Gentleman,
Kua tajiri au maskini Tanzania ni uamuzi wako binafsi. Na kua mvivu au mchapakazi mwenye bidii ni hiyari yako mwenyewe.
Ni wapi wavivu duniani hawateseki gentleman? Mbona kuna waTanzania wengi sana walikua na fikra za kuteseka kama zako, wakafanya ujanja unjanja kwa kujidanganya eti ulaya na Amerika hakuna mateso.
Walipofika huko,
waliishia kuogesha mbwa, kumenya vitunguu na kuosha masufuria kwenye mahoteli na mahospitali ya huko. Matokeo yake wamerudi nyumbani kimya kimya wakiwa wametulia tuli, na wengine wamekimbilia kwenye siasa hivi sasa, kuficha fedheha na mateso waliokumbana nayo huko ughaibuni.
So,
ni muhimu sana kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujikomboa na kutoka kwenye unyonge wa kiuchumi na kuondokana na fikra potofu kama hizo za kujidanganya eti kuna mtu mahali fulani atakuja kuondoa mateso ya maisha yako yanayo tokana na uvivu wako 🐒