Yapo madai ya kuwa dawa za asili kama ndulele, alovela na vitunguu swaumu ni dawa ambazo huweza kutibu tatizo la mdudu wa kidole. Aidha, wengine wanadai mafuta ya taa au maji ya betri pia huweza kutibu mdudu wa kidole.
Ukweli ni upi?
Ukweli ni upi?
- Tunachokijua
- Ugojwa wa mdudu wa kidole (paronychia) ni kitu gani?
Katika mila na desturi zetu ugonjwa wa paronychia umezoeleka kuitwa mdudu wa kidole. Katika mila na desturi hizi, inaaminika kuwa kuna mdudu ameingia kwenye kidole, mara nyingi chini ya ukucha, ambaye anasababisha kidole husika kikumbwe na maumivu makali sana.
Hata hivyo katika taaluma ya tiba hali haiko hivyo. Kilichoko ni kwamba ni kweli kidole kinakumbwa na maambukizi, lakini maambukizi yenyewe siyo ya mdudu unayeweza kumwona kwa macho, na pia siyo maambukizi ya aina moja.
Kitaalamu paronychia ni aina za maambukizi kwenye kidole yanayopelekea kuzaliwa kwa maumivu makali yako aina tano tofauti. Mara nyingi maambukizi husika hutokana na bakteria, isipokuwa aina moja tu. Aina hii ni ile inayojulikana kama Herpetic whitlow, ambayo husababishwa na kirusi.
Kwa kawaida ili maambukizi yatokee ni lazima kwanza kuwe na jeraha. Jeraha linaweza kuwa ni la kujikata, kung’atwa na mdudu, au kujitoboa.
Matibabu
Kihospitali, maambukizi takriban yote ya kidole hutibiwa kwa vijaua vijasumu (antibiotics) na uangalizi sahihi wa jeraha katika eneo lililoathirika. Uangalizi sahihi wa jeraha utatofautiana kulingana na aina ya maambukizi yanayohusika.
Uangalizi huu unaweza kuwa ule mwepesi kabisa kama kutoboa kidogo na kukamua hadi usaha wote umalizike, hadi ule ambao unahusisha upasuaji wa kina wenye nia ya kuondoa sehemu kubwa ya tishu zilizoambukizwa kadri inavyowezekana.
Baadhi ya haya maambukizi hutibiwa na mgonjwa kuruhusiwa kurudi nyumbani, lakini mengine yanaweza kuhitaji mgonjwa kulazwa na kupewa vijaua vijasumu kwa njia ya dripu.
Aidha, kutoa uchafu kwa kufanya upasuaji mdogo inaweza kusaidia pia kutibu changamoto hii.
Matibabu kwa njia za kiasili
Unaweza kuwa na uwezo wa kutibu kisa kidogo cha paronychia nyumbani. Matibabu mara nyingi huhusisha kusafisha eneo lililoathirika na kulifunga dawa. Ziko dawa nyingi zinazotumika kwa kazi hiyo lakini moja ambayo ni mujarabu sana ni kutumia kitunguu saumu. Kitalamu inaelezwa kuwa kitunguu ni moja kati ya zao lenye Vijasumu vingi.
Hivyo, baada ya eneo husika kusafishwa vizuri kidole chote huzungushiwa kitunguu kilichopondwa na kushikanishwa hapo kwa bandeji. Dawa hii inaweza kumsaidia mgonjwa kupoa kabisa ndani ya saa 24 tangu aanze kuumwa.
Ikiwa hautapata matokeo mazuri baada ya siku moja au mbili za kujaribu kujitibu nyumbani, nenda kituo cha afya ili liangaliwe kitaalamu zaidi.
Mafuta ya taa na ndulele ni dawa zingine za kiasili zinazotajwa kuwa na uwezo wa kuponyesha tatizo hili.