Mkuu hio unayosema wewe sio 7 series, io ni 5 series, 7 series ni kama 745i 745li 750, yaani ianze 7 ndio 7 series, i think umekusudia 745i, mkuu hizi gari zitakupa attention kutoka kwa watu sana tu, hata mwenye mark x new model ni cha mtoto kwako atakuwa, mana hii gari ni kama upo ndani ya ndege. ila wenyewe wanasema ni vyema ukatafuta za mwakaa 2004 kupanda juu, 2002 zimekuwa na matatizo mengi hasa kwenye idrive yake ambayo sana ndio inatumika kucontrols vitu vya ndani. Ukiwa nayo ujitaarishe kuishughulikia, ni zaid ya mke hio. Oil yake tu ya afadhali si chini ya 200,000, ukiweka izi za kila sik za buku 50 gari unaielekeza kwenye kaburi. Uzur wa toyota ni very easy kurepair, yani vitu vingi unaweza repair juu juu bila kufungua engine, ila hio 7 series ndugu, na hasa za 2002 zina ishu ya kuvuja maji, kuifix mpaka ufungue header i think, na hio repair kit yake, juzi niliona moja ambayo sio official recommended na BMW wenyewe ina cost kama $1500, hio ni ki pipe tu cha kupitisha maji. Wakati toyota pengine water pump laki 1 tu!
Ingekuwa BMW reliability yake ni kama toyota na parts zake ni cheap, amini mungu haikusimamii 15m, labda 25 au 30m mana kitu kiachwe tu tena. mimi BMW zinanimaliza luxury features zake tu