yako Yana cloud point ngap, Mara nyng Tanzania tunatumia cp10.
2.RBD palm olein au RBD palm oil.
Pia kuganda inategemea mafuta yako yamefkia stage gani ya kusafishwa (refinery) , RBD palm olein haya Ni mafuta ambayo yamesafshwa hayana RBD stearin,hii ndo inasababsha kuganda sababu huwa Ni solid at room temperature, na hutolewa kutoka kweny RBD palm oil kwa fractionation ili ikatumike kutengeneza margarine (samli).
RBD palm oil haya ndo ambayo huganda sababu yanakuwa hayajafanyiwa fractionation , lakn RBD palm olein hagandi kamwe mpka ifkie Ile cp yake.
 
Habari za mda huu!

Naenda kwenye mada fupi tu. Nimetaja mafuta hayo sababu common sana kwa wengi wetu. Ila kuna mafuta mengi yapo mtaani ambayo yanaganda.

Na uhakika wa haya mafuta kuwa yanaganda kwa asilimia 100. Na mafuta haya hutengenezwa na alizeti kwa mujibu wa watengenezaji, ila ukweli hamna mafuta ya alizeti yanayoganda. Pia mafuta mengi ya mimea huwa hayagandi.

Mafuta yanayoganda ni ya wanyama ambayo ni hatari sana kwa mlaji. Sasa nauliza hata kama ni wanyama wanapata wapi kiasi kingi hivi? Au ni ya nyangumi? Haya nimawazo yangu ila natamani sana kujua haya mafuta yanatokana na nini?
Ukiona mafuta ya kiwandani yanaganda then jua wametengeneza kwa kutumia artificial materials kupata product.

Mafuta ya asili ya mimeo huwa hayana tabia ya kuganda.
 
Habari za mda huu!

Naenda kwenye mada fupi tu. Nimetaja mafuta hayo sababu common sana kwa wengi wetu. Ila kuna mafuta mengi yapo mtaani ambayo yanaganda.

Na uhakika wa haya mafuta kuwa yanaganda kwa asilimia 100. Na mafuta haya hutengenezwa na alizeti kwa mujibu wa watengenezaji, ila ukweli hamna mafuta ya alizeti yanayoganda. Pia mafuta mengi ya mimea huwa hayagandi.

Mafuta yanayoganda ni ya wanyama ambayo ni hatari sana kwa mlaji. Sasa nauliza hata kama ni wanyama wanapata wapi kiasi kingi hivi? Au ni ya nyangumi? Haya nimawazo yangu ila natamani sana kujua haya mafuta yanatokana na nini?
kakudanganya nani mafuta ya wanyama ndio hatari?mafuta hatari kwa afya yako ni hayo mafuta ya mbegu yakiwemo ya alizeti ukiona unakula nyama inakudhuru sio kwa sababu ya yale mafuta ya kwenye nyma bali ni yale mafuta unayoyapaka kwenye nyama wakati unachoma lakini nyama ukichoma kwa mafuta yake hayana madhara yoyote.
 
Elimu ya Afya imepinduka kabisa. Wengine leo wanasema Nafaka ndiyo mbaya kuliko nyama, tafiti nazo zinadi seed oils ni mbaya afadhali mafuta ya wanyama. Lakini wamasai ni ushahidi hai.
 
Watu wanakula nyama tu maisha yao yote na wanaishi miaka 100 leo ukatuambie mafuta ya wanyama hatari wanatangaza biashara zao tu.
 
kakudanganya nani mafuta ya wanyama ndio hatari?mafuta hatari kwa afya yako ni hayo mafuta ya mbegu yakiwemo ya alizeti ukiona unakula nyama inakudhuru sio kwa sababu ya yale mafuta ya kwenye nyma bali ni yale mafuta unayoyapaka kwenye nyama wakati unachoma lakini nyama ukichoma kwa mafuta yake hayana madhara yoyote.
yaani watu wengi wamekaririshwa hv, sijui mjinga gani alileta hii nadharia
plants oils are heat labile, easily produce free radicals and other oxidants which are extremely harmful to our healthy compared to animal oil which are heat stable.
sasa kuna mjinga mmoja alileta hii nadharia kua plants oil ar safe and animal oil is harmful, basi imekua wimbo.
 
Back
Top Bottom