Mafuta yashuka bei baada ya makubaliano ya USS na Iran. Subiri, hapa Malawi yatapanda

Huku Bongo chini ya huu utawala tutaendelea kuteseka sana

Sijui machawa akina Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah wanalisemeaje hili
Gentleman,
Kua tajiri au maskini Tanzania ni uamuzi wako binafsi. Na kua mvivu au mchapakazi mwenye bidii ni hiyari yako mwenyewe.

Ni wapi wavivu duniani hawateseki gentleman? Mbona kuna waTanzania wengi sana walikua na fikra za kuteseka kama zako, wakafanya ujanja unjanja kwa kujidanganya eti ulaya na Amerika hakuna mateso.

Walipofika huko,
waliishia kuogesha mbwa, kumenya vitunguu na kuosha masufuria kwenye mahoteli na mahospitali ya huko. Matokeo yake wamerudi nyumbani kimya kimya wakiwa wametulia tuli, na wengine wamekimbilia kwenye siasa hivi sasa, kuficha fedheha na mateso waliokumbana nayo huko ughaibuni.

So,
ni muhimu sana kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kujikomboa na kutoka kwenye unyonge wa kiuchumi ambao ndio unachochea fikra potofu na duni kama hizo za kujidanganya eti kuna mtu mahali fulani atakuja kuondoa mateso ya maisha yako yanayo tokana na uvivu wako mwenyewe .

Mungu Ibariki Tanzania πŸ’
 
Hujajibu swali bosi
wanauliza kama bei ya mafuta itakapo rudi kama ilivyokuwa kabla ya vita ya Iran/ Marekani na hapa nyumbani bei itashuka hivyo hivyo au kuna..........watatembea na hiyo gap?
 
Hujajibu swali bosi
wanauliza kama bei ya mafuta itakapo rudi kama ilivyokuwa kabla ya vita ya Iran/ Marekani na hapa nyumbani bei itashuka hivyo hivyo au kuna..........watatembea na hiyo gap?
Gentleman,
huyupo duniani wa kudhibiti bei ya mafuta kushuka au kupanda. Hali hiyo hubadilika yenyewe kulingana na uzalishaji, upatikanaji na usafirshaji wa huduma hiyo yenyewe na kulingana na utaratibu wa soko la dunia.

Bei ya pipa la mafuta kutoka yanapozalishwa na kuuzwa ikupanda leo, basi bei hiyo itapanda vivyo hivyo duniani kote kwa mafuta yote yatakayozalishwa leo. Bei ya pipa la mafuta likishuka bei kesho, itashuka vivyo hivyo duniani kote kwa mafuta yatakayozalishwa na kusafirishwa kesho,

kue na vita ama vinginevyo,
kuikamata bei ya mafuta na kung'ang'ania nayo ni stori ingine kabisa πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…