Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Mpaka miaka ya hivi karibuni mambo ya uchumba yalikuwa hayawezi kufanyika bila ya kuwepo wazazi na familia zote mbili. Mitoko (dates) mingi na kualikana ilifanyika majumbani wakiwepo wanafamilia wote.
Kujitokeza kwa familia nyingi za kipato cha kati na vijana wengi wa umri wa kati kumiliki magari kumesaidia sana kuharibu utaratibu mzuri wa mitoko ya kimapenzi na uchumba kwa ujumla.
Magari si tu kwamba yamesababisha mitoko isifanyike majumbani, lakini pia yamesababisha ifanyike bila kuwashirikisha wazazi. Magari siku hizi yamebadilishwa kuwa vitanda vinavyotembea vinavyotumika kufanyia ngono kiholeala wakati wa mitoko.
Vijana wadogo sio kwa hapa nchini tu bali hata huko katika nchi za magharibi na ulaya wamejinyakulia uhuru mkubwa mno kutoka kwa wazazi wao, na kuzipondoponda chini mila na desturi ambazo ziliweka misingi imara katika kulinda maadili ya uchumba kwa vijana.
Lakini pia Teknolojia mpya na matumizi yake mabaya nayo imechangia kwa kiasi kikubwa kusambaratisha mila na desturi zetu zilizokuwa zikilinda maadili yetu. Simu na mitandao ya mawasiliano, ni moja ya mabadiliko yaliyotufikisha hapa. Siku hizi vijana wamegeuza mitandao kama vijiwe vya kukutania na kutongozana kimya kimya.
Ule uhakika wa mzazi kumuona binti yake akiwa nyumbani ametulia akiamini yuko salama, ni kujidanganya bure, kwani wakati mzazi akiamini hivyo binti kwa kutumia teknolojia ya intenet inayopatikani kirahisi katika simu za mkononi anatongozwa na kufanya miadi ya kufanya ngono mbele ya wazazi wake na wasijue.
Siku hizi maadili ya kumpata mwenza yamewekwa kisasa zaidi, zile taratibu za kuchunguza familia atokako mke au mume, kwa ajili ya kujiridhisha kama binti anaolewa katika familia sahihi, au kijana wa kiume anaoa katika familia sahihi, hazipo na badala yake vijana wa siku hizi wanachukuana tu, na ndio maana ndoa hazidumu, watoto hawana adabu, kutoka nje ya ndoa kusiko na simile, na kila aina ya uchafu, ili mradi fujo tu.
Je wazazi nini Kifanyike?
Weka mtazamo wako hapa kuokoa kizazi hiki cha DOT COM.
AshaDii, Kongosho, BADILI TABIA, snowhite, Fixed Point, gfsonwin, cacico, Kaunga, Preta, ICHANA, MankaM, KOKUTONA, Asprin, KakaKiiza, Jiwe Linaloishi, Ruttashobolwa, Kaizer, watu8, The Boss, Nyani Ngabu, Kiranga, Thomas Odera, KIBANGA, Elli, ayanda, mayenga, Eiyer, Ennie, sister, Ennie, Paloma, Nivea, Neylu

Attachments
Last edited by a moderator: